Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Sema tu mchakato umeingiliwa na watawala wanao tumia nguvu nyingi kuliko upeo....

Kwanini Rais Magufuli akikosea kunakuwa na kigugumizi cha yeye kuambiwa ukweli?..

Historia inamuelezea wazi Kuwa alinunua Boti chakavu..

Amesababisha hasara kwenye Samaki wa wachina baada ya kukamata ki dicteta Meli yao...

Hivyo hivyo kwa hili yeye sio mgeni kulisababishia hasara taifa.....

Hakuna cha visingizio kwa hili Lazima awajibike kwa watanzania na kuwaambia amewakosea kwa kukurupuka.


Hivi yule wa kutaka kununua mvua malasya na kutulipisha 150m daily as capacity charge Richmond, yupo, naona tunasahau tumehamia kwenye samaki na nyumba za serikali
 
Tatizo kubwa ni bunge, upinzani ukipeleka hoja yoyote yenye maslahi na taifa itapingwa, na watawala wakipeleka hoja hata kama ni ya kuuza nchi itapitishwa kwa mbwembwe nyingi, mikataba mingi imepitishwa na bunge, na pale bungeni wapinzani walizisema kasoro zilizopo na kuipinga mikataba, lakini sababu wamesema wapinzani ikapitishwa kwa nguvu.
 
Asante sana Tundu Lissu..
Bila wewe hii habari muhimu ya kodi za watanzania isingetolewa..
Mungu Akulinde Mh Lissu.
Kutokuwa na KATIBA inayomwajibisha kiongozi yeyote afanyapo makosa hata akiwa amemaliza muda wake ndio inayotugarimu watanzania.Siamini kabisa kama hawakujua madhara yatakayotokea baada ya kuvunja huo mkataba na hata mingine ijayo.
ILA KWA SABABU MWISHO WA SIKU WANAJUA HAKUNA WA KUWAULIZA BASI WANAFANYA HAYO YOTE KUWAFURAHISHA WAKUBWA WAO NA KUPATA MKATE WAO WA KILA SIKU.
Sisi wanyonge tutaendela kunyongewa chini hadi siku tupate akili,ingawa hizo dalili hazionekani kama michagngo yenyewe ndio hii inayotia aibu hivi.Mungu azidi kuwaunganisha wapinzani wa serikali hii na kuwapa umoja ili angalau waendelee kufichua udhalimu unaoendelezwa na viongozi wetu wakitudanganya kila siku kuwa ndio watetezi wetu.
 
Tatizo la wana ccm wanamshambulia Lissu aliyesema ukweli tulivyoingizwa mkenge na ccm, hawaoni athari za mapesa hayo yote tunayotakiwa kulipa! Ni kichaa peke yake anaeweza kumlaumu Lissu badala ya ccm waliovunja mkataba kinyemela na kutuingiza ktk deni hili kubwa!
 
Kwani hujafatilia wanamtukana wengi ni ukanda. Ni kama FISI anaetamani mkono udondoke.

Yaani jana walimtukana sana ukiangalia walichomtukania huoni sababu. Wanafiki sana kama walishauriwa na kuulizwa na kutoa majibu kama Lissu alivyosema jana kosa la Lissu likowapi. Majitu yamejaa misifa utadhani hii nchi ni yao.
 
Yaani watu wanye upeo mdogo wa akili their last weapon ni kumfanya mtu kua scape goat kwa thier mistake yaan lawama zote za kwao watataka kumbebesha yeye
Kiukwel ccm mnatuumiza wananchi kwan hayo makosa mnayofanya ya kijinga na kuitia nchi madeni mwishowe sisi ndo tunalipa tukitaka tusitake
Kwa hivi mnavyotunyonya kwa upumbavu wenu halaf mtegemee taifa litakua salama hili
Jueni munatufanya maskini wakupitiliza na umaskin athar yake ni kubwa hata future genaration itapata hii athar ya sasa physical ,biological , psychological nadhani wanaoweza kuchanganua hapa watanielewa namanisha nini
Hata kama maguful una nia ya maendeleo ya nchi ila badilisha style basi ambayo itakua ya misingi bora na hekima sio kua nyiny weakness ambazo munazileta sisi wananchi ndo mutukamue kiasi hiki yaani ccm mungu anawaona na maisha haya magumu munaotusababishia kwa upuuzi wenu na ulafi mutajutia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi yule wa kutaka kununua mvua malasya na kutulipisha 150m daily as capacity charge Richmond, yupo, naona tunasahau tumehamia kwenye samaki na nyumba za serikali
Wote ni majizi but huyu fisi aliye ndani ya butcher ni hatari zaidi
 
Ndugu zangu tunafurahia lipi hapa!! Kuzuiliwa kwa bombadier?! Aibu kwetu! Bado tunahitaji miongo kadhaa kujitambua!! Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika!!!!
Hakuna anaye shabikia ila Hatutaki usiri pia Mengine ni kutokana na Maamuzi ya mihemko 'Any decision you make in life you are responsible for it'
 
Huwa nafikilia sana juu ya uwezo wakufikilia hasa wanachama wa ccm sijui nikutuona watanzania wengi ni vilaza?ccm wana kela Sana hapo tundulisu anahusikaje,kututalifu wa tz au?
Serikali kudaiwa nayo wanataka iwe siri, hapo ndipo wanapotukera wengi.
 
Yaani watu wanye upeo mdogo wa akili their last weapon ni kumfanya mtu kua scape goat kwa thier mistake yaan lawama zote za kwao watataka kumbebesha yeye
Kiukwel ccm mnatuumiza wananchi kwan hayo makosa mnayofanya ya kijinga na kuitia nchi madeni mwishowe sisi ndo tunalipa tukitaka tusitake
Kwa hivi mnavyotunyonya kwa upumbavu wenu halaf mtegemee taifa litakua salama hili
Jueni munatufanya maskini wakupitiliza na umaskin athar yake ni kubwa hata future genaration itapata hii athar ya sasa physical ,biological , psychological nadhani wanaoweza kuchanganua hapa watanielewa namanisha nini
Hata kama maguful una nia ya maendeleo ya nchi ila badilisha style basi ambayo itakua ya misingi bora na hekima sio kua nyiny weakness ambazo munazileta sisi wananchi ndo mutukamue kiasi hiki yaani ccm mungu anawaona na maisha haya magumu munaotusababishia kwa upuuzi wenu na ulafi mutajutia

Sent using Jamii Forums mobile app
Inasikitisha mno watu wazima na akili zao za kuzaliwa pamoja na za shule wanaposhabikia uzembe wa hali ya juu kama huu ambao mwisho wa siku wote tutawajibika tu kulipa kama tulivyozoea bila kujali uko ccm,upinzani au hauna chama.Kodi tunazotozwa kwa nguvu zote zitaishiaga tu kuwashibisha viongozi wetu na kulipa hasara walizotusababishia.Na kwa uongozi huu,huu ni mwanzo tu!
 
Kwa hiyo mchakato umeingiliwa na wanasiasa? Wakati mlipokuwa kimya kwa nini hamkuwaambia wananchi juu ya kuchelewa kwa kuja bombardier hiyo? Siku zote tukitaka kuwa na maendeleo tuweke siasa pembeni tuache propaganda nchi itafika mbali lkn tukiamua kwenye utaalamu tunaingiza siasa hiyo sio sahihi. Tulinde Mali zetu kwa manufaa ya kizazi kijacho.
 
Ili kuanza kuonyesha umuhimu wa kufanya maamuzi makini kwa ajili ya Taifa letu, hebu tuanze na hili deni la Bombardier, watanzania tukomae hizo bilioni 87 zinazodaiwa huko Canada, mzigo huo tusibebeshwe walipa kodi wa Tanzania, Bali deni hilo alilipe yeye mwenyewe aliyetusaababishia ambaye si mwingine bali baba Jesca!

Hapo ndipo akili zitamrudi na kujua kuwa suala LA kuongoza nchi siyo sawa na kuongoza familia yako ambayo unaweza kutembeza ubabe na kuwacharaza viboko wanao......

Kwenye kuongoza nchi ni lazima Rais aitii na kuilinda Katiba ya nchi ambayo aliapa kuitii na kuiheshimu kabla hajakabidhiwa madaraka, anapotokea Rais ambaye hataki kuitii na kuilinda Katiba ya nchi yetu, kama ambavyo aliwahi kutamka Baba wa Taifa letu Mwalimu Nyerere kuwa Rais wa aina hiyo HATUFAI.....

Mwalimu Nyerere aliendelea kwenda mbali zaidi kwenye hotuba hiyo kwa kueleza kuwa Rais wa aina hiyo analazimika kutuachia Urais wetu na yeye akafanye shughuli zake nyingine kama vile kufuga ng'ombe wake........
Mkuu huyu aliyesababisha hilo deni ,sasa hivi ni kama kamungu , maana hajaribiwi na anaogopwa zaidi ya Mungu

Unahitaji kuwa Lissu kumpinga Lissu
 
Back
Top Bottom