Msamaha: Mzee Kinana amuangukia Rais Magufuli kufuatia mazungumzo yake na makada wenzake wa CCM yaliyovuja

Msamaha: Mzee Kinana amuangukia Rais Magufuli kufuatia mazungumzo yake na makada wenzake wa CCM yaliyovuja

Swala la kange lipo kwenye uchunguzi.
Acha kuwa unaandika hovyo bila mpango, wewe ni mkorofi sana

Ukorofi wangu ni nini? Suala la Kange haliko tena kwenye uchunguzi, maana Takukuru walishasema wamekamilisha uchunguzi kwa 99%. Sikushauri utetee uovu kisa unasaka mlo. Huu ni ushahidi wa wazi kuwa hakuna vita ya rushwa, bali kuna kulipizana visasi kwa mgongo wa kupambana na ufisadi.
 
Acha dhana mbaya kwa kila jambo la serikali.Embu wakati mwingine jaribu kuwa na mawazo positive
 
Natabiri
Peter Msigwa yuko njiani kwenda ccm
I can feel it
 
Acha dhana mbaya kwa kila jambo la serikali.Embu wakati mwingine jaribu kuwa na mawazo positive

Sina dhana mbaya kwa kila jambo la serikali acha kunichafua, bali ninakataa kwa nguvu zangu zote uovu wowote. Ni wapi umeona napinga serikali kujenga barabara? Ni wapi umeona napinga ujenzi wa hospitali?

Je, hayo sio mambo ya serikali? Acha kuchanganya mambo ya serikali na matumizi mabaya ya madaraka tafadhali.
 
Sina dhana mbaya kwa kila jambo la serikali acha kunichafua, bali ninakataa kwa nguvu zangu zote uovu wowote. Ni wapi umeona napinga serikali kujenga barabara? Ni wapi umeona napinga ujenzi wa hospitali? Je hayo sio mambo ya serikali? Acha kuchanganya mambo ya serikali na matumizi mabaya ya madaraka tafadhali.
Sasa kama unaona barabara zinajengwa kwa kasi na maendeleo ni makubwa kwa nini mnampinga Rais Magufuli aliesimamia hayo?
 
Kinana alidanganywa na vijana wale wakaandika kiwalaka uchwara kikawatokea puan wengine walienda ikulu kupiga goti huku jasho likiwatoka na miwan ikipanguswa jpm ni hatar
 
Source wapi mkuu ila hii habari kama ni kweli kuna watu watanuna na kupasuka, Maana tayari walishaanza kusema twende na Kinana 2020 haha, Mimi nilisha sema hakuna kitu mtu ataweza kufanya akiwa nje ya mfumo, yaani nchi hii hakuna mtu aliepo nje ya mfumo anaweza kutingisha mfumo never ever hao kina Kinana kwa sasa ni kama mtu uwaoondoe meno afu uwape nyama ambayo haija iva fresh. Hata mkwere anajua ukishakuwa nje ya system huna impact tena
Ukizingatia hao wastaafu wana makandokando kibao
Kinachowafanya wawe wapole nihayo makandokando, Kama wangekuwa wasafi naamini kwa kiburi cha Kinana asingethubutu hata kutaja jina la Jiwe. Kama kweli ameomba msamaha sawa lakini lamoyoni mwake linajulikana
 
Sasa kama unaona barabara zinajengwa kwa kasi na maendeleo ni makubwa kwa nini mnampinga Rais Magufuli aliesimamia hayo?

Barabara zinajengwa na kodi za watanzania. Kama ujenzi wa barabara ndio kipimo cha mtu kukaa madarakani, basi hakukuwa na haja ya sisi kuwatoa wakoloni, au weusi wa Afrika kusini kuwatoa madarakani weupe. Kiongozi sahihi ni zaidi ya ujenzi wa barabara/miundombinu. Rais Magufuli sio rais sahihi, bali alipaswa kuishia cheo cha waziri mkuu. Sina shaka na nilichokosema.
 
Uaimamizi bwashee.Magufuli anasimamia vizuri fedha za walipa kodi.Mkubali Magufuli mambo yaishe.
 
Uaimamizi bwashee.Magufuli anasimamia vizuri fedha za walipa kodi.Mkubali Magufuli mambo yaishe.

Ni sawa, ila akae pembeni wapo watu wanaoweza kusimamia hizo kodi vizuri na bado wakaheshimu uhuru wa watu wengine, na kuheshimu kutofautiana kimitazamo. Hiki sio kizazi cha kuongozwa kwa kushuritishwa kwa utashi wa kiongozi yoyote yule.
 
Hata askari husalimu amri wakizidiwa vitani.

Wanachukuliwa mateka ama wanakula shaba.
 
He he he heeeee uwiiii nilidhani Kinana angemfagilia Membe na lissu. Karudi CCM..... BAVICHA vipi tenaa
 
Ule msamaha aliouomba Mch. Msigwa kwa kinana umeleta taharuki ya kutisha ndani ya Lumumba kwani wanafahamu jinsi alivyo "Kiraka" hasa kipindi hiki cha uchaguzi kinapokaribia.

Kwa yaliyotokea leo ni maagizo ya kumtisha, nae kaingia mkenge maskini mzee wa watu.
 
Back
Top Bottom