Mshahara kiasi gani unatosha kwa baba wa familia ya watoto watatu?

Mimi najua kupangilia hesabu sema mtoa Mada hameshindwa kusema anapokea mshahara kias gani na hajaweka mkoa
 
Anayelupwa laki anaishi,
Anayelipwa laki 3 anaishi
Anayelipwa milioni 1 anaishi
Anayelipwa milioni 3 anaishi pia.
Wote hao hawataishiwa matatizo kipindi chote watakapokuwa kazini.
Ukipata mke kimeo umekwisha.
Ishi sawa na kipato chako.
Biblia inasema: Mali inapoongezeka nao walaji huongezeka
 
Elfu 50. Watoto book kumi kila mmoja. Mzazi book 20
 
Kuwa na mazoea ya kuorodhesha matumizi yako ya Kila Mwezi
Kwa kuzingatia umuhimu na ulazima.
Fanya hivi kabla haujaanza kuitoa hiyo pesa.

Ukifanya hivyo utafahamu pesa yako inaishia wapi.
 
nimesoma comments zenu wakuu. Nilichoelewa ni kwamba ili niweze kujikimu vizuri kwa level ya kawaida atleast nikipata 2m take home salary ndio naweza sogeza haya maisha! Au nakosea wazee ???
 
nimesoma comments zenu wakuu. Nilichoelewa ni kwamba ili niweze kujikimu vizuri kwa level ya kawaida atleast nikipata 2m take home salary ndio naweza sogeza haya maisha! Au nakosea wazee ???
Kweli mkuu.maana bado ujasaidia nyumbani kwenu watu wanasahu ilo..
 
nimesoma comments zenu wakuu. Nilichoelewa ni kwamba ili niweze kujikimu vizuri kwa level ya kawaida atleast nikipata 2m take home salary ndio naweza sogeza haya maisha! Au nakosea wazee ???
Inategemeana na matumizi yako.
Kodi/unaishi kwako
Chakula+Mboga
Maji na umeme
Gari(mafuta na huduma nyingine)
Pombe kama ni mlevi
Mpango wa pembeni(Mchepuko)
Nauli ya kwenda kazini
Nauli za watoto kwenda shuleni
King'amuzi na simu
Ada za watoto kama wapo private
Mavazi ya familia
Fedha kwa wazazi ya matumizi
 
vijana inaonekana mnaogopa sana kuwahi kuzaa mkifikiri kwamba ukichelewa kuna afadhali ya kiuchumi . Ukichelewa madhara ni mengi sana, unakuta baba ana miaka 50 mtoto ana miaka 10, ni bora kuwahi uzoee kukimbizana na hizi budgets kabla ya uzee.
Cha muhimu kujipanga mkuu na idadi ya watoto ndo ina matter kwenye budget.
 
Kimbia familia ukakae bachela afu urud kushukuru apa
 

Umelist mahitaji yangu kama unaniona vile. Stress huwa zinanichapa sana ninapopokea mshahara leo alafu ikifika kesho jioni sina kitu
 
Kwa familia yako.. Unweza tumia 7,000 per day.. Pia punguza matumizi ya vitu visivyo vya lazima sana.. Mfano kula nyama kila mlo au maziwa au azamtv ya 23000 unaweza nunua cha 8000 wali kwa wıkı mara moja
Huku ni kujitesa
 
Kuna wenzako hawana kazi ni saidia fundi tu per day anapata elfu 10 na nyumbani ana lundo la watu kama 8 hivi wanamuangalia yeye tu siku akiteguka nyonga familia inalala njaa
Tanzania wafanyao kazi ni wachache sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…