Katika vitu ambavyo nimeongeza umakini mkubwa kwenye kuzungumzia ni hii situation ya kuongezeka kwa mahusiano ya jinsia moja.
Soma huu mstari 👇👇
Mathayo 24:15
Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu),
Anaposema chukizo la uharibifu limesimama patakatifu amekazia na ASOMAYE NA AFAHAMU.
Hii situation imetabiriwa na lazima itokee na hakika yanayotokea mnayashuhudia wenyewe. Makaasisi na madhabahu imeshambuliwa na adui na hakika hakuna kilichofichika hata baada ya kauli ya majuzi ya Papa ni wazi atakayeuona ufalme wa Mungu ni yule atakayesimama kwenye toba na kumpendezesha Mungu wakati wote.
Mnapambana dhidi ya nguvu za giza kwa vita ya mwilini. Mapepo yameshaachiwa kutoka kuzimu na utaona mwanaume akiwa na hamu ya kuingiliwa na mwanamke akitamani kumiliki penzi la mwanamke mwenzake....
Tusimame kwenye nafasi yetu kuhubiri habari njema ya ufalme wa Mungu na kumuomba rehema muda wote.
Sisi wazazi wenye watoto tusizembee kwenye kuwaombea na kuwalea ktk maadili ya kujitambua na kadhalika...
Amen