Mradi wa umeme wa Stiegler's Gorge Hydroelectric Power Station kuondoka na Waziri January Makamba

Mradi wa umeme wa Stiegler's Gorge Hydroelectric Power Station kuondoka na Waziri January Makamba

Wanataka tuendelee Kuwa watumwa mbona nchi Tajiri ndiyo waharibifu wakubwa na wachafuzi wakubwa wa hali ya hewa ya dunia hawasemwe?
 
Andika pia na faida za bwawa hilo kwa ukuaji wa.uchumi wa nchi yetu,"pathetic"
 
KIBURI KIBAYA SANA.
BORA UWE NA JEURI LAKINI SIO KIBURI.
 
Mradi wa gesi umeishiwa wapi?? Kwa nini wang'ang'ane na vitu vua uharibifu wakati vitu vyenye madhara madogo tena gharama nafuu na very effective vipo??
Mkuu hukusikia Jiwe anakwambia wakubwa wamegawana gesi? Ile gesi Maccm yaliigawa kwa hati ya dharula haraka haraka wala hakuna namna
 
Kuna kitu jiwe hakisemi au anapotosha:
1. Kuna ukataji wa miti karibia ukubwa wa jiji la dar. Dar ina sq Km 1393, sasa hapo ni miti inakatwa ukubwa huo bila uoga. Kama mnakata miti hiyo je sisi wanainchi ndo tutaiacha.

2. Jana kwenye habari ITV maji ya mto wami yamepungua sana mpaka mto sehemu kubwa imebakia ni mchanga vipi mamba, viboko na wanyawa wategemeao maji kuishi. Hamjalifikiria hili

3. Maji yanapopungua kuna magonjwa yanayosababishwa na uhaba wa maji eg anthrax

4. Kama kuna mamlaka ya maji basi inabidi watumie dawa nyingi kutibu maji nayo ni hasara kwasabu itatubidi tulipe zaidi kufidia

5. Kuna swala la mmomonyoko

6. Kuna swala la uharibifu mazingira eg. kuna watu zaidi ya 3000 kuishi kule porini hilo nalo ni janga.

7. Kuna mengi nashauri tuachana na mpango huo
 
Mradi ujengwe tu maana manufaa ya kiuchumi ni makubwa kuliko hizo athari za kimazingira. Tunahitaji umeme wa uhakika kwa nchi nzima. Hao viumbe laki 2 watakaoathirika wamehesabu mpaka nyoka na kenge wasio na faida kwetu.
 
Kuna sehemu nampenda rais wangu kwa moyo wangu wooote kabisa kabisa. Bonde la mto Rufiji lipo kwetu. Mtu asitupangie cha kulitendea bonde letu. Hao walionunuliwa na mabepari kwa vijiallowance vyao wasituyumbishe. Tunataka tuwe na umeme hadi mwingine tuuweke kapuni kwa matumizi yasiyo ya lazima. Umeme wa maji ndio pekee wa gharama ya chini. Msitupangie cha kufanya na bonde letu tulilopewa na Mungu. Natamani kusikia tu kuwa Kazi imeanza
 
Hayo ndiyo madhara ya kutumia madesa,

Nadhani watakua wamekopi na kupesti ripoti za WWF , kuhusiana na huo mradi.
 
Katika hili anastahili kukosolewa, katika dunia ya leo utafiti ni kitu mhimu. Huwezi kipinga ripoti ya utafiti bure bure tu.
Utafiti wa jua na mradi tazara ukisikia mavi ukanye kawe au? Na mtu anaekuambia hvyo ana PhD khaaa
 
Uharibifu wa mazingira haujafanywa zaidi Africa kuliko sehemu zozote duniani,,, hasa mabara yao hawa wazungu,,,, nampongeza magufuli kwa kuwa mzalendo juu ya hili
 
moja ya matatzio ya watanganyika ni UJINGA.
WA KUTOYATAMBUA/KUYAKABILI MAZINGIRA YAO.
mradi Unaweza fanyika lakini je?kuna mpango mkakati wa kuitunza na kuifadhi ecology na mfumo wa pale??? nisingeprnda yale ya kihansi yajitokeze
Cha msingi ni kupambana na hujuma tu,hujuma ni kikwazo kikubwa sana,watu hutanguliza ubinafsi
 
Yule kwnge kule Porin anafaida gan kuliko Umeme wa uhakika? Wakate tu,hata dubai ilikua jangwa lakin sasa hiv ni green nas tutapafanya green.. Wale wazungu wana maslahi yao kule na tutajega tu iwe isiwe
 
Kuna sehemu nampenda rais wangu kwa moyo wangu wooote kabisa kabisa. Bonde la mto Rufiji lipo kwetu. Mtu asitupangie cha kulitendea bonde letu. Hao walionunuliwa na mabepari kwa vijiallowance vyao wasituyumbishe. Tunataka tuwe na umeme hadi mwingine tuuweke kapuni kwa matumizi yasiyo ya lazima. Umeme wa maji ndio pekee wa gharama ya chini. Msitupangie cha kufanya na bonde letu tulilopewa na Mungu. Natamani kusikia tu kuwa Kazi imeanza
ahahaa nimekukubal mangatara
 
Back
Top Bottom