Mradi wa LNG: Tukicheza Vizuri wakati huu ni hakika Umasikini tutausahau Tanzania na Samia anaweza kuwa Rais Bora zaidi kuwahi kutokea Tanzania

Mradi wa LNG: Tukicheza Vizuri wakati huu ni hakika Umasikini tutausahau Tanzania na Samia anaweza kuwa Rais Bora zaidi kuwahi kutokea Tanzania

Amani iwe nanyi wadau,

Hali ya bara ya Ulaya na Asia sio nzuri kwa sasa, Urusi anaonesha ubabe wa waziwazi kwa kuanza kurudisha maeneo ya uliokuwa Umoja wa nchi za kisovieti.

Wiki hii imeanza kwa moto baada ya Rais Putin kutangaza kuyatambua maeneo ya Donesk na Luhansk kuwa nchi huru ikiwa ni harakati za kutwaa majimbo haya kutoka nchi ya Ukraine.

Haya yakiendelea inaonekana nchi za Marekani na Washirika wake wa Magharibi hasa NATO (Nchi za Ufaransa, Ujerumani, Uingereza na nyinginezo) hawataki vita zaidi ya kumdhoofisha Urusi kiuchumi ili afe kiuchumi

Njia kuu inayotumika na inayotarajia kutumika kwa sasa katika kumdhoofisha Urusi kiuchumi ni kwa kuacha utegemezi wa gesi ya Urusi na ikumbukwe kuwa Urusi ndo nchi inayotegemewa hasa na nchi za Ulaya kwa usambazaji wa gesi

Kwa Ulaya Gesi ndo hitaji kuu la nishati kwa sababu ya Baridi kali ambayo inawafanya wategemee zaidi Gesi kwa ajiri ya kupikia na mahitaji mengine.

Jana usiku Kansela wa Ujerumani ametangaza kusitisha mpango wa Bomba la Gesi kutoka Urusi kuingia Ujerumani na kwenda nchi zingine za Ulaya huku Mataifa mengine ya Ulaya na Marekani wakiweka vikwazo vikali dhidi ya Rais Putin na mabenki yake.

Kwa sasa inaonekana nchi za Ulaya zimeanza kutupa macho kwa Tanzania kwa sababu ndo imeonekana kuwa nchi yenye siasa nzuri na yenye hifadhi kubwa ya Gesi ambayo wanaweza kuinunua na kuitumia baada ya kuachana na Urusi

Jarida Maarufu la kiuchunguzi The African Report limeandika makala hii jana

Baada ya kuona hali hii niliyoielezea hapo juu naona sasa Wazungu wako serious mradi wa LNG uanze haraka hapa Tanzania ili waachane na Urusi mazima.

Taarifa iliyotolewa na kampuni iliyo kwenye mazungumzo na Serikali ya Tanzania katika mradi huu ya Shell kuwa wako kwenye sehemu nzuri kimazungumzo na Tanzania kwa ajiri ya mradi wa LNG kuanza naona imekaa ki strategy zaidi kwa ajiri ya kuwatuliza wananchi wa Bara la ulaya ambao hadi sasa hofu yao kuu ni Maisha yatakuwaje bila Gesi ya Urusi?

Napenda kuipongeza serikali ya Tanzania kwa hatua waliyofikia kwenye mazungumzo ya uwekezaji mkubwa wa Gesi huko Lindi na Mtwara na napenda kuwahusia tu kikubwa ni kuwa hakikisheni tu nchi yetu inafaidika massively kiuchumi kutokana na huu mradi.

Kwa Rais Samia napenda kusema unaanza kusomeka kwenye ramani ya Dunia. LNG ndo main legacy yako, ukicheza vizuri hapa umaskini itakuwa historia Tanzania na utakumbukwa milele kama The best President ever to happen in Tanzania!

Muwe na siku njema!
View attachment 2128208
Hiyo gas unayojivunia life time yake wakiamua kuichimba yote ni miaka mingapi? Na je ikiisha hiyo LNG plant itabaki na kazi Gani?
 
Mzilankende mnyago...mtu ovyo kuwahi kutolea tangia dunia iumbwe
Mama anaenda vizuri sana na LPG👇

Screenshot_20220223-122555.png
 
Kama kawaida ya wabongo mwekezani 87% tz 3% kuendelea kusikieni bombani ndugu.
 
Kama kawaida ya wabongo mwekezani 87% tz 3% kuendelea kusikieni bombani ndugu.
Ndio hivyo unataka upate kingi wakati hujatafiti na hujaweka chochote hapo kwenye mradi.

Ukiacha hiyo share ila kuna ajira,Kodi na faida zingine mtambuka.

Kumbuka til.70 hizo sio pesa ya serikali ni ya investors.
 
Kati ya mambo ya hovyo kabisa yaliyowahi kufanywa na marehemu Rais Magufuli, kiasi cha watu tunaoelewa kujiuliza kama kweli Rais alikuwa katika utimamu wa akili, ni kuhusu gas.

Mradi wa gas ya Tanzania, kama ungeendelezwa pale alipoachia Kikwete, umaskini wa Tanzania ungekuwa historia. Lakini Magufuli alivuruga kila kitu. Uwekezaji wa dola bilioni 30 ukapotea. Uwekezaji ule ukapelekwa Msumbiji. Wakawekeza dola bilioni 28, ukawa ndio uwekezaji wa pili kwa ukubwa Duniani.

Marehemu akawalisha uwongo, na ujinga wa hali ya juu, watu wasio na uelewa, eti gas ya Tanzania imeuzwa kwa Wachina wakati hakuna kampuni yoyote ya China inayomiliki kitalu hata kimoja cha utafiti gas, Tanzania. Lakini huyu bwana akaropoka hivyo, na wapo waliomwona ni shujaa. Na haikueleweka inakuwaje mtu mwenye akili timamu angeweza kuripoka maneno ya uwongo kiasi kile.

Nchi ya kwanza kwa utajiri Duniani, Qatar, utajiri wake unatokana na gas.

Gas ya Tanzania ingechimbwa na kujengewa LNG, mapato yako, ukilinganisha na mapato yatokanayo na mauzo ya dhahabu inayochimbwa kwa sasa, ya dhahabu ni sawa tone la maji katika Ziwa. Ndiyo maana Prof. Muhongo wakati ule alikuwa akisema kuwa, "Tunaongelea Tanzania ya uchumi wa gas". Naye Kikwete akasema, "mimi nitakuwa Rais wa mwisho kuongoza Tanzania maskini". Marehemu akaiporomosha Tanzania kwa kiwango ambacho hata tungempa mtu wa darasa la saba, awe Rais lakini awe msikivu, asingefanya uharibifu alioufanya marehemu kwenye uchumi wa Tanzania.

Rais Samia hawezi kuwa the best President, but is much better, na Tanzania inaweza kubadilika kabisa kipindi chake, alimradi awe msikivu, ajifunze, na watu wa kumfundisha, wapo. Hili suala la gas, ni time opportunity. Na kwenye hili, kama tunaongelea uchumi wa gas, Rais Samia alistahili kumpa uwaziri Prof. Muhongo, na siyo January. Sisemi haya kwa kumchukia January au kumpendelea Muhongo lakini kwa kuzingatia ukweli wa uelewa kwenye sekta hii, na ambacho kilikuwa kimefikiwa kabla ya marehemu kuvuruga kila kitu.
Unadhani tatizo la marehemu lilikuwa ni nini haswa?. Kutaka ionekane watangulizi wake kwamba hawajafanya kitu na ni madalali wa mabeberu? Ubishi tu na ukaidi?. Au kuna alichokijua ambacho sisi hatukijui?.
 
Ila wabongo dah! Kuna watu hadi bado wanamlaumu Nyerere na wengine hadi sasa bado wanamlaumu Magufuli kana kwamba bado anaongoza nchi.
 
Unadhani tatizo la marehemu lilikuwa ni nini haswa?. Kutaka ionekane watangulizi wake kwamba hawajafanya kitu na ni madalali wa mabeberu? Ubishi tu na ukaidi?. Au kuna alichokijua ambacho sisi hatukijui?.
Hoja zao zinahoja kwa upande fulani
 
Kwa iyo unapingana na wachambuzi mahiri The African Report?

Unaonekana hata Elimu yako ni mashaka, kuna uhusiano gani kati ya LNG na Umeme au Bwawa la Nyerere?

Nani kakwambia LNG inatumia pesa za serikali?
Hilo African report ni kati ya majarida yasiyoamika duniani,lipo kisiasa zaidi.Na pia hiyo LNG unayoiongelea hujui kuwa ina wamiliki wake tofauti kabisa na sirikali ?Sasa sisi tutanufaika vipi zaid ya kuingizwa mjini kwa mara nyingine na wapigaji kwa kuwajengea miundombinu?
Tatu,sie wenyewe tumeshindwa kuileta Dar kwa matumizi ya kawaida tutaweza kuipeleka ulaya?
Na mwisho epuka propaganda za west ndugu
 
Tupe uthibitisho wa kutoaminika kwa jarida la The African Report, tupe pia uthibitisho wa wamiliki wa Gesi ambao ni tofauti na Serikali
 
Ndio hivyo unataka upate kingi wakati hujatafiti na hujaweka chochote hapo kwenye mradi.

Ukiacha hiyo share ila kuna ajira,Kodi na faida zingine mtambuka.

Kumbuka til.70 hizo sio pesa ya serikali ni ya investors.
Mawazo finyu sijawahi kuona

Utafiti gani ? Nani hajui kwamba hapo kuna Gas ?
Mikataba mibovu inafanywa kutokana na kukosa uzalendo, uroho na 10% na kuwa shortsighted...

Unaongelea ajira ?, Ajira kwa vizazi vingapi ? hio ni non renewable energy siku ikiisha na ajira zinapotea..., tungekuwa na busara madini ni mengi kwenye faida ya huku tungewekeza itusaidia na kule..., Tunawaza tu kuuza kwa bei ya kutoa zawadi badala ya kuwaza pia hio natural gas angalau kuwa piped iwasaidia wananchi kuondokana na gharama za cooking fuel (now that is thinking long term)

By the way ni lazima kila maliasili ichimbwe na imalizike kwenye hiki kizazi chetu (and what can we show for it) ? Ni kama mlevi kutumia kiinua mgongo chake kununua bling bling
 
Wewe ni mpumbavu,uliamka tuu ukajua kwamba kuna gas? Wewe ndio ulitafiti hii gas? Unadhani ni mkojo huo kwamba utakuta unavuja kama unavyojikojoleaga kitandani?

Eti kwani ni lazima ichimbwe kizazi chenu,kwa hiyo ukiacha na hujaandaa mazingira ya hicho kizazi kingine kitazaliwa kina akili automatically? Una akili timamu? Is technology waiting your kizazi? Saizi tuna maelfu ya Tani za fossil fuels unfortunately 30 years to come Dunia inapiga marufuku matumizi ya makaa,kwa hiyo kizazi kitafaidia makaa sio? Mega fool wewe.

Una hoja za kitoto na za kijinga, mnawaza ujinga mara 10% and such nonsense.Faida tutakazopata kama Taifa hizi hapa 👇

Screenshot_20220128-082359.png
 
Tupe uthibitisho wa kutoaminika kwa jarida la The African Report, tupe pia uthibitisho wa wamiliki wa Gesi ambao ni tofauti na Serikali
Huu Mchakato ulianza tangia 2016 na Stakeholder wa Kujenga hio Plant ni kama ifuatavyo

Stakeholders[edit]​

Talks between the government of Tanzania and the six oil companies involved in the project began in earnest in September 2016. The oil companies involved include:[11]

  • Equinor ASA (formerly Statoil ASA)
  • ExxonMobil
  • BG Group
  • Royal Dutch Shell Plc
  • Ophir Energy Plc
  • Pavilion Energy Private Limited
Also participating in the talks are the following parastatal agencies of the Tanzanian government.[11]

Wewe ni mpumbavu,uliamka tuu ukajua kwamba kuna gas? Wewe ndio ulitafiti hii gas? Unadhani ni mkojo huo kwamba utakuta unavuja kama unavyojikojoleaga kitandani?

Eti kwani ni lazima ichimbwe kizazi chenu,kwa hiyo ukiacha na hujaandaa mazingira ya hicho kizazi kingine kitazaliwa kina akili automatically? Una akili timamu? Is technology waiting your kizazi? Saizi tuna maelfu ya Tani za fossil fuels unfortunately 30 years to come Dunia inapiga marufuku matumizi ya makaa,kwa hiyo kizazi kitafaidia makaa sio? Mega fool wewe.

Una hoja za kitoto na za kijinga, mnawaza ujinga mara 10% and such nonsense.Faida tutakazopata kama Taifa hizi hapa 👇

View attachment 2129410
Wanajitoa ufahamu kutokana na chuki zao tu! Hawana lolote la maana zaidi ya kujawa na chuki tu

Hawajui pia kuwa sasa Umoja wa Ulaya umeamua kutambua Gesi kuwa moja ya renewable energy kwa iyo uhakika wa uchumi wa Gesi upo sana kwa miaka mingi ijayo

Kwa hali inavyoendelea sasa Ulaya wanahamia Afrika Kama sehemu yao ya kutegemea nishati na Chakula na wala sio Urusi tena. Hivyo ni fursa Kubwa sana kwetu kiuchumi
 
Wewe ni mpumbavu,uliamka tuu ukajua kwamba kuna gas? Wewe ndio ulitafiti hii gas? Unadhani ni mkojo huo kwamba utakuta unavuja kama unavyojikojoleaga kitandani?
Akili ya mtu na fikra potofu ni ku-attack personality na sio hoja; Mimi nimekwambia hayo mawazo ni potofu kuliko..., hao stakeholders sita walioingia mkataba leo ndio walifanya research, na hizo research walifanya kwa hisani? Gas huko iligunduliwa lini na nani na wanaosign mkataba leo ni kina nani ?
Eti kwani ni lazima ichimbwe kizazi chenu,kwa hiyo ukiacha na hujaandaa mazingira ya hicho kizazi kingine kitazaliwa kina akili automatically? Una akili timamu? Is technology waiting your kizazi? Saizi tuna maelfu ya Tani za fossil fuels unfortunately 30 years to come Dunia inapiga marufuku matumizi ya makaa,kwa hiyo kizazi kitafaidia makaa sio? Mega fool wewe.
Again rudia nilichoandika ni lazima natural resources zote zimalizwe katika kizazi chetu ?, Kwa matumizi mazuri tungeweza kuchimba baadhi na kutumia hio faida kuwekeza kwenye migodi mingine kwa stake nzuri zaidi.., Mfano Mkataba wa Diamond Botswana ni sawa na wa kwetu ? Je Dunia pia itapiga marufuku matumizi ya Diamond na Gold ?

Una hoja za kitoto na za kijinga, mnawaza ujinga mara 10% and such nonsense.Faida tutakazopata kama Taifa hizi hapa 👇

View attachment 2129410
Unajua maana ya faida ? Tunapata percent ngapi kwa huo uwekezaji ? Alafu usiamishe mjadala hapa umeongelea kwamba wacha tupate stake kidogo sababu hatukufanya research na hatuna uwezo ili tupate faida ya ajira na Kodi....

Kweli Akili ni Nywele....
 
Wanajitoa ufahamu kutokana na chuki zao tu! Hawana lolote la maana zaidi ya kujawa na chuki tu

Hawajui pia kuwa sasa Umoja wa Ulaya umeamua kutambua Gesi kuwa moja ya renewable energy kwa iyo uhakika wa uchumi wa Gesi upo sana kwa miaka mingi ijayo
Aisee !!!!!
Kwa hali inavyoendelea sasa Ulaya wanahamia Afrika Kama sehemu yao ya kutegemea nishati na Chakula na wala sio Urusi tena. Hivyo ni fursa Kubwa sana kwetu kiuchumi
Hivi ni lini Tanzania au Afrika imekuwa na uhaba wa Natural Resources ? Tuna Dhahabu, Diamond, Tanzanite, Tourist Attractions n.k. (kuwa na vitu vyenye thamani haijawahi kuwa tatizo tatizo ni kwenye mikataba ya kinyonyaji na kipuuzi tunayoingia)

Pili hata bila ulaya soko la LNG lipo kubwa tu hata huko China, Japan n.k. Ndio maana USA analionea Potential na hata Canada na yeye anataka kuingia kwenye uwanja....

Mambo ya Russia mwisho wa siku yatakuwa solved its cheaper kutumia Natural Gas ikiwa Piped kuliko hio Natural Gas kuwa liqufied (its costly kufanya hivyo na storage yake ni expensive)
 
Back
Top Bottom