Msaada: Nimeuza nyumba, niliyemuuzia hataki kunimalizia fedha yangu mwezi wa nne huu, nikiuza tena kuna kosa?

Piga risasi mshenzi kwanini akusumbue miaka nenda rudi
 
Chukua hela Mkuu, huko Mabaraza ya ardhi sio poa unaweza kupitisha miaka 5 bila kuona haki ni ya nani!
 
Mimi niliuza nyumba Ili ninunue nyingine nae anajua. Anafahamu anavyonilipa na Mimi NAENDA kulipa kule. Kuvheleweaha kwake kunilipa kumenifanya nikose nyumba na nimekatwa hela ya usumbufu.

Mkataba wetu ulitemgemezwa na mwanasheria wake na yeye, unasema hela ikichelewa atalipia ASILIMIA 18, , yeye hataki kumlipia ASILIMIA 18, na amepitiliza miezi minne. Tena nimekuwa mstaarabu nimemwambia alipoe ASILIMIA hizo za mwezi tu hataki anakuwa mkali. Nimegundua hicho kipengele aliweka Ili nikubali alipoe nyumba miezi sita.

KINACHONIUMA SANA alipolipa Ile awamu ya kwanza ambayo ilikuwa milioni 10 kati ya 50m alienda akawafukuza wapangaji wangu alisema yeye tayari amenunia nyumba. Kistaarabu alitakiwa angojee amalize kulipa ndo maswala ya wapangaji yafaye kwani nao Wana haki zao. Na kwenye mkataba iliandikwa kabisa Mimi nitaendelea kukusanya Kodi mpaka siku amalize kulipa ndo nyumba inakuwa Mali yake. Sasa mkuu tangu mwaka Jana mwezi wa kumi na mbili Hadi Leo huoni hasara anazonitia Tena makusudi?
 
Kabla sijasaini huo mkataba nilipeleka kwa wanasheria na tukajiridhisha ndipo nikasaini. Hadi mwanasheria wake anamshangaa sana.
 
Pole sana! Ni kutokujua,. Japo wengine pia tunajifunza hapa,. Ilitakiwa hayo yote yabainishwe kwenye mkataba. Nyumba ingebaki chini Yako hata kuchukua pango Hadi atakapomaliza malipo yote,. Ilibidi iwekwe wazi na kukuruhusu wewe kuuza nyumba pale atakapo shindwa kutimiza masharti. Sasa umegeuka mtumwa wa kumsikiliza na kumnyenyekea yeye. NB: Ndugu chukua fedha fanya mengine mtasumbuana Bure na mwisho fedha itaisha yote hata kiwanja hutopata.
 
Na mkataba una expire date, na according to him mkataba usha expire hadi sasa!!
 
Either umrudishie pesa alizokupa mmununuzi wa kwanza. Au uuze halaf utoe kidogo umlipe

Lakini hili itabidi umkalishe chini uongee nae
 
Kama mkataba kaandika mwanasheria wake chukua hela sepa hata usiangalie nyuma. Kwenye kesi utapoteza zaidi. Nina ndugu yangu kesi yake ilianza mwaka 1994 kuhusu ardhi hadi leo inaendelea.
 
Siyo rahisi kama unavyo zani, hakuna kazi ngumu kama kumnyanganya tapeli Aridhi, maana ameshajipanga na kuna sehemu anategemea kupata msaada wa kuzulumu!!
Akamhukumu mahakama ya mnyonge kilinge. Kucheza na wapuuzi ni kupotezewa rasilimali pesa na muda.
 
Jana kuna mtu alikuwa anafafanua case ambazo polisi hapaswi kuingilia hii ni mojawapo🤣
 
Haha, hii nchi Kuna ilivyo na inavyopaswa kuwa.
Oya acha tu unaambiwa zile style za flani kakudhulumu sijui au kakutapeli unakimbilia dawati la askari kwamba wamtaitishe ili alipe ni kosa kisheria. Au kumuweka ndani mtu kwa ishu hizo haikubaliki🤣!

Nilimsikiliza yule msenge kwa makini kisha nikatabasamu tu ila niliporomosha tusi kimoyo moyo ili wife asiskie na watoto.
 
Chukua mpunga halafu isimkabidhi waraka mpaka akupe ile asilimia ya kuchelewesha malipo kama kweli ipo kwenye mkataba. Tena mwambie akutilie kwenye bank account asijekukubananisha ya nipe nikupe.
 
Jambo kama hili labda Raisi aliseme hadharani ndo wananchi watafunguka. Hata hivyo huwa wanageuza kesi utasikia inasemekana umetishia kumuua hivyo tunakuweka ndani kwa uchunguzi.
 
Jana kuna mtu alikuwa anafafanua case ambazo polisi hapaswi kuingilia hii ni mojawapo[emoji1787]
Madai sawa police hapaswi kuingilia ,ila wajanja wanakugeuzia kesi ya utapeli wa kujipatia Fedha kwa njia ya udanganyifu ,hapo kesi ya madai inageuka kua criminal case!!
 
Chukua hela hiyo mkuu alafu next time ukiuza nyumba, kiwanja ama gari usikubali kuuza kwa installment yaani hata kama atasema hela ngumu wewe mwambie akope sehemu alafu atawalipa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…