Kwanza ulifanya makosa sana kukosana na baba yako kwa ajili ya vyama vya siasa. Baba duniani unaye mmoja tu, hivi vyama vinakuja na kuondoka, lakini baba ni baba tu. Palepale ulipaswa kukubaliana naye, hata tu katika hali ya kumridhisha, lakini sio kugombana naye kabisa.
Hukupaswa kamwe kumdai baba yako hilo laki saba, huyo ni baba yako. Mambo mangapi amekufanyia wewe? Na bado ulikuwa unakaa kwake, nyumba bure, chakula bure, maji bure, umeme bure, labda hata ukiugua mzee anahaingaika, tv (kama ilikuwepo) bure na mambo mengi alikuwa anakufanyia, Kweli ulishindwa kabisa kuachilia hiyo laki saba? Jinga kabisa! Sasa hiyo laki imekufikisha wapi?
Haya ukamdai na kumdhalilisha mzee wa watu mpaka serikali ya mtaa, huko ni kujitafutia laana kabisa. Ninaongea kama baba na moyo unaniuma kuwaza kuwa mtoto niliyemhudumia tangu akiwa hajitambui mpaka hapo halafu anageuka na kwenda kunishtaki! Hilo lilikuwa ni kosa kubwa mno!
Kujionyesha usivyo kuwa na uwezo hata wa kupambana na kujitegemea mwenyewe unarudi kwa baba huyo huyo uliyemdhalilisha! Halafu unategemea ukuchekee tu! Hivi watoto wa siku hizi mnakwama wapi kwenye hizo akili zenu? Mnajifanya wajanja mpaka mnadhalilisha wazee wenu kumbe kichwani hamna kitu kabisa!
Ungelikuwa kweli mjanja ungelipambana utoboe mwenyewe! Una zaidi ya miaka 30 halafu unarudi kwa baba kulia lia, bure kabisa!
Yaani wewe unarudi tu kwa baba maisha yakikugonga, maana yake kama mambo yako yangelikuwa mazuri usingelirudi kabisa kwa baba yako! Hii ni akili au matope?
Wewe sasa ni mtu mzima, hupaswi kabisa kumtegemea baba yako kuendesha maisha yako, unapaswa kujitegemea mwenyewe.
Kwa taarifa yako hakuna sheria yeyote ile inayomlazimisha baba kuendelea kumtunza mtoto mwenye umri kama wa kwako! haipo hiyo sheria, hivyo hakuna utakapoweza kwenda wakakusaidia!
Unachotakiwa kufanya, kwanza fahamu kuwa umemkosea sana baba yako na ulimdhalilisha mno, na hivyo uwe tayari kumuomba msamaha ili uhusiano wa baba na mwana urudi, sio tu ili kwamba upate mahali pa kukaa.
Pili, tafuta mzee wa karibu na baba yako, anaweza akawa baba mkubwa au mdogo, mjomba, hata rafiki yake. Uende ukaongee naye taratibu, huku kweli ukionyesha kutambua na kukiri makosa yako na kuomba msamaha.
Tatu, pambana kwa ajili ya maisha yako, sio kila saa unarudi kwa baba kulia lia kama mtoto wa chekechea.
Nne, vijana wote muwe na adabu kwa wazazi wenu, achaneni na huo upuuzi wa kileo.
Mwisho, nawaomba msamaha wote kwa kutumia lugha kali kidogo! Admin, please do not punish me