Mradi wa SGR umeendeshwa vibaya na utalitia Taifa hasara kizazi hadi kizazi

Hakuna mradi ulioendeshwa na Serikali ukafanikiwa. Sio kampuni za simu, posta, Tanesco. Reli ya Kati na Tazara. Sijui unataka mfano gani. Juzi mkaguzi mkuu alitangaza hasara ya bilion zaidi ya 90 kila mwaka kwenye Air Tz Sasa unategemea miujiza ipi?!
 
Kwenye nchi yoyote, mitandao ya barabara na reli ni jambo la muhimu kweli kweli. Huwezi kuendesha nchi bila mizigo na watu kusafiri. Na reli ni moja ya njia za kuaminika na rahisi kwa usafirishaji. Tatizo liko kwenye uendeshaji. Ndiyo maana watu wenye akili wanasema tunatakiwa kufumua system yetu yote ya utawala na kuisuka upya. Viongozi wawe wanapimwa kwa wanachofanya na siyo wanavyoropoka.
 
Pili si kila mradi wa serikali upo pale kuleta faida, mingine inakuwa ni vichocheo vya uchumi,
Kwani wewe ukiona serikali inajenga barabara za lami kwa mabilioni ya shillingi unategemea serikali ipate faida ya moja kwa moja?

Mkuu, naona unadogosha tatizo la ufanisi kwa kutumia dhana kuwa vitu hivi ni vichocheo vya shughuli za uchumi. Kama tukienda na dhana hiyo, je kufa kwa reli za kati na TAZARA ni vielelezo kuwa hakuna tena shughuli za uchumi?? Je hiyo imekaaje ukilinganisha na ukuaji wa usafiri wa barabara ambao ni aghali zaidi kukiko reli??

Kama huna taaluma na usafirishaji, nyamaza na usiyaone mambo haya kama ni siasa. Usafiri wa barabara umekuwa kwa kasi ukiziba matatizo ya usafirishaji wa reli kuanzia wizi, ucheleweshaji na ukosefu wa taarifa! Dunia ya sasa inahitaji mnyororo wa ugavi (supply chain) ulio haraka, ufanisi na gharama ndogo. Mambo hayo matatu yameleta reli kuwa za gharama - gharama kubwa ndio zinafanya supply chain moja kuwa aghali kuliko nyingine na hata kuondoa watu katika biashara kabisa.

Ulilotaja kama sababu ya miundombinu kuwepo ndio hasa sababu ya miundombinu hiyo kufa. Kwa kuwa uongozi unaiona kama huduma, kumekuwa hakuna bidii hata kubreak-even, achilia mbali kupata faida kidogo!!

Unachoshangilia ni kuifanya serikali kukosa kiasi cha fedha kuangalia mambo mengine katika jamii na badala yake ku-safe face kwa miradi hii na kama hilo litatokea kwa SGR - itakuwa ni jambo kubwa sana!!

Niliwahi kushauri hapa, hatukuhitaji SGR kwenda Mwanza bali Tunduma. Ingekuja mpaka Dodoma kisha ikapita Iringa, Mbeya hadi Tunduma!! TRL ingeimarishwa kutoka Dodoma kwenda Kigoma na Mwanza. SGR ingelenga Zambia, Malawi, DRC.

Interest declaration: mimi ni supply chain professional!
 

Kwa nadhalia Serikali Inaweza ikafanya kilakitu. Ila unapotengeneza hoja lazma tuje na vividi. Tuje na mifano halisi. Lini na wapi ilifanya biashara kwa ufanisi na kufanikiwa? Ila kwa biashara za kitabuni wako vizuri sana. Kama motivation speaker na hadithi ya faida ya kilimo Cha matikiti. Juzi walijaribu kwenye korosho ikawaacha watu kwenye maumivu makali sana ambayo hawatayasahau.
Kama Serikali ikiamua kufanya biashara hiyo ya usafirishaji inabidi ijiandae tu kukabiliana na figisu na kila changamoto kutoka kwa wenye mabasi na reli. Isitegemee mseleleko. Ipambane iwe Bora kuliko wao na iweze kujisimamia isihujumiwe. Na ndio maana halisi ya ushindani lkn isiwafunge mikono washindani wengine. Na Kama haiwezi isifanye biashara.
 
Pili si kila mradi wa serikali upo pale kuleta faida, mingine inakuwa ni vichocheo vya uchumi,
Kwani wewe ukiona serikali inajenga barabara za lami kwa mabilioni ya shillingi unategemea serikali ipate faida ya moja kwa moja?
Tunazungumzia option za kuufanya mradi uwe na faida. Lkn huu mradi akitaka aujenge na kuuendesha mchina. Angeachiwa tu. Serikali ikawa inakula Kodi tu za Vat na nyingine. Swala sio kujengwa. Swala itaweza kujisimamia. Na Kama unagarimu ma tilion unachochea au fifisha uchumi?
 
Majizi yameshaanza kupapatuka
kama hili sijui hata kama yanaelewa vizuri faida ya mradi wa SGR kwamba utakomboa wengi.....
hamtaki kuona wtz wananyanyuka
 
Una Akili kubwa Sana. Ubaya kwa Akili hii huwezi kupata nafasi kubwa serikalini.
 
TAZARA ilishindwa nini kuwakomboa wengi kwa miaka 50 ya uwepo wake?
Hizi ndio zile hadithi zenu za Muongo za gesi ikipatikana tataizo la umeme litakuwa la kihistoria..propoganda ni rahisi sana.
Majizi yameshaanza kupapatuka
kama hili sijui hata kama yanaelewa vizuri faida ya mradi wa SGR kwamba utakomboa wengi.....
hamtaki kuona wtz wananyanyuka
 
Mradi wa mwendokasi ulianza kipindi cha mwendakuzimu, na bado ulifeli, nikawa najiuliza na hata humu ndani nimeuliza zaidi ya mara moja, nini kinafanya tuamini SGR itakuwa na ufanisi?
hofManya mradi wa mwendo kasi usijiendeshe kwa ufanisi wakati abiria wa kumwaga ndicho kitakafanya SGR isijiendeshe kwa ufanisi!

Uvivu, ufisadi na ujinga wa mwafrika
 
Nauli wanayotoza inalingana na vyombo vya usafiri vya watu binafsi. Inakuwaje wao washindwe wakati watu binafsi wanamudu kwa nauli hiyo hiyo? Au umeishiwa na utetezi?
Yaani mpaka iwe bure kabisa ndo ujue ni huduma kwa jamii?
 
Inaleta faida indirect kwa hayo mabasi yaliyoharibika?
 
Izo Basi zikiwa za kampuni binafsi kipi kitaharibika. Serikali kumiliki mabasi NI ujinga uliopitiliza. Landcruser mkonge mpya halmashauri inazitumia miaka minne tu zinalala. Leo imiliki bus kweli.
 
Mradi wa mwendokasi ulianza kipindi cha mwendakuzimu, na bado ulifeli, nikawa najiuliza na hata humu ndani nimeuliza zaidi ya mara moja, nini kinafanya tuamini SGR itakuwa na ufanisi?
Yani wewe huyo mwendakuzimu wako bado anakuchapa hata baada ya kufa!

Miradi ya selikali inafeli sababu moja tu!
Uvivu, ufisadi na ujinga wa mtu mweusi.

Hapa nlipo nmelipia kwa ajili ya kuwekewa maji, lakini ni wiki ya pili hii sijaletewa maji naambiwa mita zimeisha!

Nayo hii mwendakuzimu wako yupo?

Huyo mtu atakutesa sana maisha yako.
 

Kwani kipi kilikuwa tofauti kipindi cha mwendakuzimu?
 
Kuna watu waliamini hiyo reli inajengwa na fedha za serikali na sio kwa mkopo..

Yule jamaa alijua kuwafanyia hadaa watu sana!
 
Kwa mawazo yako unafikiri kila kitu kiko sawa usipoona huo ushahidi?
 
Mwendakuzimu anakufanya unaweweseka vibaya sana

Shetani aliasi miaka na miaka iliyopita lakini mpaka leo bado tunamsema, itakuwa huyo dhalimu uchwara?
 
mbaya zaidi hizo huduma hazitolewi. leo hii TAZARA inatoa huduma gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…