Likely huyo alikuwa ameolewa kwa hizi ndoa bubu za wanachuo - akifua, kupika na kupelekewa moto kila siku. Amepigwa chini ghafla vu bin vu sasa cha moto anakiona.
Inavyoonekana bado yupo kwenye denial stage; na hajakubaliana na hali halisi kuwa keshaachwa. Akija kuondoka kwenye denial stage basi ndiyo safari halisi ya uponaji itaanza. Kwa sasa anahitaji watu wa kuwa karibu naye na kumtia moyo. Kama chuo kina washauri nasaha au wanasaikolojia ya mandeleo basi aende akaongee nao. Naamini atakuwa OK na akijipa muda atakuja kukiona kipindi hiki kuwa ni cha muhimu sana kwake maana kitakuwa ndicho hasa kimemfundisha mambo mengi ya muhimu kuhusu mahusiano na maisha kwa ujumla. Na pengine hatarudia tena kosa la kuolewa na hivi vivulana vyenzie vya chuoni 🚮
View attachment 3219437