Kuna clip Moja inazunguka kwenye mitandao ya kijamii, ikimuonyesha Mbunge wa Arusha mjini, Kwa tiketi ya CCM, Mrisho Gambo, alimkashifu Sana Mbunge wa zamani wa jimbo hilo, Godbless Lema, kuwa alikuwa mtu tapeli, ambaye hata alipokwenda salon ya kunyoa, alikuwa akiwakopa na kiondoka bila kulipa chochote!
Akaendelea Mbunge huyo kueleza kuwa Mbunge huyo wa zamani wa Arusha mjini, alikuwa pia akila chakula Kwa mama ntilie, bila kulipa!
Akazidi kuelezea Mbunge huyo Gambo kuwa hata sababu zinazotolewa na Mbunge huyo wa zamani kukimbia nchi, Kwa madai ya usalama wake, ni ya uzushi na ukweli aliodai yeye ni kuwa Mbunge huyo aliikimbia nchi, kukimbia madeni anayodaiwa sehemiu mbalimbali nchini.
Tunafahamu kuwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan, wakati anaonfoa zuio hilo batili la kutofanya mikutano ya hadhara Kwa vyama vya kisiasa, alitoa tahadhari Kwa viongozi wa vyama hivyo, kufanya siasa za kistarabu na Wala siyo za matusi Wala kuchafuana.
Ninachouliza, je tahadhari hiyo aliitoa Kwa viongozi wa vyama vya upinzani pekee na kuwaacha viongozi wake wa CCM waweze kujiropokea watakavyo, kama alivyofanya Mbunge Mrisho Gambo?
Je ikitomea Lema naye ayakaporejea nchini, aamue kujibu mapigo, si ndiyo hapo patakapochimbika?
Ingekuwa vyema chama chake Cha CCM, kikumuita Mbunge huyo Mrisho Gambo, kwa kuwa ustarabu wetu wa nchi yetu, hayo maneno hayakustahili kutamkwa na mtu mwenye heshima kama yake ya ubunge, badala yake maneno hayo yalipaswa kutamkwa na vijana wa vijiweni.