Amani iwe nanyi wadau,
Hali ya bara ya Ulaya na Asia sio nzuri kwa sasa, Urusi anaonesha ubabe wa waziwazi kwa kuanza kurudisha maeneo ya uliokuwa Umoja wa nchi za kisovieti.
Wiki hii imeanza kwa moto baada ya Rais Putin kutangaza kuyatambua maeneo ya Donesk na Luhansk kuwa nchi huru ikiwa ni harakati za kutwaa majimbo haya kutoka nchi ya Ukraine.
Haya yakiendelea inaonekana nchi za Marekani na Washirika wake wa Magharibi hasa NATO (Nchi za Ufaransa, Ujerumani, Uingereza na nyinginezo) hawataki vita zaidi ya kumdhoofisha Urusi kiuchumi ili afe kiuchumi
Njia kuu inayotumika na inayotarajia kutumika kwa sasa katika kumdhoofisha Urusi kiuchumi ni kwa kuacha utegemezi wa gesi ya Urusi na ikumbukwe kuwa Urusi ndo nchi inayotegemewa hasa na nchi za Ulaya kwa usambazaji wa gesi
Kwa Ulaya Gesi ndo hitaji kuu la nishati kwa sababu ya Baridi kali ambayo inawafanya wategemee zaidi Gesi kwa ajiri ya kupikia na mahitaji mengine.
Jana usiku Kansela wa Ujerumani ametangaza kusitisha mpango wa Bomba la Gesi kutoka Urusi kuingia Ujerumani na kwenda nchi zingine za Ulaya huku Mataifa mengine ya Ulaya na Marekani wakiweka vikwazo vikali dhidi ya Rais Putin na mabenki yake.
Kwa sasa inaonekana nchi za Ulaya zimeanza kutupa macho kwa Tanzania kwa sababu ndo imeonekana kuwa nchi yenye siasa nzuri na yenye hifadhi kubwa ya Gesi ambayo wanaweza kuinunua na kuitumia baada ya kuachana na Urusi
Jarida Maarufu la kiuchunguzi The African Report limeandika makala hii jana
Baada ya kuona hali hii niliyoielezea hapo juu naona sasa Wazungu wako serious mradi wa LNG uanze haraka hapa Tanzania ili waachane na Urusi mazima.
Taarifa iliyotolewa na kampuni iliyo kwenye mazungumzo na Serikali ya Tanzania katika mradi huu ya Shell kuwa wako kwenye sehemu nzuri kimazungumzo na Tanzania kwa ajiri ya mradi wa LNG kuanza naona imekaa ki strategy zaidi kwa ajiri ya kuwatuliza wananchi wa Bara la ulaya ambao hadi sasa hofu yao kuu ni Maisha yatakuwaje bila Gesi ya Urusi?
Napenda kuipongeza serikali ya Tanzania kwa hatua waliyofikia kwenye mazungumzo ya uwekezaji mkubwa wa Gesi huko Lindi na Mtwara na napenda kuwahusia tu kikubwa ni kuwa hakikisheni tu nchi yetu inafaidika massively kiuchumi kutokana na huu mradi.
Kwa Rais Samia napenda kusema unaanza kusomeka kwenye ramani ya Dunia. LNG ndo main legacy yako, ukicheza vizuri hapa umaskini itakuwa historia Tanzania na utakumbukwa milele kama The best President ever to happen in Tanzania!
Muwe na siku njema!
View attachment 2128208