Msaada: Mama yangu kaolewa na kijana umri sawa na sisi wanae

Sawa lakini usiandike kama vile ni kitu cha kawaida.
 
Sawa lakini usiandike kama vile ni kitu cha kawaida.
Yaani niwewe tu ulichukulia ukawaida wakati watu tumelichukulia uzito, kuna muda katika maisha wema ni bora sana kuliko chuki, maana unaweza yaona mambo mengi sana ambayo katika chuki hayaonekani
 
nawewe tafuta mzee kuliko mama ako umuoe
 
Dunia Ina mengi Sana machafu ambayo mengi yao chanzo ni mchafuko wa roho. Roho ndio uongozwa mwili. Watu wengi sana Wana maradhi ya kiroho kuliko mwili. Ndo maana unaona vurugu nyingi kwenye ndoa, mahusiano, watoto kuvuta bangi, ushoga, ukahaba, nk. Haya ni maradhi ya kiroho na tiba zake ni za kiroho pia. Check wataalamu wa tiba za kiroho wanalo jibu. Hakuna tabia yeyeto isiyotibika kiroho. Roho ikiwa chafu matokeo uonekana mwilini.Hii duniani ina siri nyingi na Ina elimu nyingi Sana.
Check wataalamu wa kutibu roho watakusaidia atatulia.
 
Pole Sana ndugu .. hapo mzazi wako alichokosea ni kuhuza mashamba na kujiingiza kwenye madeni kitu ambacho kitawaumiza nyie hapo badae, maswala ya mapenzi hayo nahisi yasikupe stress japo Kwa umri wake ajafanya poa lakini ni maamzi juu ya mwili wake. Tuliza Mawazo umwombee Kwa Mungu arudi katika njia salama maisha yaende .

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Daah....kwahiyo dogo anamkunja bi mkubwa na kumkamulia halafu hujui cha kufanya! Endelea kusubiri amvunje uti wa mgongo ukamtibu.
Ila wazazi wengine wanatia hasira sana
 
Pole sana aisee. Hili jambo ni zito kiukweli. Kwa sasa cha kufanya ni kufocus tu na mambo yako aisee, hakuna namna. Kadri muda unavyokwenda utajikuta akili inatulia na hili jambo halitokuumiza tena kichwa
 
Haiwezekani MAMA MZIMA unaolewa na kijana sawa na umri wa mtoto wako wa kumzaa! HUO NI UPUMBAVU!

Eti mapenzi! Mapenzi gani hayo ya kuaibisha watoto wako!

Mama gani hana hek'ma hawezi hata kujisitiri mbele ya wanae?
Mapenzi ni upofu, ref. ufaransa
 
Jitahidi kumuheshimu huyo babaako wa pili
 
Mambo ya ndani (chumbani) ya wazazi waachie wenyewe, shukuru huyo mama yako alikuzaa akakulea akakukuza hadi Leo hii upo chuo kikuu ,vinginevyo angeitoa mimba yako au kukutupa au kukuuua au vyovyote vile
 
Wewe chukua ushauri wa Baba yako,kazania kitabu tu usimuwaze kabisa huyo Bimkubwa wako. Kama ni muumini basi muombe Mungu akutie nguvu.
 
Actually inaumiza sana bt jikite katika kujenga Future yako...Suala hili linahitaji Muda kwa maana si jambo la kawaida huenda kuna kitu flani hakipo sawa kwa Mama yako huyo...Once again lipeni Muda hili suala as you know Muda ni mwalimu mzuri sana.
 
Kijana mapenzi uondoa stress,kwa baadhi ya watu na wengine wakila ndumu au fegi wanaondoa stress wengine pombe na club,wengine wakikosa bando wanachanganyikiwa japo aperuzi myandao ya kijamii kutwa nzima,akikosa tu stress
Turudi kwa mama inawezekana yeye ni kati ya watu wanaopoteza stress kwa mapenzi
Hayo yanaweza kukuta pia nawe,maana kujijua unazeeka unaweza kujua ila unaweza kujiona bado hujamaliza maarifa mengine na ukajikuta unajishangaa mwenyewe wakati watu wanakushangaa
Mimi nikiangalia age yangu najitambua kabisa tayari nimekwisha ila najiona kama bado kijana
Na wakati age yangu inabadilika nilikuwa nashangaa na amkiwa na kijana mkubwa tu baadhi ya sehemu na baadhi ya wanawake wakiniamkia na wengine kunisalimia kama malingana nao,
Hapo ilibidi nijikubali kuwa nimekuwa mzee sasa
Kuna wakati nikiibua wanawake ,nikiwa katika uhusiano nao anaweza kuniambia wewe unalingana na baba yangu!! Hapo ndipo nilipochoka
Mimi ni mmoja wa watu ninao ondoa stress kwa mapenzi yaani Hata niende sehemu niangalie mabinti na mavazi yao ya kisasa,kwenda beach vile so nainjoy sana
Mwache mama yako ainjoyo ila asikuaibishe tu kuwa malaya
Umri ni namba tu kama kajara na harmo[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Ni muhaya, mrangi, nyaturu, mmbulu au kabila gani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…