Venus Star
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 26,519
- 78,311
- Thread starter
- #81
Nashukuru sana kwa maelezo yako mazuri na marefu. Umekuwa na msisitizo kuhusu kuwa na katiba mpya. Na umeibua mada ya kuhusu wazanzibar waulizwe. Sasa ninakuuliza nani awaulize hao wazanzibar? Je, huku bara hawatakiwi kuulizwa kuhusu muungano?Kwanza, wazo wa EAC kuwa Federal state halipo na halitawezekana kwa miaka 25 ijayo.
Tulishindwa wakati wa EAC iliyokufa 1977 kwasasa haiwezekani hasa tukizingatia nchi zilivyoongezeka
Hadi sasa kuna suala la Tariff lisilo na jibu, kuna suala la Monetaty union lipo pending kuna ugomvi wa Taasisi gani iwe nchi gani. Wanachama hawalipi ada, mfano, South Sudan imelipa baada ya miaka 7.
Katika mazingira hayo, federation is a myth.
Suala la Zanzibar haliamuliwi na EAC, lina amuliwa na Wazanzibar wenyewe. Ni kwa msingi tunashauri sana kwamba kabla ya kuandika katiba ni vema Wazanzibar wakaulizwa kwa referendum ikiwa wanahitaji Muungano.
Ikiwa hawataki muungano hakuna tatizo, kama wanautaka Muungano ni wakati wawe washiriki na si mzigo
Kuhusu R4, nimekueleza hazina maana yoyote kwa maisha ya Mtanzania.
Reconciliation( maridhiano) : Na nani, kwa kitu gani.
Resiliency (ustahimilivu) : Nani anahitaji hili kwasababu Watanzania wanaishi kwa utangamano bila tatizo
Reform ; Haya yapelekwe CCM kwasababu wametawala miaka 60 na umasiki upo pale pale
Rebulilding; Nani alibomoa ? Hakuna Chama chochote kilichowahi kutawala, akaongea na CCM
Tunahitaji Katiba, hizo 4R hazina manufaa kwa Taifa.
Ni slaogani tu kama ile ya maisha bora kwa kila Mtanzania leo tunajua ni maisha bora kwa Familia yake,
Kuwauliza wazanzibar na wa bara hayo ndiyo maridhiano kiongozi wangu.
Je, tuendelee na ile ya Warioba au tuifanyie marekebisho.
Nimeongelea kuhusu EAC maana ndiyo direction yetu kuwa na federal state. Sasa unaposema miaka 25, mbona ni michache sana? Kwahiyo tuunde katiba itakayodumu miaka 25 tu? Katiba isiyoangalia mwelekea wa EA federation?
Mimi nadhani bado 4R zinahitajika. Lazima tukae kama nchi tujadiliane na kuridhiana. Tukienda kwa mihemko tutajikuta tunaunda katiba mbayo haitadumu.
Yangu ni hayo.