TANZIA Msajili wa Vyama vya Siasa Mstaafu, John Tendwa Afariki Dunia

TANZIA Msajili wa Vyama vya Siasa Mstaafu, John Tendwa Afariki Dunia

Jamani tufanye yote lkn tukumbuke Mungu yupo.
CCM hawajui hilo. Ndiyo maana wanapotelea kuzimu. Wanasema wanaiba uchaguzi baadae wanaenda kutubu. Wanadhani Mungu ni mjomba wao. Mwisho wanajikuta wamejazana kuzimu na huko hakuna vyeo wala uchawa.
 
mzee Tendwa nilikuwa napenda sana anavyozungumza kiswahili chake.

Nakumbuka wakati wa CCJ alitumia vocabulary fulani ya kiingereza kusema hiki chama hakipo.

Alikuwa ni miongoni mwa viongozi wachache sana wakati huo wanaozungumza kiswahili fasaha kwenye media na public.
Viongozi wengine waliokuwa wanatamka kiswahili kwa ufasaha wakati huo ni marehemu mzee Samuel Sitta, na Mama Dk. Asha Rose Migiro, na hata Mwina Kaduguda japo Kaduguda hakuwa kiongozi wa kitaifa.
 
Waliohusika kunajisi Sanduku la kura wanapelekewa ujumbe.
 
Aisee!

CCM imeshindwa kuzuia kifo chake kama wanavozuia maandamano ya wasio wana CCM?

Acheni Mungu aitwe Mungu.

GOD BLESS TANGANYIKA
 
Alijitahidi sana kuwa fair wakati akiwa msajili wa vyama. Pia wakati ule viongozi walau walikuwa na hofu ya Mungu.

Mungu amjalie amani na pumziko miongoni mwa wateule wake
Alikua mcheshi sana. Kabla usaji wa vyama vya siasa, alikua msajili pale industrial court kabla ya ujio wa CMA, late 90s
 
R.I.P
KIpindi tunasoma maarifa ya jamiii tulikuwa tunasoma jina lake..
 
Ndugu zangu Watanzania,

Habari ndio hiyo ya majonzi juu ya kifo cha msajili wa vyama vya siasa mstaafu John Tendwa ambaye amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo.

Amekuwa msajili tangia wakati wa hayati Benjamini Mkapa mpaka wakati wa Daktari Jakaya Mrisho Kikwete 2013.

Amepigana vita iliyo njema, Mwendo Ameumaliza na imani Ameilinda .

Bwana alitoa,Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.

Pia soma
- Tendwa amkosoa Msajili wa vyama kuhusu ukomo wa madaraka CHADEMA

View attachment 3178639


Hivi Mungu akimuuliza alisaidia Tanzania watu wapate haki au aliongoza genge la wanyima haki? Na akidanganya anaenda motoni na akisema ukweli anaenda mbinguni Je atajibu nini?

Maisha ni mafupi tuwe makini na tutende haki
 
Back
Top Bottom