Mshtuko mkuu ndani ya CCM. Ushindi wa Lissu na Heche ni chanzo. Je, Mungu anaifuta CCM?

Sawa, afanye juhudi za kuwaunganisha hao wa asilimia 48% kabla ya CCM. Vinginevyo kama alivyotengeneza upinzani nao wanaweza fanya hivyo.
Asilimia 48 unayoisema, ni matokeo ya rushwa na siyo mahaba kwa Mbowe.

Wajumbe wengi wanataka mabadiliko. Njaa na vitisho vimekuwa vingi kwao


Tanzania ya ndoto zako haipo mbali nawe. Shiriki
 
Naona sasa ile hoja ya kwamba CHADEMA ni chama cha wachaga imekufa Rasmi kwa sababu katika kamati kuu mchaga aliyebaki ni Lema pekee
 
Mungu aendelee kutujalia uhai, mwaka huu lazima nisafiri zaidi ya km 2,000 kuhakikisha napiga kura Kwa mara ya pili katika maisha yangu. Naamini kura yangu haitapotea Tena.
 
Naona sasa ile hoja ya kwamba CHADEMA ni chama cha wachaga imekufa Rasmi kwa sababu katika kamati kuu mchaga aliyebaki ni Lema pekee
Uchaguzi huu umeua propaganda zote za CCM dhidi ya CHADEMA.

Propaganda kuwa chama ni cha wachaga imekufa rasmi

Propaganda kuwa chama ni cha familia imekufa

Propaganda kuwa chama kinaendeshwa kifalme na mwenyekiti wa Kudumu imekufa

Propaganda kuwa chama ni cha kidini imekufa.

Kama CHADEMA watasoma hii comment wajue kuwa sasa wajiandae kuingia Ikulu.
 
Walikua na hoja moja tu chadema chama cha Wachagga kwisha habari yao
Japo mimi si mchagga lakini wachangiaji wadogo kwa wakubwa walikichangia bila kuchoka wana nidhamu ya pesa, na kutokata tamaa sio bendera kufuata upepo.
Endelea kuwakebehi ndio mtajua umuhimu wao.No money no honey.Asubuhi usishangae TLP ikawa afadhali kuliko People's. Mkono mtupu haulambwi.
 
Duru za ndani ya CCM zinanyetisha kuwa hali ya mtafaruku na mfadhaiko mkubwa imeikumba CCM kutokana na pigo takatifu la ushindi wa Tundu Lisu na John Heche katika uchaguzi wa CHADEMA taifa.
 
51% vs 49% Maana yake Chadema imepasuka Msambani yaani katikati 🐼

Hawa walipiga kura, 49% wameshindwa kwenye box la kura in fair election, hawa 49% ni rahisi kuunga mkono na kuungana na wenzao 51% maana Demokrasia ilifanya kazi.

Sasa shida iko kule Dodoma, ambako watu wamekaa chumbani wakaamua na kuwalazimisha watu kusema ndiooo huku wakiburudishwa na akina Zuchu, Diamond, Ally kiba nk.
Inaonekana wafuasi wa CCM kwao wao ni muhimu sana kuwaona akina Doto Magari, Baba Revo, Mwijaku, Juma lokole, Irene uwoya nk kuliko kumchagua Mwenyekiti wa Chama na mgombea wao wa Urais.
 
Akili mgando hizi. Hiyo dhana ilitengenezwa mahsusi ili kukidhi matakwa yake tu,haiwezekani chama chenye wanachama zaidi ya milioni 5 kishindwe kujiendesha,ni mipango tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…