Msaada: Mama yangu kaolewa na kijana umri sawa na sisi wanae

Akuna kitu nilikuwa na pinga kama hiki ila niliamua kuacha baada ya kuona kumbe nao wanateseka kukaa bila mwanaume
Mimi mama yangu ameolewa na kijana ambaye mimi nina mzidi umri na nina muita baba ndo chaguo la mama yangu
Aibu sana.
 
Vijana acheni kuwala mama zenu,hao tuachieni sisi wastaafu.
Mwisho wa siku mnakuja kuwaambukiza magonjwa ya zinaa ikiwemo ukimwi mama za wenzenu.
Vijana mnajitafutia laana kuwavua pichu mama watu wazima.
Pole mleta mada aisee!
 
Mimi naona uachane na mambo ya bimkubwa wako..muombe Mungu akupe nguvu ya ku focus kwenye mambo yako.
 
Mimi mama yangu ameolewa na kijana ambaye mimi nina mzidi umri na nina muita baba ndo chaguo la mama yangu
Inahitaji roho wa Mungu kutekeleza hili uliloandika hapa.

Labda kumheshimu tu, sio kumwita baba mtu ambaye nimemzidi umri...hapana kubwa.
 
Usingejibu hivyo aisee
 
Dogo usisikilize maneno ya kuambiwa. Mama yako yuko katika mikono salama kabisa. Mimi ndiye baba yako mdogo. Kiukweli nina miaka 72! Na siyo hiyo 25-40! Kama ulivyo danganywa na hao wambea.

Tunaishi maisha yetu ya kawaida tu huku Ukumbi, Wilayani Kilolo Mkoani Iringa. Na tunaprndana kweli kweli. Mafinga tuhama miezi miwili iliyopita. Ukifunga chuo pitia uje utusalimie. Piga kitabu mwanangu. Acha kabisa kumsikiliza mzee wako. Taarifa nyingi anazo kuambia kumhusu mama yako, hazina ukweli hata kidogo.
 
Tuliza pumb zako kijana
acha kufuatilia mambo ya mama,
wewe angalia huyo ni mama yako full stop inatosha
mpe heshima yake kama ulivyokuwa toka mwanzo hayo maisha yake achana nayo
pokea simu ya mama ongea naye vyema kabisa ,
usiingilie maisha yake hata kidogo,
haujui mama amekumbwa na nini huenda kwa namna mnavyomuona wa ajabu ndio unazidi kumpoteza mama, hakuna mtu mzima aka namna hiyo isipokuwa kukiwa na jambo lisilokuwa sawa.

Ukipotezea Utakuja kunikumbuka, hauwezi pata mama mwingine jitahidi sana tena sana muangalie mama usiangalie maisha mengine binafsi
 
Mkuu kua 'strong' una sababu bilioni za kufurahia maisha .
 
Daa mbona unamuumiza mwenzio?
 
Yaani acha kabsa mkuu,hii dunia nimeamini usione mtu asaidii wazazi au ana mawasiliano mabaya na wazazi wake ukamshangaa,vijana tunapitia mengi sana ila yote tunamuachia mungu
Kwa hili nakuunga mkono, kwenye familia hizi kuna siri kubwa, kuna wazazi vichomi, pole sana wewe achana naye ndoa ya wazazi uiache kama ilivyo Baba yako anajua anachokitafuta Mama yako na hawezi kutoa siri hiyo.
 
Mama, Baba, mtoto haiwezekani wote wakafanana akiri, hii ni chai
 
Pole sana, kama ambavyo wazazi wetu hupata maumivu makali sana pale sisi watoto wao tunapofanya mambo ya ajabu ajabu vivyo hivyo na sisi watoto wao huwa tunaumia sana pale mzazi anapofanya mambo mabaya
 
Nakujibu kiume: kuna siri kubwa hapo, mzee hamridhishi mama; na mama bado yuko hot, nachokushauri, pambana na maisha yako kwa sababu na wewe ni baba mtarajiwa.
Nimeandika huko juu wadau wamenimwagia mapovu,sijui kwanini watu hawapendi kuambiwa ukweli!
 
Kwenye kuolewa na kijana mdogo hapo hakuna tatizo ni mapenzi yake afu ni ishu binafsi sana hiyo
Haiwezekani MAMA MZIMA unaolewa na kijana sawa na umri wa mtoto wako wa kumzaa! HUO NI UPUMBAVU!

Eti mapenzi! Mapenzi gani hayo ya kuaibisha watoto wako!

Mama gani hana hek'ma hawezi hata kujisitiri mbele ya wanae?
 
ndugu umepanici sana aisee, hili ni suala la maoni tu hupaswi kupinga maoni ya mwingine nawewe toa maoni yako,
chuki siku zote sio jawabu,
na panapouma ndipo penye lathamani zaidi la kujifunza,

kwa mfano ndugu ukiona mama yako wewe anafanyiwa hivyo unaenda kumtoa huko au unakuwa unamchunga kama demu wako au inakuwaje?

ushauri wakujenga ni mzuri sana kuliko wa kubomoa, aibu na fedheha ni uchaguzi tu, sio kila unaloliona wewe kila mtu anakuwa nalo.

hebu chukua nafasi wewe ndio mama yangu unakazwa na bodaboda huko halafu falimilia yako tunakutenga na kukuchukua, na fika haukuwa hivyo toka tukiwa watoto wadogo hadi tukuwa wakubwa imetokea tu umebadirika gafla mama yetu, hakuna ndugu anayejua ni nini unapitia, hakuna anayejua uko sawa kiakili au hauko sawa, kila ndugu anakuangalia kwa namna ya zamani na kuona kwasasa umeamua kufanya makusudi,
hakuna anyekuangalia na kutaka kuwa msaada kwa hali ya sasa, hivi unadhani ungejisikiaje mama yetu? huwenda una tatizo kubwa sisi hatujui tunakuchukia tu ungejisikiaje mama yetu?

Sikia bro uchungu unaouona hapa ndio huohuo hata mkeo au demu wako anaupata unapokuwa unachepuka hili liwe funzo kwako kuwa mtakatifu kwa mahusiano yako ili usiwe mfano mbaya katika jamii ukawe mfano mwema.
Above all mama yako hata awe anauza nyapu hatabadirika kutokuwa mama yako atabakia kuwa mama yako vilevile hadi anaingia kaburini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…