Msaada: Nataka kwenda Ustawi wa Jamii, baba wa watoto ananisumbua huduma

Ukweli.
 
NANI ANAWAJIBIKA KUTOA MATUNZO YA MTOTO.
Kifungu cha 41 cha Sheria ya Mtoto ya 2009 kinasema kuwa wajibu wa kutoa matunzo ya mtoto upo kwa mtu anayetambulika kama mzazi.
Kifungu hakikutaja jinsia ya mzazi bali kinamtaja yule ambaye ni mzazi. Hii maana yake ni kuwa kila mzazi awe baba au mama anao wajibu wa kuwajibika katika kutoa matunzo ya mtoto.
Kifungu kinasema mzazi atawajibika kutoa yale mahitaji yote muhimu kwa mtoto( necessities).
Kifungu cha 8( 1 ) cha sheria hiyohiyo nacho kinaeleza kuwa wajibu wa kutunza mtoto ni wa mzazi, kwa maana ya mzazi yeyote kati ya wawili.
 
Naam kabisa mkuu.
Wanampump na yeye anajaa kisha wao waliomjaza wanaendelea na maisha yao.
Haya mtoa mada njoo soma comment ya mdau hapa.
Kukusaidia ni kwamba jali utu kwanza kabla ya hiyo pesa.
Nenda taratibu,zungumza na mwenza wako kwa kuwa ni lazima mmoja ajifanye mjinga.
Hao wanaomwambia wanamudu kulea peke yao kuna muda wanalia pekeyao chumbani kwa kiwa single mama
 
chanzo uhuni alikuwa muhuni sana ila mimi nilikosea kununa kumfwatilia kuhusu simu naongea ukwel kabisa sijui utoto ujinga au nilipenda sana

nmekuj shtuka kushakucha kumchunguza mwanaume japo na yeye alikosea kwa upande wake hakuwahi niheshimu
Dah ila wanawake muwe makini sana unapotaka kumbadili mwanaume wako juu ya swala la kuwa na wanawake nje yako. Kabla haujaanza kumforce na kutumia nguvu kumcomtrol me nashauri anza kwanza kuona nini kimepwelea ndani hapo anachokwenda tafuta huko nje.
 
Kwani wakati ule Adam anapewa Majukumu ya Kula Kwa Jasho pale Bustanini Eden ulidhani ilikuwa no Adam yule Pekee.

Ilikuwa ni Jukumu la Kila Mwanaume kula kwa Jasho.

Jukumu la Mwanamke ilikuwa ni Kuzaa kwa Uchungu tu, hivyo Boss wangu



Ni zaidi ya hivyo aisee.

Neno la Mungu ni full package.

Usichukue andiko moja tu.

Mwanamke anatakiwa kuzalisha mali na kulea familia.

Soma Mithali 31: kuanzia mstari wa 10 hadi mwisho,

Hapo utaona jinsi mwanamke anavyotakiwa kuwa Kamanda Na mzalishaji mali Kwa manufaaa ya familia.
 
Ashasema ndoa sio priority yake,,asa nazani unaelewa ni mwanamke wa aina gani uyu...
Na huyo mzazi mwenzake keshamsoma ndio maaana kaamua aendelee kutafta maisha kuliko kudeal na mwanamke ambaye hajui hata ni kwa nini alimtafta huyo mtoto.
Wanaume tunapenda sana kulea watoto wetu ila tunaposhtukia kwamba mwanamke hashi kwa akili zake bali za kushikiwa huwa tunaangalie anaejielewa.
So,anataka amfanye mtoto kitega sio duh kagonga mwamba sasa.
 
yaan tushakuwa chui na panya sujui nifanyaj maan hazungumzi na mimi kbs anapitia kwa dada yangu ila sio mm
Kama anaongea na dada yako basi bado kuna nafasi ya kuweka mambo sawa. Hebu rudisha ukaribu nae mapema sana kabla mambo hayajawa mabaya zaidi.

Ongea na dada yako akuombee nafasi ya kukutana na jamaa. Kisha msikilize terms zake anataka nini kubaliana nazo halafu taratibu mfanye aone kuwa unashirikiana nae kwenye swala la watoto sio kushindana nae.

Wanaoteseka hapo ni watoto sababu ninyi mnachagua kushindana badala ya kuishi pamoja. Kaa nafasi yako ya mwanamke muache yeye akae nafasi yake ya mwanaume. Usimpangie usimuingilie.
 
Mara zote nilizosikiliza kesi za wanawake wakiwalalamikia wanaume niliamini wanaume wenzangu ni mashetani

ila nilipopata nafasi ya kusikiliza na upenda wa wanaume wenzangu niligundua kumbe wanawake wale ndo walikua mashetani ila wana uwezo mzuri wa kuvaa sura na maneno yanayo shawishi kuonewa huruma ili waonekane hawana hatia
 
Ngoja nipate wasaa niisome hiyo Mithali ya Mfalme Suleimani.

Ila agizo Mama ni Mwanaume kula kwa jasho ikiwemo kutunza familia.

Mwanamke anatakiwa kukuzalia watoto hata 12 kama uzazi anao, ila jukumu let sisi Wanaume ni kuhakikisha tunahudumia familia
 
Dah mkuu hii ilipaswa kuwa comment namba moja ila ndo hivyo tena.
Lakini pia haijachelewa,itamsaidia kushusha temba na hayo manegative aliyojazwa kwenye ubongo.
Wenzake wakiamua kudanga wanadanga wee then wakiamua kuzaa wanazaa afu wanakuwa wapole.
Hakuna mtu yuko tayari kuhudumia mtoto ambaye anaishi na mama aina hii
 
sawa nitajaribu kuweka mambo sawa ila kwa yeye anaonekana hataki kabisa tushajaribu sawa sijui nifanyaje aseee nawaza sana nahis nina depression
 
tajiri mkopeshaji wewe ni jiniazi,,,,,,ngoja nitafute nauli nikapate mafunzo mahususi jinsi ya kuwatawala hawa viumbe kule AFGHANSTAN chini ya mwalimu aitwae HAFIF kutoka kundi la TALEBAN,,,ndo manake TALEBAN wamewazuia hamnakufanya kazi wala kwenda skuli,,,,ni kukaa nyumbani na kuingiziwa TANGO tu ndo kazi yao!!!!!bwana mkubwa hili la stroke wanaume wenyewe tunalitaka,,,mtu anakunyanyasa,anakunyima unyumba,unakusema vibaya kwa ndugu,jamaa na marafiki,mbaya zaidi mpaka kwa watoto,,,,utaskia anawaambia watoto "mnamwona baba yenu alivo mlevi,yaani bila mimi mtakufa njaa,kumbe ela unatoa wewe"matokeo yake msongo wa mawazo mpaka unapata stroke!!
 
sure uyu dada anaitaji ushauri mzuri..hao wanaharakat wanazidi mvuruga.mafeminist na masingle Maza furaha yao ni kuona wengine wakiharibikiwa..

Kamwe usipokee ushauri wa single maza sabb weng wao tayar washakua abnormal kiakili.😂😂😂
 
Sure mkuuu wanaume wengi wanakufa na tai shingoni, lakin wanayataka wenyewe!!

Huwezi pingana na agizo la Mungu ubakie salama. Mungu ameagiza mwanaume mtawale mkeo afu ww unakuja na habar za huruma sijui ubinadam mara haki sawa!! lazma utafeli.

Mwanamke atawaliwe ndani ya ndoa!!abakie na machaguo mawili atawaliwe Kwa hiyari?ama atawaliwe Kwa nguvu? lakin lazim atawaliwe Kwa namna yoyote.. wanaume wengi wanaponzwa na huruma na mwisho wa siku ndio vifo vya pressure na stroke!!!
 
WEKA AYA KWENYE UANDISHI WAKO.
UNATEGEMEA MATUNZO YA WATOTO NDIO UISHI AU?
ANDIKA VIZURI NI SOME NIELEWE.
PUNGUZA HASIRA NA JAZBA, KAA UFIKIRIE HASA UPATE SHUGHULI UFANYE ILI UKIPATA MATUNZO YA WATOTO YASAIDIE KWELI WATOTO.
KUNA MNOKO HAPA AMESHAURI UFIKE OFISINI KWA MJUBA, ANZIA HAPO.
USISAHAU KUTUPA MTEJESHO KILA HATUA.
 
Dah ila wanawake muwe makini sana unapotaka kumbadili mwanaume wako juu ya swala la kuwa na wanawake nje yako. Kabla haujaanza kumforce na kutumia nguvu kumcomtrol me nashauri anza kwanza kuona nini kimepwelea ndani hapo anachokwenda tafuta huko nje.
ushauri Bora wa thread....
Kama hatosikiliza huu ushauri basi hakuna namna ya kuweza kumsaidia uyu mama.!!
 
Pambana mwenyewe dada. Baadae watoto wakipata mafanikio utamuona huyo anajileta kama baba Mondi. Na hiyo ndo Itakuwa adhabu yake.
 
uyo ni mmoja ya watu wanafiki anataka sehem yenye rangi nyeusi tuseme nyeupe!! Watu wanafunguka ktk mitazamo mbalimbal kusudi mhusika ndio achambue achukue lipo na aache lipi..asa uyu Trudie anataka wote mumshauri kama anavyopendelea yy...kitu ambacho ni nonsense 😂😂😂
 

Jamii yetu ndio iko hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…