Mshahara wa Dkt. Ndugulile akishaanza kazi WHO ni noma. Rais wa India akasome

Wewe hujui mambo ya mishahara naona.hapa hap Bongo kuna ma CEOs wengi sana wanalipwa hela mara mbili ya hiyo.unachofanya hapa ni kumtafutia matatizo ya machawa tuu.Yaani wale wasiojua mambo ya mishara watakuletea lundo la shida
 
Watu kupata hio 30m kwa mwezi hapa TZ haimanishi kuwa hio hela ni ndogo. Ukitaka kujua hio hela sio ndogo jiulize ni watu gani wanapata hio hela kama mshahara hapa Tz. Kama CEO wa kampuni inayoingiza mabilioni kwa mwaka analipwa 30m au zaidi ina maana hio hela sio ndogo.
Nashindwa kushangaa mtu ambae hapati hio 30m kwa mwaka mzima nae unamkuta hapa anasema hio hela ni ndogo.
 
Milioni 360 kwa mwaka ni hela ndogo mkuu? Watanzania wangapi unaowajua wanaingiza hiyo hela?
Kuna watanzania wakuu wa makampuni ya kigeni ya wawekezaji na walioko vitengo muhimu yaliyoko nchini mshahahara yao inaanzia milioni 150 kwa mwezi

Hiyo hela ya Ndugulile kwa post kama hiyo ndogo sana
 
Mbona pesa ya kawaida sana. Ila kwasababu ya umaskini inaonekana nyingi.
Ni milioni 30 kwa mwezi, pesa ambayo ukifika mgodini Bulyanhulu watu wengi wanalipwa hiyo pesa na wengine zaidi
 
Hata senior engineer tu wa Ulaya anapata hizo pesa. Hata senior doctors wa Ulaya wanapata hizo pesa.

Hizo ni Pesa za mchezaji wa mpira wa ligi kuu ya Uingereza kwa wiki moja..

Hizo ni pesa mchumi wa kawaida kabisa kwenye mabenki ya Ulaya.

Kwa kifupi hizo sio pesa za kutisha. Watanzania wengi tu kwenye Kazi kubwa za engineering na u daktari walioko huko Majuu wanapata
 
Kwenye uwaziri wa afya anapata hela nyingi kuliko hiyo kwa mwaka.

Waziri wa afya ana fursa nyingi sana za kupiga hela
Watanzania na akili ya uwizi uwizi tu. Eti nafasi ya kupiga pesa. Inakuwa waziri badała ya kufanya Kazi uache legacy Fulani hapa duniani muda wa kupiga pesa mnautoa wapi? Na hizo pesa mtaenda kufanyia nini?

Hiyo yote ni mishahara mikubwa. Kilichobaki wafanye Kazi.
 
Mbona pesa ya kawaida sana. Ila kwasababu ya umaskini inaonekana nyingi.
Ni milioni 30 kwa mwezi, pesa ambayo ukifika mgodini Bulyanhulu watu wengi wanalipwa hiyo pesa na wengine zaidi
Tatizo wa Tanzania kutotoka nje kusaka kazi wanaona nyingi hiyo pesa ya Ndugulile ukienda hapo Kenya tu

Co-operative Bank of Kenya chief executive Gideon Muriuki earned Sh455. 5 million kenya shillings last year, cementing his position as corporate Kenya's t a daily average earning of Sh1. 25 million Kenya shillings

Huyo mshahara wake ukipiga hesabu kwa pesa ya Tanzania huyo mkuu wa benki ya ushirika ya Kenya kwa mwezi analipwa shilingi milioni 750 kwa mwezi hiyo hela Ndugulile kwake ndogo mno
 
Ni ajabu Kuna mtu nimeona hapo juu amekomenti eti mshahara wa milioni 360 atakaolipwa Ndugulile Kwa Mwaka ni mdogo wakati huo huo yeye akichanganya kipato chake chote Kwa Mwaka hakifiki hata milioni 12 yaani haingizi zaidi ya milioni 1 Kwa Mwezi 🙌

Yaani tumezoea roho mbaya tu 🙌
 
Ccm imewafanya Watanzania wengi wajinga sana. Hawayajui kabisa ya duniani
 
Naingiza mill 51,120,000/=
 
Masikini anayepata elfu moja kwa wiki aweza ona yeye tajiri kuliko maskini anayepata mia tano kwa wiki akampuuza mpata mia tano kuwa lofa kumbe wote maskini na malofa hakuna tajiri hapo wanapishana tu kiwango cha umaskini ndio maana wazungu wakiangalia Tanzania wanaiita nchi maskini na akina Ndugulile wanahesabiwa humo.humo
 
Mbona hizo ndogo sana, kuna wengine wanalipwa 1.7 Million GBP kwa cheo kama chake kwa mwaka na wako kimya tu humu...Hongera kwake lakini kwa kuwakilisha nchi na wananchi vyema.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…