Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

Uko sahih watoto wengi pia was level za English medium wengi wankuwa wanalaini sna na hawajui hesabu wengi ,wengi Ni vilaza wa hesabu mno
Hata walimu wenyewe hakuna anayejua hesabu, kuandika tu ni shida, elimu ni kama unavyo mpira wa miguu ni ngumu nchi masikini kuchukua kombe la dunia na elimu hivyohivyo.
 
Zikikuwa private za dini za katoliki, Anglican ,Agha Khan nk serikali ya kikoloni haikuwa na shule za Serikali ilileta tu syllabus na mitihani ya Cambridge

Mkoloni hakuwa na shule hata moja ya serikali
Tabora School na Middle School(Native Authority) hizi nyingi zilikuwa za boding'i na karibuni majimbo yote(mikoa) zilikuwepo na baada ya uhuru zilikuwa chini ya serikal za mitaa(Local Authority)
 
Nazishukuru shule za kulipia bila hivyo maisha kwangu yange kuwa magumu zaidi na sidhani kama wangevuka kidato cha nne.Nikikuta mtoto hajafaulu ninavyotaka nafoka kweli, hiyo huduma hauwezi kuipata st.kayumba.Na vyote unafanya, nyumba na kusomesha usafiri juu, maisha yanasonga, nyumba na viwaja ni vya nini kama kama mtoto hana elimu niipendayo?
 
Lakini yote maisha,na kama anajifariji bas ni njia nzuri kuliko njia ya kujistress mkuu.Mungu aendelee kumpigania huyu mpambanaji👊
 
Anajisifia baada ya kuwarudisha shule za kayumba amewanunulia kiwanja, sijui atawajengea nyumba na hapati stress za ada. Huyu hakuwa na hela tu alifake maisha.
Kuna watu watoto wao wanasoma shule za hela, nyumbani kila mtoto ana gari lake akimaliza hapo anaenda kusoma nje ya nchi na akirudi.
Anaingia kufanya kazi kwenye kampuni ya mzazi wake au anaingia kwenye kazi ambaye mzazi wake ametengeneza connection
Kuna watoto masomo wanapangiwa kusoma, akimaliza ni simu moja tu anaingia kufanya kazi. Hao ndiyo utawakuta BOT sehemu nyeti nyeti za nchi wapo.
 
Ngoja nipige kambi hapa nipate data za kuweza kuwafanyia Evaluation Watanganyika.
Maana kuna vitu navisoma hapa naishia kusikitika.
Wote mna comment vyema
 
Tafuta hela wapeleke watoto shule nzuri
Wengine pesa wanazo kuna sehemu nilikaa nikashangaa mzazi ana hela anasomesha mtoto kayumba kisa anasema anataka mwisho wa siku mtoto akimaliza form six aje apate mkopo bodi ya elimu ya juu bila shida

Mtoto akamsomesha shule ya msingi ya kayumba Darasa zima wakafaulu kwenda shule ya kata ya Kayumba Form one

Form four shule haikuwa na division one wala two wote waliishia division three ,four na zero na hakuna ambaye combination ya kwenda Form five ilikubali

Ndoto za mwanae za ohh akasome high.school ya serikali form five iliishia mwisho cha ohh apate mkopo bodi ya mikopo zikayeyuka hewani.Sababu hata hiyo form five hakuiona

Mzazi kama kipo usiwe na vi theory vya kiajabu ajabu utaumiza mtoto.Somesha shule nzuri
 
Maneno kama ya mwanamke shangingi. Huu Uzi ni wanaume wanao tafuta hela na ambao wana jua ugumu wa hela. Wewe unakaa kwa shemeji huwezi elewa chochote
Usiandike km umekatwa kichwa. Kuna tofauti kubwa sana kati ya mtu anayetafuta hela na mwenye hela.
Huyo alikuwa ana fake maisha. Mtoto wa Samia, Majaliwa, MO, Bakheresa, Jafo, Mwigulu nchemba na Diamond unaweza kuwakuta kwenye shule za kayumba?
 
Kwa mnaosomesha watoto private schools, muwe mnawawekea watoto wenu akiba benki kila mwezi kutoka kipato chako.
Pesa hiyo itamsaidia sana mtoto wako kulipa karo na kukuondolea msongo wa mawazo hata kama umeyumba kiuchumi.
 
Tabora School na Middle School(Native Authority) hizi nyingi zilikuwa za boding'i na karibuni majimbo yote(mikoa) zilikuwepo na baada ya uhuru zilikuwa chini ya serikal za mitaa(Local Authority)
Level ya shule za msingi sidhani kulikuwa na shule hata moja ya serikali kipindi cha mkoloni .Zote zilikuwa za private English medium Schools
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…