Mshahara kiasi gani unatosha kwa baba wa familia ya watoto watatu?

Mkuu, kuwa na watoto 3 ni kuzaa hovyo?
Mkuu kuzaa bila kupiga hesabu ni kuzaa hovyo.. kama angekuwa kashapiga hesabu kabla asingekuja na malalamiko maana kila kitu angekuwa kashapanga kabla hajawaleta hao viumbe.. angalia hali ya maisha ilivyo hivi sasa na mapato yetu ya kila mwezi utagundua kuna ratio haiko sawa baba umeoa una watoto watatu na huyo mkeo kimahaseabu ni wanne sasa angalia kipato chako then gawanya kwa idadi ya watu hao wanne walio nyuma yako utagundua wewe utaishi kimaskini mpaka unaingia kaburini. mi naenda zangu
 
Maombi yanahitajikq hapo aisee, jamaa ana makasiriko na watoto wa 1998😀😀
oya kumbe unanichimba😂😂😂😂anyway kipindi hicho nikiwa naparangana na huyo dem nlikuwa kitaa sina mishe yoyote, biashara niliokuwa naifanya ni kufuga broilers(kuku wa nyama), on the run nikapata kazi ya kaujiriwa ambayo ndio nafanya mpaka sasa.

huyo dem wa 98 kapiga hela za urithi kapewa kama 100m+ aisee, haniongeleshi tena. Wanawake wengine sio kabisa
 
sawa mkuu siku zote hakuna mshahara mdogo kwani kadri unavyopata mshahara mkubwa ndo matumizi na matatizo huongezeka cha msingi tu wekeza hata kwenye shughuli nyingine tofautofauti ziwe zinakuingizia mapato.fikiri mwalimu anapokea laki 3 kwa mwezi na anafamilia ya watoto sita lakini anapambana wote wanafika chuo kikuu kwa hiyo jiongeze usitemee zaidi mshahara, hakuna mshahara mdogo coz more money more problems.
 
Nimepanga nalipa kodi 300,000 kwa mwezi, ada za watoto jumla kuu ni 8,000,000 tsh kwa mwaka
Mkuu unafanya nini!!!!! Mimi nina take home mara tatu ya kwako na kamwe siwezi lipa rent hiyo na nina watoto watatu pia.unahifadhi chochote kweli.wewe kwa mshahara huo rent haitakiwi kuzidi laki 2
 
Kwa familia yako.. Unweza tumia 7,000 per day.. Pia punguza matumizi ya vitu visivyo vya lazima sana.. Mfano kula nyama kila mlo au maziwa au azamtv ya 23000 unaweza nunua cha 8000 wali kwa wıkı mara moja
Sasa hayo maisha au adhabu kwa watoto??
 
Si ulisema kwenue uzi wako kuwa ulikuwa humpi hela wewe !!! Sasa aongee na wewe kwa jambo lipi? Kama una uzoefu wa kufuga kuku hao broila fuga, hilo ndio jibu la kuongeza kipato. Mimi nafuga hapa wananisogeza sogeza kiaina
 
Ikiwezekana aanze kuandaa CV ya kuombea kazi DP World watakapotua Dar. Lazima jamaa mishahara yao itakuwa vibunda sana
 
Kama hakuna ya kumwagilia moyo hii bajeti ni batili.
 
Kwa familia yako.. Unweza tumia 7,000 per day.. Pia punguza matumizi ya vitu visivyo vya lazima sana.. Mfano kula nyama kila mlo au maziwa au azamtv ya 23000 unaweza nunua cha 8000 wali kwa wıkı mara moja
Hapo kwenye azamtv nimejikuta nacheka kwa sauti.
 
Hapo kwenye azamtv nimejikuta nacheka kwa sauti.
ukipost changamoto unayopitia kama ivi unakuja gundua kuwa haupo mwenyewe kwa ground unateseka, watu wanateseka aiseee, imagine azamtv ya 23,000 ni anasa inaonekana.
 
Tatizo letu vijana, mshahara wa laki nane unataka uishi maisha mazuri, watoto wasome za hela.

Yaani ni ufahari kila mahali. Ndo maana mishahara inakuwa haitoshi. Jitahidi kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima.
 
Nimepanga nalipa kodi 300,000 kwa mwezi, ada za watoto jumla kuu ni 8,000,000 tsh kwa mwaka
Maisha haya kumbe mshahara wangu wa mwezi ni kodi kabisa dah sawa mkuu ngoja tupambane tu na hizi stress😂
 
nimesoma comments zenu wakuu. Nilichoelewa ni kwamba ili niweze kujikimu vizuri kwa level ya kawaida atleast nikipata 2m take home salary ndio naweza sogeza haya maisha! Au nakosea wazee ???
Sahihi kabisa
 
Nimepanga nalipa kodi 300,000 kwa mwezi, ada za watoto jumla kuu ni 8,000,000 tsh kwa mwaka
Mshahara wako kwa mwaka jumla ni milioni 12. Ukitoa ada za watoto milioni 8 zinabaki milioni 4. Kodi jumla ni milioni 3 na laki 6. Hapa mnabaki na laki 4. Mkae na mkeo mpunguze matumizi wapendwa.
Mfano mtazame shule za bei nafuu & Nyumba ya bei ndogo. Msisahau kula mlo kamili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…