Msiba wa Lowassa ni gunia la misumari kwa Kikwete

Tuachane na ubishi turudi kwenye uhalisia na turudi 2005 ,ushawishi ule wa JK ulitengenezwa na Lowassa ? Najua hii ni stori ya kijiweni ambayo mpaka kesho inasemwa hivyo
Hahahauahaaaa!
Yaani ikifika hapo mi ndo nawapuuuza kabisa hawa haters wa jk, kiukweli kuna ratizo mahali katika bongo za watz......?.'elimu, elimu, elimu' kama alivyowahi kusema mwendazake!
 
Dah, mwamba una maswali magumu sana!
 
Zirudie akili zako na hapa nitakuelekeza kwa mifano maana Biblia inatufundisha kutumia mifano.

Kwa mfano, umegombana na mtu aliyekuwa rafiki yako sana na ukawaambia watoto wako kwamba Fulani nimegombana naye msimuamini sana. Miaka ikasonga, mkaombana msamaha na uliyogombana naye mkayamaliza. Je, watoto watamsamehe huyo mtu kama ulivyomsamehe wewe?
 
Ukaskazini nao umempaisha Lowasa
 
Hahahauahaaaa!
Yaani ikifika hapo mi ndo nawapuuuza kabisa hawa haters wa jk, kiukweli kuna ratizo mahali katika bongo za watz......?.'elimu, elimu, elimu' kama alivyowahi kusema mwendazake!
Watoto wengi wa 2000 wanakua wanakutana na stori ya Lowassa kumuweka Kikwete madarakani halafu Sasa walivyo wepesi wa kubeba Kila stori wanaamini ni kweli.
 
Una ushahidi au ni stori za vijiwe vya kahawa
 
Kwa hiyo mlotaka ampe urais kisa ni rafiki yake? Thank u kikwete uliangalia maslahi mapana ya nchi kuliko kujali uswahiba nchi itumbukie shimoni japo jpm ndo alikuwa rais mbovu sana kuwahi kutokea Dunia hii
Hakumpa nafasi ya kujieleza mbele ya wajimbe ambao ni wapiga kura kimsingi hakutendewa haki angewaacha wajumbe waamue
 
Kwa logic yako - Kama walikuwa marafiki na huu ni Msiba wa rafiki yake Ulitegemea awe na hali gani ?!!!
Furaha ?!!!!

Mimi kama mlipa Kodi ningekuelewa zaidi ungesema hawa jamaa wawili hawakututendea haki katika Sakata la Richmond - Hayo mengine nadhani yatakuwa hayatuhusu unless na wewe ni mwanafamilia....
 
Wenye akili ndogo wanadhani uadui wa lowasa na kikwete ni personal,yaani wao binafsi walikosana wakawa maadui!!

Sivyo kabisa,urafiki wao ungedumu Hadi Leo ungeleta madhara kwa dola,ilikua lazima wakosanishwe Kwa vyovyote vile Kwa mstakabali was taifa la kesho!!

Urais was kupeana kama marafiki ni hatari sana Kwa taifa,ndio maana wanamtandao walipaswa kusambaratishwa Ili 2015 wasiingize mtu wao ikulu,na hilo Dola walifanikiwa sana kuwasambaratisha!

Mengine ni makosa ya kibinaadamu pale uadui unapozidi viwango!!

Nadhani!!
 
We ulitajwa?
 
“Mheshimiwa Lowassa ni muhanga wa mifumo yetu ya uchaguzi. Alikuwa mgombea wa urais wa kwanza katika upinzani kupata kura zaidi ya milioni sita. Halikuwa jambo dogo…… The full potential ya uongozi wa mheshimiwa Lowassa haikuwahi kutumika, tuwape watu nafasi katika misingi ya kweli na haki, watumike” - Freeman Mbowe, Monduli, 17.02.24
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…