Msiba wa Lowassa ni gunia la misumari kwa Kikwete

Huna ujualo, Huyo Kikwete hata hiyo miaka 1995 hakuwa na mawazo kugombea Urais. Ni ushawishi wa EL na RA

Sent from my SM-A107M using JamiiForums mobile app
 
Kumbe!
 
Sio kweli! Alimtenda sana Lowasa!
 
Hiyo tezi dume si alitibiwa?
 
Heshima aliyopata ni kwasababu ya Kikwete. Lowassa alikuwa mwizi asiyeshiba ulitaka aachwe? Yeye si wa kwanza kujiuzulu hata Warioba alipigwa chini. Rais ndiye mkuu wa nchi
Maneno ya DrMwakyembe kuwa kuna taarifa zilifichwa na endapo wangeziweka wazi wangeangusha serikali ndio yanafanya Lowassa aonekane alitolewa sadaka ili JK na serikali yake apone
 
Lakini sababu hasa ya Jakaya Mrisho Kikwete kulaumiwa kwa ajili ya Edward Ngoyai Lowassa ni zipi?

Je, zaweza kuwa ni hizi mbili?

1. Inasemekana tangu mwaka 1995 walifanya alliance ya mmojawao either by hooks or by crooks ni lazima aje kuwa Rais na mwingine PM.


Mwaka 1995 waliingia kwenye mchujo. Hawakupenya kwa sbb mwasisi wa taifa hili Hayati Mwl. Julius K. Nyerere aliwapiga "veto". Nyota ikamzukia Hayati Benjamin William Mkapa

Hawakufa moyo. Waliendelea mbele na mipango yao hadi 2005. Mchuano ulikuwa mkali sana kati yao. Mazungumzo yakafanyika nje ya kapu la mchujo. Mkataba ukaingiwa kati yao kuwa EL amwachie JK na yeye zamu yake ingekuwa 2015 na sharti lingine ktk mapatano hayo likawa, angeshinda (JK), basi mzee EL angekuwa PM wake. Ndivyo ilivyokuwa.

2. Mambo yaliharibika mara baada ya safari yao ya matumaini ilipoanza Novemba, 2005.

Katikati hapo (mwaka 2008) ikazuka kashfa ya kampuni ya ufuaji umeme ya Richmond PLC.

Zigo la kashfa hiyo likamwangukia EL pekee. Rais na rafiki yake JK akashindwa kumlinda wala kumtetea.

Wapambe wakavuruga kila kitu. Na kwa sbb hiyo PM - Edward Lowassa akajiuzuru u - PM mwaka huo 2008.

Njiani pale wakapozana kwa namna walivyojua. Lakini wapambe wa katikati wasiotaka EL aje kuwa Rais, wakajaribu kila njia kumchafua na hata kumuua kwa sumu.

Hilo lilimsumbua sana EL kiasi cha kujiuliza nini kimempata rafiki yake (Rais JK) ambaye ana resources zote za kuhakikisha anamlinda lakini akashindwa kufanya hivyo hata kuacha mifumo ndani ya serikali na chama chao CCM kumsakama na ku - tarnish image yake kiasi kile.

Mzee akasubiri hadi 2015. JK alijaribu kutunza ahadi yake kumwachia rafikiye. Vurugu zilizotokea Dodoma mwezi Juni, 2015 wakati wa mkutano mkuu? Halmashauri kuu ya CCM? kuteua mgombea kila mtu anakumbuka na kuelewa vyema. Jakaya Mrisho Kikwete akamtosa rafikiye mchana kweupe!!.

EL kwa hasira akaondoka CCM na kujiunga na CHADEMA. Huko akapata nafasi ya kutimiza ndoto yake. Akagombea Urais kwa udhamini wa CHADEMA kushindana na mgombea wa CCM John P. Magufuli.

Ushindani ktk uchaguzi huo ulikuwa mkali sana. Kura zikapigwa na kuhesabiwa. Eti John P. Magufuli wa CCM akatangazwa mshindi. Lakini wachunguzi wa mambo wanasema wazi kuwa Lowassa ndiye aliyeshinda kwenye ballot box lakini ktk kutangazwa, akatatangazwa John P. Magufuli!!

Hilo likathibitisha pasipo shaka kuwa rafikie alikuwa na dhamira ya kumtosa tangu mwanzo. Angekuwa ni mtu wa kusimama ktk mapatano yao na kama huko CCM mlango ulijifunga pasipo kutarajua, basi JK alikuwa na uwezo wa kumpa rafikie u - Rais wake hata kupitia CHADEMA. Hakufanya hivyo!!

Hiki ndicho kinachomuumiza Jakaya Mrisho Kikwete. Dhamira yake inamsuta. Anaona aibu. Na yule mtu waliyempa u - Rais kupitia CCM (John P. Magufuli) alitumia nafasi na mamlaka yake sawasawa kuwanyoosha akiwemo yeye mwenyewe Kikwete.

Yaani Jini walilolifuga na kulilisha wenyewe (John P. Magufuli), likawageuka na kuanza kunyonya damu zao. Mwisho wa siku wakaona kuwa, ipo siku linaweza kuja kuwaua. Wakaamua kutumia umafia kuliondoa!!
 
Unalazimisha tuwaze unavyotaka wewe?
 
Wewe umejadili lupi kubwa hapa.
 
Mwacheni JK,Lowassa kamati kuu ilishamkataa kipindi cha mwalimu,yaliyomkuta ni ajali ya kisiasa na ni political vibes tu hizo,kwani Lowassa aliandikiwa lazima awe Rais wa nchi hii?watu wanataka kutengeneza story tu,amemaliza Muda wake ,apumzike kwa amani,tutaendelea kumshukuru JK kwa kutuletea Chuma Magufuli
 
Hata kama ni wewe rafiki yangu uje unisukumie kashfa nipate ajali ya kisiasa nianguke kukulinda wewe, nijikongoje niinuke, uje tena unifyekelee mbali nisiyafikie maono yangu, huo moyo wa kukuvumilia undava wako mimi rafiki yako mkubwa nitautoa wapi?
 
Hata muandike nini, itakuwa na itabaki kuwa kwamba JK alimsaliti rafikiye Lowasa , hakuna wa kubadilisha hilo duniani, mbinguni wala baharini.

Hata uje na majini kama yake ya Yanga ukweli utabaki hivyo. Usaliti!
 
Tushike lipi si wanasema bila Mkapa jpm asingekua Raisi sasa jk analaumiwa kwa lipi
Baada ya kuzidiwa na upepo na nguvu ya Lowassa wakati anampambania BM ndipo akaomba msaada wa mzee wa Lupaso,hapo ndipo mzee akatumia fursa hiyo kuingiza kijana wake.Alikubali ni bora kachero aukose ukuu lakini EL asiingie jumba jeupe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…