Mshangao; KFC ni kwa ajili ya masikini nchi zilizoendelea ila Africa ni kwa ajili ya matajiri!

Mshangao; KFC ni kwa ajili ya masikini nchi zilizoendelea ila Africa ni kwa ajili ya matajiri!

KFC kkoo nje kuna watu wanauza matunda na mwengine anauza kahawa hizi za 100, ndani kinafasi kidogo watu wanapanga foleni, ukipata chakula uondoke ama ukakae kwenye meza, shukuru Mungu ukipata kiti otherwise vile viti.kama vigoda na kimeza chembamba kinakuhusu.

Mtoa mada hii ndio KFC kama hujawahi fika
View attachment 3559405
Kuna maelfu ya Hotel Tanzania hii nzuri kuliko KFC.
Na ukutani namuona Mzee mwenyewe picha kila Kona za miaka 1896😁
 
hata woolworths huko nchi za watu nasikia ni mchikichini iliyochangamka ila huku kwetu ndo kwa watoto wa mboga saba.
 
Hayo ma junk food kwa weneztu bei ni za kawaida
Ila kwenda kula kwenye restaurant ndiyo ghali na watu wenye uwezo wanaenda

Ova
 
Remy kapiga kwenye mshono😀
Tajiri gani mwehu anakula KFC? Huko ni kwa vijana malimbukeni tu. Yaani tajiri aache kula kuku original Golden Tulip akale broiler KFC? Serious kabisa?
 
Bei ya KFC Bongo maskini wataweza? BTW hata Africa wateja wengi wa KFC ni middle class ambao hata nchi zilizoendelea ni walaji wazuri wa KFC McDonalds etc
Watanzania maisha yao ni hayo kila kukicha zikijaa shoprite za kutosha utawasikia ni maduka ya masikini yasipokuwepo ni ya matajiri..
 
Tajiri gani mwehu anakula KFC? Huko ni kwa vijana malimbukeni tu. Yaani tajiri aache kula kuku original Golden Tulip akale broiler KFC? Serious kabisa?
Wageni wanakula kuku wa kufugwa mkuu hawa kuku wa kienyeji tunakula sisi hata hapo Zambia tu kuku wa kienyeji unaweza kupewa kwa bei chee ila sio hao kuku wao...
Kuku wa Kienyeji wanaitwa village chicken Wazambia kavu sana..
 
Uliambiwa hao wanaokula KFC wanakula Kila Siku?
Maskini wakiweka pesa kwa wiki wakasema waende hapo KFC wakala chakula cha ,40k utasema sio maskini kisa wamekula chakula cha 40k?
Acha uongo maskini wa Tanzania hawana mda hata na KFC
Mtu anaingiza elfu tano au kumi kwa siku umuuzie kuku elfu 20 ilihali anaweza nunua kwa elfu 1500

Uliza randomly maeneo ya uswahilini kama hata wanahabari na kfc

Watu wanashindia miguu ya kuku, vichwa na dagaa Michele aende akatoe elfu 20 au 30 unajua ni siku ngapi anatumia kuipata

Wanaokula KFC kwa Tanzania ni middle class na sio maskini
 
Miaka ya ujanani tulikuwa tunakula baga

NANDOS

Mademu wakali pale;
 
Futari ya leo

1773862175183.png
 
Wadau wahoji na kushanga jinsi migahawa ya KFC imekuwa ni kwa ajili ya wenye kipato au matajiri nchi nyingi za Africa wakati nchi zilizoendea huko duniani kuanzia Marekani, Canada, Ulaya, Japan n.k KFC ni kwa ajili ya masikini au watu wenye kipato cha chini!

Wadada wa mjini wanavyopenda kuku wa KFC sijui kama wataelewa hili suala.
View attachment 3559358
Chai
 
Kuna watu wanakula hizi junk foods daily kuanzia asubuhi Hadi jioni, ni hatari Sana...
 
Acha uongo maskini wa Tanzania hawana mda hata na KFC
Mtu anaingiza elfu tano au kumi kwa siku umuuzie kuku elfu 20 ilihali anaweza nunua kwa elfu 1500

Uliza randomly maeneo ya uswahilini kama hata wanahabari na kfc

Watu wanashindia miguu ya kuku, vichwa na dagaa Michele aende akatoe elfu 20 au 30 unajua ni siku ngapi anatumia kuipata

Wanaokula KFC kwa Tanzania ni middle class na sio maskini

Elfu tano ni Fukara.
Maskini kipato chake ni Kati ya 200k - 1M.

Middle class ni 2M - 20M monthly

Wewe kama kipato chako kipo below 1M bado upo kundi la Maskini. Ingawaje kuna Maskini aliyechangamka
 
Elfu tano ni Fukara.
Maskini kipato chake ni Kati ya 200k - 1M.

Middle class ni 2M - 20M monthly

Wewe kama kipato chako kipo below 1M bado upo kundi la Maskini. Ingawaje kuna Maskini aliyechangamka
Yaani unamuweka mtu wa 2m na 20m kundi moja? Hebu kuwa serious basi.
Vipi wa 1m-2m hana class?
 
Back
Top Bottom