Acha uongoJana nilikuwa safarini kuja Dar na bahati mbaya mwenyeji wangu niliyekusudia kunipokea simu yake haikupatikana
Kwa kuwa mimi siyo mwenyeji saaana,kupitia hapa jf niliomba kupata msaada wa mtu kujitokeza anipokee maana ningefika usiku sana
Hata hivyo nashukuru sana kwa wenyeji kujitokeza kwenye pm yangu ili wanipokee,jumla ya watu 87 walijitokeza kunipokea bahati mbaya hakuna mwanamke aliyejitokeza kunipokea, nashukuru sana hao 87
Niliwapa watu 11 namba yangu ya simu,watu 7 walinipigia ila wanne walinitext
Nilipofika stendi watu watatu walihakikishia kuwa wapo stendi ya Magufuli ila wawili walikuwa na magari,mmoja yeye alikuwa kwa mguu akiniahidi kwenda kwa daladala Mbagala
Niliposhuka niliondoka na jamaa mmoja aliyejitambulisha Kama M sitamtaja majina yake kwa faragha
Kwenye gari yake walikuwa wanaume watano,mpaka nikaogopa ila wakanihakikishia kuna usalama,nikaingia kwenye gari
Nikakaa siti ya mbele na M tukaanza kuondoka,huku nilimuuliza M Kama hawa jamaa wengine ni member JF akasema hapana
Safari ikaenda Kama saa 3,tukaingia kwenye majengo fulani kwa bahati nikawa nimeona sehemu pameandika Nkuruma hosteli,nikamuuliza M mbona huku ni hosteli,akajibu nataka nishushe hawa wenzangu hapa tuendelee na safari...........
Itaendelea
Hodiii Dar, naomba mwenyeji Buguruni jamani
Nipo safarini nakuja Dar kuwapa hi na utalii wa ndani Buguruni moja hiyo mwenyeji ajitokeze basi coz mi si mwenyeji sana katika hili jiji zaidi ya Mwanza
Wanaume wa Dar ni bahili, naondoka bila zawadi
Nilikuwa kwenye ishu zangu hapa Dar, nikakutana na wanaJF 4 pm kwa pamoja wakaniomba tukutane nimewakubalia. Wanaume watatu na mwanamke mmoja, nashukuru kukutana na nyinyi ila nyie ni mabahili hatari, soda Pepsi imagine wanaume watatu. Mje wenyewe kabla sjataja ID zenu. Asante Dada M ubarikiwe...
Msaada: Nahisi nimepotea humu Dar es Salaam
Nipo Mikocheni karibu na kituo cha polisi, nataka nirudi Kimara lakini nahisi nimepotea. Nifanyeje nirudi Kimara ndugu zangu, nilikuwa natokea Makumbusho nikajikuta nashukia Mikocheni. Nifanyeje nirudi Kimara usiku unaingia, si ndo nitapotea zaidi?