Nazidi kuuliza maswali ili kuweza kujua zaidi ya hiki ulichoandika. Umesema wazanzibar pekee yao ndio wapewe 'referendum' na ukaeleza sababu zake. Ukakasi wangu ni nani awape hiyo "referendum" Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar au Serikali ya Muungano? Hapa nakazia nataka unipe jibu ya hili.
Kuna njia mbili zinazoweza kutumika.
Moja, kupitia Baraza la Wawakilishi wanaweza kuja na azimio la kura ya maoni (referendum).
Kuna Wabunge 5 kutoka BLW wanaoingia Bunge la JMT.
Pili, katika masuala yanayohitaji 2/3 katika Bunge la JMT ni suala la Muungano. Wazanzibar wanaweza kutumia 2/3 kudai referendum au ku-block kila agenda ndani ya Bunge wakidai mswada upelekwe wa referendum.
Kumbuka kwamba idadi ya Wazanzibar ndani ya Bunge la JMT inaweza kuathiri maamuzi hata yasiyo ya Muungano. Kwa hili la Muungano wanayo nafasi kubwa sana, hawajaweza kuitumia.
Lakini pia kuna njia yingine ya mkato, ni wao kukataa kuhudhuria mikutano ya Bunge, hilo tu linazuai shughuli zote za Bunge la JMT kwasababu Zanzibar haipo hata kama yanayojadiliwa ni ya Tanganyika! wierd eh!
Wakati nasubiria jibu ya jambo nililouliza nataka kuendelea na maswali yangu ya kidadisi, Kwanini unawabagua watu waliotoka Tanganyika, je hawana cha kuongea kuhusu muungano? Je, wanauhitaji muungano au la? Kwanini na wenyewe wasipewe referendum?
1. Wenye malalamiko ya kuonewa ni Wazanzibar. 2 Kanuni za kawaida ni haki kupewa mlalamikaji kama nilivyokupa mifano. Ethiopia haikupiga kura, Eritrea ilipiga, ndivyo ilivyokuwa kwa Scotland , Timor, Quebec Canada n.k.
Kumbuka kwamba Watanganyika wanapoteza zaidi kwa kuhudumia Muungano na SMZ kwa pamoja.
Kwa mujibu wa maelezo yako umesema watu kutoka Tanganyika wamekuwa wakiwabeba wazanzibar na wazanzibar wamegundua kuwa wanabebwa na watanganyika; je, huoni kuwa wale wanaotakiwa kufanyiwa referendum ni watanganyika
Elewa Tanganyika ndio Tanzania kwasasa. Hakuna ''admin. structure'' inayoweza kusimama as 'an entity'.
Ni kwa msingi huo rasilimali za Tanganyika zinatumika kama za Muungano hata kule ambapo si pa muungano.
Ndani ya Bunge la JMT hakuna Wabunge wa Tanganyika, lakini kuna Wabunge wa Zanzibar! umeelewa?
Hakuna Mbunge wa JMT wa Bara anayeweza kufikisha mswada kwa niaba ya Tanganyika kwasababu haipo.
Bunge la Tanganyika ni la Muungano, Rais wa Tanzania basically ni wa Tanganyika, ataitisha vipi referendum ya Tanzania akadai ni ya Tanganyika!
Ni kwasababu hizo Tanganyika inakuwa abused kwa jina la Tanzania. Mfano, Zanzibar wanachukua kodi za TRA fedha za huduma za uhamiaji zinabaki huko.
Gharama za Wafanyakazi wa TRA na Uhamiaji zinalipwa na JMT kwasababu ni suala la Muungano ambazo ni kodi za Watanganyika kwa jina la Tanzania.
Maridhiano yanafanyika kama kuna pande mbili au zaidi zinatofautina kwenye mitazamo, imani nk. Siyo ungomvi pekee yake ndugu yangu.
Hakuna kutofuatiana mitazamo na Zanzibar. Kinachotakiwa ni kusimamisha 'abuse' ya kutumia kodi za Watanganyika vibaya, na kuhakikisha Zanzibar inakuwa mshiriki na inawajibika katika Muungano si kulalama bila ushiriki.
Tayari Zanzibar na Bara kuna mitazamo ambayo inakinzana. Lazima kukaa pamoja na kuweka misingi ambayo iteleta kuelewana. Hayo ndiyo maridhiano. Sasa kama imedhihirika hawana mchango wowote katia muungano sasa tufanye nini? Unapendekeza jambo gani lifanyike?
Tunakaa pamoja na Zanzibar kujadili nini? Ikiwa wanataka Muungano lazima washiriki na si tegemezi.
Pili, Katiba mpya itakayoweka Tanganyika na uongozi wake ili isimamie rasilimali zake bila kuwa 'abused'
Mwananchi wa Temeke na Manzese analipa bili ya umeme na kodi zaidi Wazanzibar watumie umeme bure
Bilioni 60 ni kiasi kikubwa sana kwa shirika kama Tanesco. Hii ni 'abuse ' ya hali ya juu sana.
Ni abuse kwasababu marais waliopita hawakukubali ujinga huo! Waliona si haki ni abuse kwa Tanganyika.
Naendelea kusema mchakato wa katiba iliyopendekezwa na ile nyingine inayoitwa ya Warioba iliundwa kwa mujibu wa sheria. Na sheria hiyo haiwezi kufanya kazi tena kwa sasa. Wewe binafsi unataka rasimu ya katiba ya Warioba ndiyo iwe katiba ya Tanzania, je, huoni kuwa tayari sheria yake kwa sasa haifanyi kazi? Na huoni kuwa hiyo rasimu ilitakiwa kuingizwa kwenye bunge maalum la katiba ili ifanyiwe marekebisho?
Sheria zinatungwa na Bunge , zinafutwa na Bunge kila siku. Sheria inaweza kurudishwa na kuhuishwa
Hivi Kikosi kazi kimeanzishwa kwa sheria gani ya Bunge!
Je tuunde tena bunge maalum la katiba ili tuijadili rasimu ya warioba? Nataka unieleze kwa kina katika utatanishi huu wa kisheria unataka Serikali ya SSH ifanye nini kwa sasa?
Rasimu ya Warioba imebeba maoni ya Wananchi na ndipo pa kuanzia. Tunakwendaje mbele ndio mjadala.
Haya ya Mkandara si yametumia pesa, ni kwa sheria gani iliyoanzisha na kwa ridhaa ya chombo gani.
Nashindwa kukuelewa sasa maana wewe umesema EA federal state inaweza kupatika kwa miaka 25. Nikakujibu kwahiyo tuunde katiba ya miaka 25 tu? Umekuja kuibua issue ya EU huku ukikwepa mada husikia. Unataka sasa tuanze kuongelea issue ya EU na kuacha kuongelea suala la msingi la kuhusu katiba yetu ya Tanzania.
MIMI MWENYEWE NATAKA TUWE NA KATIBA. Lakini niambie tuwe na katiba hiyo kwa utaratibu upi?
25 nilisema kama 'nominal' tu kuonyesha ilivyo impossibe, ukweli ni kwamba hatuwezi kuwa na federation
Nkrumah, Nyerere, Biumediane, Gamal Abdel Nasar, Sekoutoure, Obote, walishindwa ! hawa wa leo hawawezi.
Ona sasa 4R siyo kitu unatakiwa ukibebe, 4R ni falsafa inatakiwa ikae kwenye ubongo na itekelezwe. 4R siyo maridhiano pekee bali kuna Reforms, Resilience na Rebuild.
Falsafa! tafadhali tuache hili la 4R. Ni kupoteza muda hakuna falsafa yoyote!
Sasa unaposema unahitaji Katiba na Sheria za nchi hayo ni sehemu ya 4R kwenye kipengere cha reforms. Ndiyo maana kwa sasa kuna miswada ya sheria inayohusu Uchaguzi, Tume ya Uchaguzi, Sheria ya Vyama vya Siasa nk.
Hatuhitaji 4R kwa sheria za nchi, hayo ni maono ya mtu anaweza kuwa nayo.
Kama Taifa hatuoni umuhimu zaidi ya kupotezeana muda tu. Hivi hawa si walikuwa katika serikali zilizopita! kipi kipya walifanya zaidi ya umasikini miaka 60 leo wanakipi cha kusema.
Falsafa tuongelee akina Nyerere!
Ndiyo maana kwenye mada hii tunajadili mrejesho wa mkutano uliofanyika kuhusu sheria hizo. Sasa wewe unataka watu wote waamini unachokiamini wewe, comrade wangu imani yako baki nayo lakini unachotakiwa uwe na ustahimilivu maana na wenzako wapo na imani zao.
Hakuna mabadiliko ya sheria bila kufumua Katiba. Tume ya uchaguzi ipo kisheria utawezaje kubadili tume bila kugusa katiba. Sitaki mtu aamini ninachoamini , kila mtu ana mawazo yake na yaheshimiwe kama yangu pia.
Tunachosema wengine ni kwamba mikutano inayofanyika sasa hivi ni kupoteza muda, fedha na ulaghai tu hakuna chochote cha maana. Kama ndio 4R basi ni dead on arrival. Tunahitaji kuikwamua nchi !