Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

Inategemea private zipi ilikuwa aibu shule kama shaaban robert, aga khan mzizima hizi nazo ilikuwa aibu?
 
Umefanya la maana,mimi pia nimewashauri wengi kufanya hivyo.Bora kwajengea watoto nyumba zakuwasaidia.Hata we.we hizo nyumba,zitakusaidia.
Unakaa nyumba ya kupanga,halafu unalipa mamilioni ya ada za shule.Wenye shule wanajenga majumba,wewe unabakia na mavitabu ndani ya nyumba.Kila mwaka wanataka ununue vitabu vipya,ukiwa na watoto wanne,wanasoma private,lazima upate presha tu.
 
Hata mimi kipato kilipokata nikatoka kwenye steki na soseji nikaingia kwenye dagaa wale wanaokaangwa barabarani, nikawasifu sana kwa utamu wake na ubora wake kwa kurumangia dona.
Safi sana hamna kukaa kinyonge🤣😂
 
Fanya kitu kulingana na uwezo wako. Pia calculate risks kabla ya kufanya kitu chochote. Jiulize mpango wako wa fedha ukoje kwa miaka 7 ijayo ya mwanao huko English medium. Ukiona huelewi peleka St Kayumba. Kusema kwamba English Medium wanatoa watoto mayai ni zile stori za sizitaki mbichi hizi...
 
Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete walisoma silabasi ya uingereza na mitihani ilitoka Kembriji, ilisahihishwa Kembriji na matokeo yalitokea Kembriji.
.
Sahihi Wengine humu wanajifariji wanadhani hao maraisi walisoma kayumba walisoma shule za private msingi tena za kulipia kama za private za sasa hivi
 
Hapana, hazikuwa za praiveti bali mfumo wa elimu enzi hizo ulikuwa ni wa uingereza.
Zikikuwa private za dini za katoliki, Anglican ,Agha Khan nk serikali ya kikoloni haikuwa na shule za Serikali ilileta tu syllabus na mitihani ya Cambridge

Mkoloni hakuwa na shule hata moja ya serikali
 
Naunga mkono hoja asilimia mia.
Shida inapokuja unataka kuishi kama tajiri wakati ni masikini. Una fake maisha.
Shule za wenye hela, na wewe unapata vihela vihela unataka upeleke shule ya wenye hela matokeo yake unaishia kwenye madeni na kuwarudisha nyumbani.
Kuna watoto wazazi wao wanasowasomesha Fedha boys, akimaliza anaenda kusoma chuo nje ya nchi.
Tusifake maisha, ishi kwa uhalisia wako. Ukimpeleka za wenye hela lazima siku moja uumbuke.
Usijifariji kwasababu umepata faida, sema hauna hela. Kuna watu watoto wao wako kwenye shule za hela, na maendeleo anafanya na hakopi wala hawawazi ada. Amini hilo
 
Umefanya la maana,mimi pia nimewashauri wengi kufanya hivyo.Bora kwajengea watoto nyumba zakuwasaidia.Hata we.we hizo nyumba,zitakusaidia.
Wazazi wengi wenye mawazo yako walijikuta mbele wanakwama Ohh nawajengea hizi nyumba wanangu hapa kijijini

Watoto wanapata kazi mikoa au wilaya nyingine au mikoa mingine au nje ya nchi na hawana mpango wa kurudi kwenye hivyo vijumba viko chini ya kiwango cha kisasa vilivyoko kijijini au nje ya mji huko visivyo kwenye fashion ya kisasa viwe vighorofa nk

Watoto somesha vizuri the rest watajaza wenyewe mbele ya safari kama nyumba wao ndio wajenge nyumba wapi ndani ya nchi au nje ya mjini au kijijini ya kiwango gani na fashion ipi kwa wakati wao watakao kuwa nao

Huwezi kubeba hadi maamuzi yao ya future .Wewe kazana kusomesha elimu nzuri tena mno .Future waachie wenyewe Usiingilie hadi huko
 
Muache mtoto ajichanganye na watoto wengi ili wampe changamoto. Kuna baadhi ya shule za private darasani kuna wanafunzi wanane mtoto anakuwa bwege halafu anakuwa bored pia.


Dunia ni mbaya na ina watu wabaya. Huo ndio uhalisia wa dunia. Kumuweka private kwa sababu hutaki akutane na uhalisia wa dunia ni kufanya kama mbuni, anajificha macho ili asimuone adui yake halafu anaacha matako wazi.

Akitoka shule atakuja kukutana na huo uhalisia ambao ulikuwa hutaki au experience ilhali wenzake tayari wamesha u experience

Muache mtoto ajifunze kuhusu uhalisia wa maisha yeye mwenyewe. Kuna jamaa mtoto wake kaanza kupanda mwendokasi yupo darasa la kwanza anatoka kimara anaenda gerezani.
 
Kumbe? 🙌 Ni hatari aisee
Unajua sisi masikini huwa tunajifariji sana tusionekane tumeshindwa au hatuna hela. Utasikia yeye anaishi kwenye ghorofa mimi kwenye nyumba ya kawaida ila usingizi ni ule ule.
Hapa duniani kuna watu wanaishi na wengine wanapambana ili waishi.
Kuna watu watoto wao wanasoma kwenye shule za hela, maendeleo anafanya, akimaliza mtoto anaenda kusoma nje ya nchi km Canada. Sisi masikini ukipata hela, una fake maisha ili uonekane na wewe una hela.
Kuna watu wanakaa hoteli ya nyota 5 mwaka mzima akifanya shughuli zake yaani kifupi hela kwake siyo tatizo.
Huyu bwana hakuwa na hela ila alifake maisha aonekane na yeye ana hela matokeo yake akarudi kwenye uhalisia.
Kuna watu wanahela na hela kwao siyo tatizo.
 


Uko sahihi sana watu wanalazimisha shule sio za level zao.

MO DEWJI alosomeshwa IST sababu ndio uwezo wa familia yao utajiri mkubwa ulikuwa upo kwenye familia yao. Hakuwai kusimamishwa asiende shule kisa ada.

Na wala baba yake hakuwai kwenda kukopa hela ya Ada ili amlipie Mo dewji IST.

Mo dewji hakuwai kuzunguka na bahasha kutafuta ajira ama kazi

MO DEWJI WAKATI YUPO A LEVEL ( HIGH SCHOOL ) baba yake alikuwa ananunua shirika la National milling kutoka kwa serikali kwa mabilioni ya pesa.
 
wataje hao watu so that we be sure ur not talking about ghosts
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…