Option ya kwanza.
Baada ya utenguzi huu naona Siasa za Arusha zikibadilika. Mrisho Gambo naona akienda KUGOMBEA Jimbo la Arusha Mjini. Kama ikiwa hivyo Lema atakutana na Wakati mgumu Sana kwa fitna na weledi wa Gambo Jukwaani. Itategemea pia kama Chama kitampitisha.
Option ya Pili.
Kuna harufu ya Jimbo la Arusha kugawanywa Mara mbili na kuzaa Jimbo la Muriet. Kama likigawanywa kwa Jimbo hili Gambo atakwenda kugombea Muriet. Hii itampa unafuu Sana Mh Lema Kama Atabaki na kugombea Arusha. Itategemea pia Kama Chama bado kinamuhitaji.
Hasara anayoweza kuipata kwenye Option hizi.
1. Makundi ambayo alikuwa anagombana mayo kila siku kwenye Chama je watamuunga mkono?
2. Kuondolewa kwenye nafasi sio sifa nzuri, yaani "Demotion" sio sifa ya kiongozi anayehitaji kusogea juu zaidi. Ana kazi ya kuwaaminisha waliomteua na wananchi kuwa anaweza zaidi.
All in all Vijana tuna mengi ya kujifunza kwenye Hili tunapokabidhiwa majukumu ya kiuongozi. Bado ana nafasi kubwa tu kwenye siasa, Kila la Kheri.
View attachment 1484003