Mradi wa SGR umeendeshwa vibaya na utalitia Taifa hasara kizazi hadi kizazi

Hakika wewe ni mpumbavu juha Waheed
 
Mkuu
 
Unaropoka sana aisee

Perhaps hata familia na ndugu wa Karibu unashindwa kwenda nao sawa lakini unajipa uwezo president a kuanalyse multi million dollar project

What the heck
 
Well Said,ndio eti think tank kijijini kwao,kama taifa tuna hasara dhidi ya vijana model hii
 
Ule ulioua mashirika kadhaa ya umma baada ya kupelekwa private?
 
Tazara imelegalega sababu ya ufisadi na usimamizi mbofu.
Trc vilevile imekuwa hivyo .
Atc vilevile.
DART/ BRT vile vile.

Suluhisho : sgr miundombinu imilikiwe na serikali 100%, treni na huduma imilikiwe na serikali 20% na 80% sekta binafsi ya kampuni za kimataifa zilizofanikiwa Kwenye huduma ya reli sio kampuni za mifukoni

Atcl : 51% imilikiwe na serikali na 49% kampuni kubwa za kimataifa za ndege zilizofanikiwa sio kampuni za kuletwa na watu kwa manufaa ya ten percent

Tazara , Trc na BRT ziendeshwe kama mfumo wa sgr
 
Shetani aliasi miaka na miaka iliyopita lakini mpaka leo bado tunamsema, itakuwa huyo dhalimu uchwara?
Unaishi kwa shida sana mkuu!
.
Marehemu bado anakuchapa hata baada ya kufa
 
Ni wachache watakuelewa
 
Hujui kusoma financial statements, kojoa ukalele. Kilochopo kwenye hiyo statement ni kama kuchukua pesa mfuko wa shati ukaongezea zilizopo kwenye mfuko wa suruali halafu ukajisifia umeongeza utajiri.
Huko ndio kule kunasemwa unajitekenya na kucheka mwenyewe.
 
Unachanganya Mambo wewe. Ungeweza ungeuliza mawali uelimishwe.
 
JF tafadhali mwalikeni waziri wa miundombinu atueleze ni kwanini Tazara, Mwendokasi na TRC wanafanya biashara kwa hasara.

Anzisheni kipindi hapa ili apewe maswali na ayajibu.

Binafsi nimesikitika sana marehemu JPM kuondoka sababu nilidhani ni yeye angeiweza Tazara na kujificha kwa sababu ya kuwa ni maamuzi lazima yakubaliwe pande mbili za nchi yaani Zambia na Tz.

Kuna kipindi alipelekwa Ndumbaro pale sijui alibadilisha nini haswa.
 
Kipimo kizuri cha Magu ilikuwa ni mabasi ya mwendo kasi maana wakati anaingia madarakani, alikuta ni mradi na akauzindua. Je huo mradi uliendeshwa kwa ufanisi? Kile kivuko cha mv Bagamoyo alikinunua yeye, kilikuwa na ufanisi? Hapo piga jibu mstari wa reli ya SGR, achia mbali propaganda nyingi zilizokuwa kwenye huo mradi wa SGR, kama kipande cha Dar-moro kuwa tayari hadi November 2019.
 
Ametoa alert sasa wewe msomi mtafuta mafakti jiongeze utafute izo data kamili tatizo wasomi wa Nyambari Nyangwinye mmezoea kutafuniwa ninyi mmeze tuu...mtamezaga sumu
 
Mkuu 'Hamatan', hukunielewa nilichoandika, au kwa vile ni lazima kufupisha maelezo, sikutoa ufafanuzi wa kutosha kukuelewesha wewe nilichonuia kukiwasilisha.

"Serikali ya Tanzania haina uwezo wa kuendesha chochote kwa faida" Sawa kabisa, na hili ndilo nililoliwasilisha, labda kama sikulinyoosha kama ulivyolinyoosha wewe.
Lakini tukishasema hivyo, haina maana kwamba "Serikali ya Tanzania ikidhamiria, haiwezi kuwa na uwezo wa kuendesha mashirika yake kwa faida". Sasa tunachotakiwa kufanya ni kueleza ni njia zipi zinazotakiwa kufanywa na serikali ili iweze kufanya hivyo.

Mimi hata siku moja sikubaliani na hiyo dhana potofu kabisa ya kusema serikali haiwezi, huo ni uongo.
 
Mkuu Yoda, sijasema kwamba serikali ijiingize katika kufanya kila aina ya biashara inayoweza kufanywa na yeyote, na siyo maana yangu kusema kwamba sekta binafsi izuiwe kufanya biashara.

Kuna baadhi ya mambo ambayo serikali inahitajika kuyafanya kwa ufanisi kwa manufaa ya jamii nzima. Haya ndiyo tunayoyazungumzia hapa

Ni vyema umeanza andiko lako kwa hayo maneno "Ni nadra" ikiwa na maana kwamba inawezekana hata ikiwa ni mara chache.

Umetoa mfano wa serikali ya Marekani na mashirika binafsi, lakini hujatolea mfano na serikali ya China, au Soviet, enzi zile, au Korea Kaskazini leo hii wanapotengeneza 'hypersonic' missiles.

Hata hizo kodi unazosema serikali ikusanye, itazikusanya vipi iwapo inashindwa kuendesha hata shirika moja la kutoa huduma kwa wananchi kwa ufanisi! Unachojisahaulisha hapa ni kwamba serikali haifanyi kazi inavyotakiwa na wananchi ifanye, halafu unachukulia hali hiyo kuwa ndiyo hali ya kawaida inayotakiwa kuwa nayo serikali! Hili sikubaliani nalo.
 
Huwezi kujua sababu uwezo wa kuchambua mambo ni finyu.Acha mradi umalizie wajukuu zako wataona faida.Miaka 100 ijayo wataona faida yake siyo wewe
 
Huwezi kwenda na PPP reli ni usalama wa nchi acha ujuha
 
Bado huelewi ninachosisitiza hapa.
Sisemi serikali ifanye kila kitu, na wala siandiki popote kwamba sekta binafsi haitakiwi. Usilazimishe hoja zisizokuwepo.
Siyo nadharia kama unavyosema wewe kwa serikali kufanya kazi zake kwa ufanisi, ikiwa ni pamoja na kuendesha mashirika ya umma. Duniani kote kuna mifano halisi ya serikali nyingi kufanya hivyo.
Kwa hiyo hapa una maana serikali iache ujenzi wa miundo mbinu hiyo kwa kuogopa "figisu"?
Inachotakiwa kufanya serikali ni kuhakikisha inasimamia utendaji kazi kwa wajibu wa taratibu za kazi hiyo kwa hao watakao kuwa kwenye utumishi wa kuendesha kazi hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…