Nilitamani sana nisiwashwe kuchangia hii mada lakini nimejikuta nashindwa. Nianze na wewe
mama cutest, kwa uandishi huu nilivyojudge haraka haraka una umri mdogo. Kama nimekosea samahani sana.
Sasa my dear..maisha yako ni ya kwako pekee. Sisi wa mtandaoni hatuishi na wewe. Wewe ndo unajua machungu, adha na kadhia unazopitia. Naelewa suala la malezi ni gumu sana tena hasa ukiwa solo.
Lakini kwa ninavyokusoma, kuna pride, hasira inakutafuna deep inside. Na ndo maana umesema una depression. Una chuki na mzazi mwenzio na possibly unatamani hata baya limfike kwa sabbu ya aliyokufanyia. Sikulaumu..pole!!
Lakini my dear, sisi tunapenda kuchangamsha genge humu. Kila mtu na maisha yake humu. Kuna waliokuwa kama wewe lakini kwa kudra za Mungu wameweza kusimama na wanalea watoto wao wenyewe..well and good, ila sasa kwa upande wako, kaa chini, samehe kwanza..maana ndo utaweza kufanya maamuzi sahihi. Kuna wengine tunakwambia pambana umlee lakin huna moja wala mbili. Utulivu na busara vikusaidie ili uweze kujua namna ya kumlea m/wa toto wako vizuri kwa kushirikiana na mwenzio. Hakuna faida ya kutunishiana misuli.
Na hii ni kwetu sote. Kama unaona hutaki ushauri unaoumiza, usiandike unachokipitia na sisi tukasoma. Kumbuka tuko watu wa kariba tofauti humu. Haipendezi kila siku tunakua kwenye misuguano and we can avoid that. Wengi wetu tunaandika shida na tunachagua maneno tunayotaka kusikia..its crazy. Sentensi tunayoipenda wanawake ni fainali uzeeni. Hii sentensi imebeba kisasi, uchungu, hasira nyuma yake. Na inaamanisha kwamba unatamani mwenza wako limkute baya uzeeni ili akome. Resentment..haina manufaa, zaidi ukija kumuona uzeeni anang'aa utaramani umroge maana ulichokitamani hakijamtokea.
NoJanga la Single mama kwa juu juu limemfanya mwanamke victim. Lakini deep down wanaume wengi ndo mavictim. Hii ni mada nyingine. Tumeshakosea..tusizidi kukosea. Haina maana yoyote kila mara kuja kubishana mitandaoni..lets amend our ways na tumtegemee Mungu katika malezi, lets be humble and wise. Ukikaa katika haki, Mungu atakusaidia huyo mtoto akue vizuri na akikusaidia no kujisifu bali uwe mnyenyekevu sio useme nimepambana mwenyewe, nimefight, akati hata oxygen Mungu ndo amekupa.