Msaada kwa wenye utaalamu na masuala ya dini je ni kweli Quran imeshushwa kutoka mbinguni?

Msaada kwa wenye utaalamu na masuala ya dini je ni kweli Quran imeshushwa kutoka mbinguni?

Sasa kama umetoa ushahidi juu ya Mwenyezi mungu kuweza kuyaandika mawe na kumkabidhi nabii Mussa, unashangaa nini juu ya Quran tukufu kushushwa?
Kwahiyo Quran imeshushwa? Kumbe mbinguni kuna printer kabisa?
 
hapo ulipo but your not aware of it
kwa mujibu wa maandiko wansema juu utaona hata YEsu alikuwa anainua mikoni yake juu nakuelekea mbinguni
Maneno aliyasema yesu na kuinua macho yake kuelekea mbinguni BABA saa imekwish fika <yohana 17> kwa mujibu wa dini mbinguni ni juu sasa ww unasema hapo nilipo 😇😇😇
 
Heri ya Pasaka?

Heri ya Mfungo kwa WAISLAMU.

Ndugu zangu wataalamu wa Masuala ya Biblia na Quran NAOMBENI MSAADA wa hili swali linalonisumbia Daima?

JE ni KWELI QURAN ilishushwa kutoka MBINGUNI?

1. Inamaana Mungu alitengeneza karatasi.

2. Akatafuta Penny Compyuta printer nk?

3. Mbona ni tofauti sana na KIPINDI Cha Musa Mungu aliandika zile Amri Kumi kwenye mabamba mawili ya mawe na kumpa Musa kwenye Mlima Sinai. (Kutoka 24:12-18) Zile Amri Kumi zimeorodheshwa kwenye Kutoka 20:1-17 na Kumbukumbu la Torati 5:6-21.

4 JE tuna ushahidi Gani kama Quran ilishushwa na Mungu?

Natamani Mjadala Huu tujikite kwenye kujibu hoja sio Dini .

Natanguliza shukrani nyingi.
Hapa napo pana kau kakasi ngoja tuwaskilize miamba
 
Mungu anatafutwa kwa shida na mashaka sana,
Yaani watu wana-force hata kusadiki!
Kwa sifa za Mungu mwenyewe, yafaa Mungu mwenyewe awasaidie watu, kwa kuwa nia yao ni njema, wanataka kumjua kama walivyofanya Waisrael walipomwambia Mussa wanataka kumwona Mungu wenyewe, wakidai wamechoka habari za kuletewa, wanataka wamwone ili wamtukuze! Cha abau kuna watu wengi wamepoteza maisha yao au wakati wanalazimishwa kusadiki au wakati wa kulazimisha wengine wasadiki.

Sent from my TA-1004 using JamiiForums mobile app
Dini ni dhana na mawazo ya kufikirika zaidi.
 
Heri ya Pasaka?

Heri ya Mfungo kwa WAISLAMU.

Ndugu zangu wataalamu wa Masuala ya Biblia na Quran NAOMBENI MSAADA wa hili swali linalonisumbia Daima?

JE ni KWELI QURAN ilishushwa kutoka MBINGUNI?

1. Inamaana Mungu alitengeneza karatasi.

2. Akatafuta Penny Compyuta printer nk?

3. Mbona ni tofauti sana na KIPINDI Cha Musa Mungu aliandika zile Amri Kumi kwenye mabamba mawili ya mawe na kumpa Musa kwenye Mlima Sinai. (Kutoka 24:12-18) Zile Amri Kumi zimeorodheshwa kwenye Kutoka 20:1-17 na Kumbukumbu la Torati 5:6-21.

4 JE tuna ushahidi Gani kama Quran ilishushwa na Mungu?

Natamani Mjadala Huu tujikite kwenye kujibu hoja sio Dini .

Natanguliza shukrani nyingi.
Ndugu Quran haikushushwa Kwa karatasi au kwenye mawe quran imeshuhswa Kwa njia ya Revelation{wahyi) ambapo malaika jibril au Gabriel alikua akiifikisha moja Kwa moja Kwa mtume Muhammad Kwa njia hio kutokana na matukio mbali mbali na Muhammad aliyasoma maneno hayo Kwa wafuasi wake
Na wengi wao wakahifadhi kichwani hayo maneno ya Qur'an
Qur'an kunakiliwa kwenye karatasi Kwa kutumia kalamu imenakiliwa na masahaba za mtume na wala haikushushwa ikiwa imeandikwa tayar

Natumai utakua umenifaham ndugu yangu
 
Yani mbinguni Joka kawasumbuwa tukatupiwa duniani.

Ukitaka kujuwa dini ni Utapeli ndio kwenye maandiko kama haya.

Lusifer Alikuwa MBINGUNI MALAIKA Alikuwa KIONGOZI wa Kuomba na kusifu.
MUNGU alimpendelea sana.

Alipoasi yeye na theluthi ya MALAIKA akatupwa Duniani.
Baada ya kutupwa Duniani, Lusifer akaitwa Shetani, au Joka.
MALAIKA walioasi wakaitwa Majini, MAPEPO, MASHETANI nk....

Hii ni kwa mujibu wa Bible
 
Kwahiyo Mungu akaona duniani ndio panawafaa viumbe aliowashindwa hata yeye?

Logic inakataa, hapa mtunga mashairi alipuyanga.

Ukisoma mashairi ya Shabaan Robert kumbe wa juzi tu, basi hawana magenius wa zamani walikuwa washairi wazuri ila kuna sehemu logic inakataa.
 
Allah anasema kitu cha kwanza aliumba kalamu , akaiamrisha iandike , ndio ikaandika mpaka Koran

.....‘I heard Muhammad saying: “Verily the first of what Allah created was the Pen. He said to it: “Write.” So it wrote what will be forever.’”Jami` at-Tirmidhi 3319
 
Na wengi wao wakahifadhi kichwani hayo maneno ya Qur'an
Qur'an kunakiliwa kwenye karatasi Kwa kutumia kalamu imenakiliwa na masahaba za mtume na wala haikushushwa ikiwa imeandikwa tayar

Natumai utakua umenifaham ndugu yangu
Izi zilizoandikwa zilikuwa zipi ?

Aishah said:
“The Verse of stoning and of breastfeeding an adult ten times was revealed1, and the paper was with me under my pillow. When the Messenger of Allah died, we were preoccupied with his death, and a tame sheep came in and ate it.” Sunan Ibn Majah 1944
 
Heri ya Pasaka?

Heri ya Mfungo kwa WAISLAMU.

Ndugu zangu wataalamu wa Masuala ya Biblia na Quran NAOMBENI MSAADA wa hili swali linalonisumbia Daima?

JE ni KWELI QURAN ilishushwa kutoka MBINGUNI?

1. Inamaana Mungu alitengeneza karatasi.

2. Akatafuta Penny Compyuta printer nk?

3. Mbona ni tofauti sana na KIPINDI Cha Musa Mungu aliandika zile Amri Kumi kwenye mabamba mawili ya mawe na kumpa Musa kwenye Mlima Sinai. (Kutoka 24:12-18) Zile Amri Kumi zimeorodheshwa kwenye Kutoka 20:1-17 na Kumbukumbu la Torati 5:6-21.

4 JE tuna ushahidi Gani kama Quran ilishushwa na Mungu?

Natamani Mjadala Huu tujikite kwenye kujibu hoja sio Dini .

Natanguliza shukrani nyingi.

Qur'an haikushuka jinsi unavyodhani.

Qur'an ni ufunuo alioshushiwa Mtukufu mtume Muhammad (saw) na Allah kupitia Malaika Jibril (as), yaani Wakati ufunuo wa Qur'an ulipokuwa unaanza malaika Jibril alimfahamisha Mtume (saw) kupitia Wahy ili awaandae Waandishi kwa ajili ya kuandika kile ambacho wakati huo atakuwa anafunuliwa,

Ukiangalia Qur'an mwanzoni mwa Sura zake inanza na; بسم الله الرحمن الرحيم, yaani kwa jina la Allah Mwingi wa rehema na ukarimu, hapo wale waandishi huanza kuandika wakijua Kwamba hapo ndio mwanzo wa ufunuo na waliendelea kuandika hadi mwisho wa sura, baada ya ufunuo kumalizika hapo ndipo mtume (saw) aliwaambia wale waandishi waanze kumsomea ili ahakiki kwani Mtume (saw) baada ya kufunuliwa Qur'an ilinasa hapohapo kwahiyo kama katika kuandika kungekuwa na makosa basi hapo angeyasahihisha.

Qur'an yote iliandikwa kwa kipindi cha miaka 23, miaka 13 Mtume (saw)akiwa Makkah na miaka 10 akiwa Madina.

Hadi mtume (saw) anafariki Qur'an ilikuwa imeandikwa kwenye vipande vya ngozi na magome ya miti maalumu ya kuandikia (scrolls) nk na ni kipindi cha Khalifa Seydna Umar (ra) ndipo alipofanya juhudi ya kuikusanya na kiuweka katika jalada moja (compiled in one volume from the scrolls) na hizi Qur'an za leo zilizoandikwa kwenye karatasi za kisasa zimetokana na hiyo Qur'an iliyokuwa compiled na khalifa Hadhrat Umar (ra), hiyo ni historia fupi ya jinsi Qur'an ilivyoshuka/ilivyoshushwa.

Inaonekana kilichokuchanganya ni neno "kushuka/kushushwa" ukadhani kwamba inaposemwa kitu fulani kimeshuka hususan kutoka mbinguni basi huenda kitu hicho kimetoka mbinguni kidhahiri.

Neno "shuka" limetumika sana katika Qur'an kwa maana ya kuja, kutokea, kupatikana nk kwa kitu chenye manufaa makubwa kwa binadamu, neno mbinguni nalo maana yake ni ulimwengu wa kiroho, ulimwengu wa heshima nk hivyo inaposemwa Qur'an imeshushwa kutoka mbinguni maana yake ni hiyo tu Kwamba Qur'an imeshushwa au imekuja kutoka kwa Mungu na sio vinginevyo.

Mfano; katika Qur'an Mungu anasema; "--- na ametushushia wanyama wanane" (39:6 Qur'an), je hapo unaweza sema Wanyama hao 8 wemeshushwa kutoka juu (mbinguni)??

Pia Allah anasema; قد انزل الله اليكم زكرا , yaani; bila shaka Allah amewashushia ukumbusho (Qur'an ), (65:10)

Isitoshe Allah anasema; و انزلنا الحديد yaani; tukakishusha chuma (57:25), hapo Allah amesema "tukakishusha chuma" haina maana kwamba Chuma amekishusha kutoka juu/mbinguni bali maana yake ni kwamba Chuma kinayo faida kubwa kwa binadamu ndio maana Allah kasema kakishusha na hivyo ndivyo inaposemwa Qur'an imeshushwa maana yake ni hiyo hiyo kwamba Qur'an inayo faida kubwa sana kwa binadamu.
 
Nasubiri mtu mwenye majibu ya uhakika wakuu.

Sijapata Bado jibu lenye mashiko........
 
Back
Top Bottom