Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Mjinga mkubwa wewe! Ndugu zako vijijini wanakufa kwa kunywa maji wanayochangia na mifugo, wanafunzi wanakosa mikopo vyuoni na wanapewa masharti ya ajabu ajabu, hospitali hazina madawa, vitanda hakuna halafu unasimama kutetea ujinga. Mnachekelea kuona nchi inaingizwa katika hasara ya kulipishwa mabiilioni ambayo yangesaidia huduma za kijamii. Mnafanya siri halafu mtu anayeeleza ukweli mnampiga mkwara wa kumuua? Hayo makombo unayodondoshewa ndio yanakutoa akili kiasi hiki?
 
Kabisa Mkuu na ndiyo sababu yule mama alifanya ujasiri wa hali ya juu kukataa kumfanyia kampeni lakini mafisadi Kikwete na Mkapa wakamshinikiza. Yule mama alijua huyu jamaa hana hata chembe ya uongozi ni janga kubwa la Taifa.

Anashindwa kuiongoza familia yake, mnategemea ataweza kuliongoza taifa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bila shaka na wale wamiliki wa Meli ya Fish iliyokamatwa na bwana yule watakuwa wanaivizia ile terrible teen dreamliner ili nao walipwe fidia ya 1.3 trillion..Ha!hahahaha Just hahahahahaha

Delle Alli
 
MASWALI 10 KUHUSU MAJIBU YA SERIKALI JUU YA NDEGE YETU KUKAMATWA CANADA.

Jana Lissu aliibua mjadala kuhusu ndege yetu kukamatwa huko Canada kutokana na deni la TZS Bilioni 87 tunalodaiwa na kampuni ya Stirling Engineering Ltd, kutokana na kuvunja nao mkataba wa ujenzi wa barabara ya Wazo Hill - Bagamoyo mwaka 2009.

Mjadala ukawa mpana baada ya kupata attention kubwa kwa watu na vyombo vya habari. Mbunge wa Kigoma mjini ZZK akauendeleza mjadala huu kwa kumuita Waziri Mbarawa kwenye ukurasa wake ili ajibu kama ni kweli ndege yetu imekamatwa au lah.

Alhamdulilah. Waziri akajitokeza. Kama mjuavyo Waziri Mbarawa ni mtumiaji mzuri wa mitandao. Mbarawa akakanusha taarifa hizo na kusema ni uongo na uzushi. Akaema ndege ipo na HAIJAKAMTWA, isipokua kuna mambo ya kiufundi hayajakamilika. So yanamaliziwa and soon ikiwa tayari itawasili nchini.

Vijana wa CCM wakamshangilia majibu hayo "mazuri" na wakaanza kumtukana ZZK kwamba anashabikia propaganda za uongo za Lissu.

Leo Naibu Murugenzi ya Idara ya Habari Maelezo, ambaye pia ni Naibu Msemaji Mkuu wa serikali Bi.Zamaradi Kawawa amefanya mkutano na waandishi wa habari. Kwa kinywa chake amekiri kwamba NI KWELI NDEGE YETU IMEKAMATWA CANADA kutokana na kesi iliyofunguliwa mahakama ya usuluhishi ya kimataifa na kampuni ya Stirling Construction Ltd. Lakini akasema wanasiasa ndio wamechochea hadi kesi hiyo kufunguliwa na ndege hiyo kukamatwa. Kwa kifupi amewalaumu sana wanasiasa na kuwabebesha mzigo wote wa kukamatwa ndege yetu.

Maelezo ya Zamaradi leo na yale ya Prof.Mbarawa jana yamenipa maswali yafuatayo:

1. Kwanini Zamaradi amesema Wanasiasa ndio wamechochea ndege hiyo kukamatwa? Ina maana "driving factors" za kukamatwa ndege hiyo ni wanasiasa tu? Just that? How?

2. Kuna uhusiano gani kati ya wanasiasa na kitendo cha kuvunja mkataba na kampuni ya Stirling Constructuon?

3. Wale vijana waliomtukana Lissu na ZZK jana mitandaoni na kuungana na Prof.Mbarawa kusema hakuna ndege ya Tanzania iliyokamatwa, wamejisikiaje baada ya Zamaradi kukiri kuwa ni kweli ndege yetu imekamatwa?

4. Kwanini maafisa waandamizi wa serikali (Waziri na Msemaji mkuu wa serikali) wanapingana hadharani? Waziri anasema ndege haijakamatwa, Msemaji mkuu wa serikali anasema ndege imekamatwa. Je Waziri hakua na taarifa au alidhamiria kudanganya?

5. Je, inawezekana Waziri husika asijue kuhusu suala hili la ndege wakati lipo chini ya Wizara yake?

6. Kwanini Zamaradi hajawataja hao wanasiasa waliozuia ndege yetu kukamatwa? Na kwanini hajaeleza wamezuiaje?

7. Kama serikali ilivunja mkataba na kampuni ya Stirling Construction, na kampuni hiyo ikaenda mahakamani na kupewa kibali cha kukamata ndege yetu, kwanini Zamaradi asiseme kwamba aliyezuia ndege yetu kukamatwa ni Waziri wa ujenzi (wa wakati huo) aliyefanya maamuzi ya kukurupuka, badala ya kuwasingizia wanasiasa?

8. Kwanini serikali haikusema mapema jambo hili kabla Lissu hajaliibua? Walitaka kuficha nini?

9. Lissu alieleza jana kwamba serikali italipa Dola milioni 12.5 (Kama TZS Bilioni 30) ili ndege hiyo iachiwe, wakati mazungunzo mengine yakiendelea (kuondoa pingamizi lililopo mahakamani). Maana yake ni kwamba tukiona ndege hiyo imetua tujue tumeshalipa Bilioni 30 za awali. Je pesa hizo zinatoka wapi? Ni kodi za wananchi? Kwanini Waziri aliyevunja mkataba huo asiwajibishwe kulipa peke yake?

10. Basil Mramba na Grey Mgonja walisababishia taifa hasara ya dola 7.5M sawa na TZS Bilioni 11, wakashtakiwa na kufungwa jela. Je serikali haioni kuna umuhimu pia wa kumshtaki waziri wa ujenzi aliyevunja mkataba na kampuni ya Stirling kwa kukukupuka?
 
Nadhani angetajwa tu huyo mtu kulikoni kuwa na habari za kufikirika maana tuna shida ya kupeana updates yaani serikali ni bora ingekaa kimya kulikoni kuja kujibu hoja baada ya Lissu kuibuka....(mambo mengine huwa yanaibuliwa kwa kuwa wenye dhamana ya uongozi kutokupenda kutoa updates maana ndege ilitangazwa na imekuwa ikitangazwa kwa mbwembwe kwenye majukwaa ya kisiasa itawasili kama muda uliopangwa alafu baadae haijaonekana hivyo kilichotakiwa ni kutoa updates angalau kwa zile kauli zetu za "kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu............."
 
Huyu si tumeambiwa ni punguani ? kwa hiyo hata akichekacheka hatuoni cha ajabu
 
umepata like yangu.Yani umeandika yote ambaye mwenye uelewa angemuhoji msemaji wa serikali.
 
Siku ya jana Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Rais wa TLS Mhe Tundu Lissu alieleza kuwa ndege aina ya 'Bombadier Dash Q400' mali ya shirika la ndege la ATCL imeshikiliwa huko nchini Canada na kampuni moja ya Ujenzi ijulikanayo kama Stirling Civil Engineering Ltd kutokana na kuidai serikali ya tanzania kiasi cha USD 38M (Takribani TZS 87BL). Alieleza pia Kampuni hiyo imetishia kuipiga "mnada" ndege hiyo kufidia deni lao, ikiwa serikali ya Tanzania haitawalipa.
Katika ufafanuzi wake alidai kuwa mnamo Mwaka 2009 kampuni Stirling Civil Engineering Ltd, ilipewa kandarasi yakutengeneza Barabara ya Wazo Hill – Bagamoyo. Kabla ya kukamilisha kandarasi hiyo, aliyekuwa Waziri wa ujenzi wakati huo alivunja mikataba bila kuzingatia sheria, na kuinyang'anya kampuni hiyo kandarasi hiyo na kuagiza kampuni hiyo kutimuliwa nchini.

Kampuni ya Stirling Civil Engineering Ltd, ilifungua kesi katika mahakama ya kimataifa ya usuluhishi mjini Paris. Tarehe 10 Desemba, 2009 mahakama hiyo iliipa ushindi kampuni hiyo na kuagiza serikali ya Tanzania kuilipa takriban dola za Marekani milioni 25 (Takribani TZS 40BL kwa wakati huo).

Serikali ya Tanzania ilikata rufaa, lakini ikaangukia pua kwenye hukumu ya tarehe 10 Juni, 2010 ambapo mahakama hiyo iliagiza Tanzania ilipe fedha hiyo pamoja na riba ya 8% kila mwaka hadi malipo kamili yatakapofanyika. Tuzo hiyo imesajiliwa na kutambuliwa kama deni halali la Serikali ya Tanzania kwa Stirling Civil Engineering Ltd.

Lakini serikali ilikataa kulipa deni hilo, licha ya jitihada mbalimbali zilizofanywa na kampuni hiyo. Kutokana na ucheleweshaji wa malipo, deni hilo limeongezeka hadi dola za Marekani 38.7M kufikia tarehe 30 Juni, 2017.

Hapo ndipo Stirling Civil Engineering Ltd. ilipoamua kuomba amri ya Mahakama Kuu ya Montreal ya kukamata mali zote za serikali ya Tanzania zilizopo nchini Canada zikijumuisha ndege ya Bombardier Q400. Mahakama ilitoa kibali na ndege hiyo kukamatwa.

Kwa mujibu wa Mhe.Tundu Lissu serikali iliomba mazungumzo na kampuni ya Stirling Civil Engineering Ltd ili kutatua tatizo hilo. Katika mazungumzo hayo ambapo serikali ya Tanzania iliwakilishwa na Waziri wa mambo ya nje Balozi Augustine Mahiga, aliomba kampuni hiyo kuepuka suala hilo kujulikana hadharani.

Kwa upande wake, kampuni ya Stirling Civil Engineering Ltd. imekubali kuiachia ndege ya Bombardier Q400 kwa malipo ya mwanzo ya dola za Marekani milioni 12.5 (Takribani TZS 30B) na baadae itatuma ujumbe wake Tanzania kwa ajili ya kuja kufanya makubaliano ya mwisho juu ya kulipa deni hilo. Endapo malipo hayo yatafanywa na Serikali, Stirling Civil Engineering Ltd, itasitisha mpango wake wa kuipiga mnada ndege yetu ya Bombardier Q400. Ikiwa serikali itashindwa kutimiza makubaliano hayo basi ndege hiyo itapigwa mnada.

Siku ya Leo Serikali kupitia msemaji wake, Kawawa wamejibu taarifa ya Lissu na kukiri juu Ya hilo lakini bado taarifa hiyo ya Kawawa inakaribisha maswali zaidi:
1. Kawawa amelaumu wanasiasa kwa kuhujumu Uchumi wa Nchi Kutokana na matendo Hayo, bila shaka hapa anatueleza kwamba maamuzi ya kukiuka sheria ndio msingi wa nchi kudaiwa, sasa ni vema atuambie ni Waziri gani katika Wizara husika katika mwaka 2009 alifanya maamuzi ya kukurupuka na hivyo kuiweka nchi katika deni LA takribani bilioni 80?
2. Je kama tuhuma hizi ni kweli, Kwa nini Serikali kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Nje ambaye amekuwa katika majadiliano kunusuru Bombadier kupigwa mnada ametaka suala hili liwe Kimya?, kwamba lisifahamike kwa tax payers wa nchi? Je ule uwazi unaohubiriwa katika mikataba ndio huu? Waziri gani analindwa, na kwa Maslai ya nani?
3. Je ni nani huyo, na kwa utaratibu upi akikataa kulipa deni halali LA takribani bilioni 40 mpaka sasa deni limekuwa na tunatakiwa kulipa bilioni 80?
4. Je Tanzania hii inapozidi kuathiriwa na maamuzi binafsi ya kukurupuka na yasiyozingatia weledi nani atawajibika katika hilo?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Weka picha ya washangiliaji, mim ninavojua ukiumbuliwa lazima upanic,
 
Iko cku tutakuwa wamoja izo n changamoto President Magufuli usichoke kuvumilia izo changamoto

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Aliyefanikisha deal done, ndo kawapa updates. Serikali wenda walikuwa wana take time, wicked one hua hawezi subiri sana lazima a come out kujipiga kifua ili achukue credit.
 
LISSU NI MJINGA MKUBWA HIVI ANACHOFURAHIA NI NINI ? LENGO ZIMA NI MAENDELEO NA KUJIKWAA SI KUANGUKA , NA KAMA IKIJA NDEGE ATAJINYONGA MAANA ANASUMBULIWA NA WIVU MTUPU.PENYE NIA PANA NJIA LISSU KAMA SHETANI ASHINDWE KWA JINA LA YESU AMEN !
Sijui ni kwanini kumekuwepo na ongezeko kubwa la ujinga awamu hii!
 
Hopeless! Mbeba mabox kwenye ubora wake!!
 
Huyo mpuuzi YEHODAYA hajui kuwa mali zetu zimekamatwa na tumekubali kulipa,tena na fidia juu!!!!
Kachanganyikiwa haswaaaaa+
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…