Kwanza umesema zamani wazanzibar walikuwa hawataki muungano maana walikuwa wanasema kuwa wanaonewa. Ukasema kwa sasa wamegundua kuwa muungano upo na manufaa kwao. Sasa hao hao ambao wanapata manufaa eti ndio walalamike. Niambie sababu ya wazanzibar kutaka referendum ni zipi?
Umeshasiki kitu kinaitwa ''mamlaka kamili''. Huwezi kuwa na mamlaka kamili katika Muungano.
Hakuna anaye define mamlaka kamili ni kitu gani. Ili kuondoa malalamiko hayo, Wadai referendum.
Which is Which? Kwahiyo Watanganyika hawana malalamiko? Hapa tunapojadili wewe ni mtanganyika na moja ya malalamiko yako ni haya ya Tanganyika kuihudumia Zanzibar.
Watanganyika hawana malalamiko! Wanachotaka ni kudhibiti 'abuse' inayotumiwa sasa hivi. Mifano
Kwanini Zanzibar wapewe 9% ya Bajeti ya Tanganyika ikiwa kuna mgao wao wa BoT n.k.
Kwanini Wazanzibar watumie huduma, gharama alipishwe Mtanganyika.
Kwanini Zanzibar wakusanye kodi, mishahara ya wakusanya kodi wa Zanzibar alipe Mtanganyika
Kwanini Mzanzibar aamue hatma ya mambo yasiyo ya muungano ndani ya Bunge
Kwanini Kodi za Watanganyika ziende mfuko wa jimbo Zanzibar! Watu 2.500 sawa na Ubungo watu milioni 1.
Kwanini Zanzibar itumie jina Tanzania kama uchochoro wa kodi kwa gharama za Watanganyika
Kwnini Zanzibar apewe mkopo na deni lilipwe kwa jina la Tanzania kupitia kodi za Watanganyika
Orodha ni ndefu sana,
Yote yanafanyika kwa 'abuse' ya jina Tanzania. Siyo malalamiko ni 'abuse' ya Rasilimali za Tanganyika
Sijaju kwanini unakimbia kuongelea maridhiano. Lazima tuwe na common understanding. Kama tunataka kuendelea na muungano lazima wote pande zote mbili wahusishwe. Na kama wazo lako la kufanya referendum basi pande zote wafanye. Lakini sasa siyo tu kuongea kufanya referendum nani ambaye anayakiwa ku initiate?
Simple, Tanganyika haihitaji Zanzibar! Wanaohitaji wafanye referendum waamue wanahitaji Muungano au la. Kama wanahitaji wakubali hakuna mamlaka kamili na wawajibike katika Muungano si kushiriki
Unaposema Rais wa Tanganyika ndiye wa muungano maana yake hatakiwi rais kutoka Zanzibar akawa Rais wa Tanzania? Bado sijakuelewa mantiki yako hapa.
Ni kweli kwasababu inahitaji kufikiri ili upate mantiki. Nitakusaidia
Hakuna Wizara, Taasisi, shirika au mamlaka ya ''Tanzania'' isiyokuwa na mbadala Zanzibar. Kama ipo nitajie moja tu
Kwa mantiki hiyo, kila kinachoitwa cha Muungano ni cha Tanganyika kwasababu Zanzibar kuna mbadala wake.
Kumbuka Zanzibar wanapohitaji ku 'abuse' wanatumia taasisi za Tanganyika kwa jina la Tanzania .
Mfano;
Mgonjwa toka Zanzibar anakujaTanganyika na kudai apelekwa India kwasababu yeye ni Mtanzania.
Wizara ya afya si ya Muungano. Mtanganyika hawezi kuhudumiwa na SMZ katika afya. Abuse ya jina.
SMZ inakataza Mtanganyika kumiliki ardhi. Mzanzibar anamiliki ardhi Bara kwa jina la Tanzania . Abuse
Rais Mwinyi alikuwa Mbunge wa Mkuranga kwa jina la Tanzania. Ni haramu Mtanganyika kufikiria hilo Zanzibar
orodha ni ndefu
Unasema Tanganyika imekuwa abused kwa jina la Tanzania. Je, hatuhitaji reforms?, Je hatuhitaji maridhiano? je, Hatuhitaji Rebuilding?Tunaridhiana na Zanzibar kwa lipi? Kwanini huelewi ! Hatuhitaji reform au rebuilding, tunahitaji kusimamisha 'abuse'
Kuna ''abuse'' kubwa sana, hivi kodi zinajenga Ofisi ya Mkamu wa Rais na Waziri mkuu Zanzibar kwa faida gani.
Ni kuweka majengo na kutengeneza ajira Zanzibar kwa jina la Tanzania na kuhudumiwa na kodi za Tanganyika. VP na PM hawana kazi Zanzibar. ''abuse' ya kodi za Tanganyika. Nyerere hadi Magufuli hayakuwepo haya.
Je, unazijua hadidu za rejea za kikosi kazi?
Nimezisoma , ni non sense. Kwamba Tatizo la Tanzania ni uwiano wa jinsia!
Nikajibu hata mimi Ninataka hiyo Katiba mpya. Lakini utueleze ni
KWA UTARATIBU UPI?
Rasimu ya Warioba irudishwe. Mswada upelekwe, sheria zinatungwa na kufutwa na Bunge.
Kwani sheria gani ilianzisha kikosi kazi?
Hatuwezi tukaacha, ni lazima tujadili na kutoa maoni yetu maana ndio mwongozo wa kiongozi wa nchi.
Endelea kujadili 4R
Hatuwezi kukaa kimya tu eti tu member mmoja wa JF amekataa. Utaacha wewe kujadili lakini walio wengi watatoa maoni yao.
Wananchi wamegoma! sijui una umri gani! ukirejea 'slogan' za waliopita hili Wananchi wamegoma.Maoni yangu
Ni Nyerere pekee anayetakiwa kuwa na falsafa? Hapa sijakuelewa kabisa mantiki yako.
Hutanielewa, tuachie hapa maana tutavuka mipaka. Viatu vya Nyerere wapo wasioweza kuvibeba.
Watu wanakuwa na falsafa kwenye familia zao, watu wanakuwa na falsafa kwenye makampuni yao, watu wanakuwa na falsafa kwenye imani zao. Iweje nchi kama ya tanzania isiwe na falsafa? Watu wenye muono hafifu hawataona chochote kwenye falsafa hii ya 4R. Lakini kwa watu intellectual wanaona mwelekeo wake.
Falsafa ya nchi ni maono ya Wananchi siyo maoni ya Mwananchi.
Unapokuja na kuongea tu bila kuleta mapendekezo watanzania wakueleweje sasa? Rais amekuja na falsafa ya 4R wewe huitaki; sasa unataka falsafa gani?
Katiba haiandikwi kwa 4R au kikosi kazi. Katiba ni nyaraka shirikishi iliyobeba maoni na maono ya Wananchi kama alivyofanya Jaji Mzee Warioba, Mzee Butiku na Mzee Salimu.
Hawa Wazee ni hazina, wanaijua Tanzania walikwenda kuwasikiliza Wananchi. Kikosi kazi kimefanya ''survey' .
Njoo na solution ya "TUNATAKA KATIBA, KWA NAMNA GANI TUIPATE?"
Turudi kwenye Rasimu ya Warioba iliyobeba maoni yetu. Upelekwe mswada wa mchakato.
Lichaguliwe Bunge la Katiba lisilo na Wanasiasa bali wawe sehemu ya Bunge. Tuendelee kuanzia hapo.
Kikosi kazi ni kupoteza muda na rasilimali, zaidi ya kutaka usawa wajinsia katika vyama Kikosi kazi hakikuwa na chochote kipya zaidi ya Rasimu ya Warioba.
Kikosi kazi kimetuletea hoja ya kwamba '' Vyama vya siasa viwe na uwakilishi wa 50/50' katika uongozi.
Pamoja na umasikini uliotopea hili ndilo tatizo kuubwa saaaana la Watanzania. Kikosi kazi! Mungu ibariki Tanzania