- Sielewi kwa nini wanawake wanaongelewa sana, kulingana uwiano wa Ke na Me kwenye matokeo ya sensa, kama wanawake hawaolewi inamaanisha kuna wanaume hawajaoa. Thamani ya ndoa ipo kwa wote ME na KE. Mwanaume pia kama hana mke huonekana hana thamani bila kujali elimu, pesa wala umri.
Nadhani kuna mambo ambayo jamii ya sasa ni vema ikayaelewa. Hapa kuna asili ya maisha ya mwanadamu na kuna aina ya maisha tunayoishi sasa. Ni vema kuwe na balance.
Kwa nilichokiona, mwanamke anayesoma hadi kufika elimu ya juu, hajakatazwa kuolewa na wala si kwamba haiwezekani yeye kuolewa na akasoma vizuri tu na kumaliza elimu ya juu na siky ya graduation mumewe, watoto na familia wakaja kusheherekea nae. Haya yapo na tumewaona wanawake wa hivi.
Shida inaanza na mitazamo. Mabinti wanapokuwa shule wanakatazwa na wazazi kuwa na mahusiano ila je ni kweli huwa hawana mahusiano? Tena wanakuwa na mahusiano na wanaume hata sita. Wote hawa wanamla mwanamke mmoja.
Sasa wazazi hili wanaliona wanapiga kimya ila waanapiga kelele na kumtisha binti yao asiolewe huku akiendelea na mambo yake ya elimu, shida ipo wapi.
Kwann mnataka kuona ni sawa mtoto wa mtu wa kiume aoe binti ambaye huko chuo ameishi na kijana kinyumba kama mume na mke na wameachana baada ya kumaliza chuo. Hii imekaaje?
So nadhani muhimu sana kama jamii tulitazame hili upya kuwalinda mabinti zetu. Wakiwa ndani ya ndoa wanalinda heshima yao, kwakuwa na mume wake ambaye wataweza kuwa nae maisha yote lakini pia wataweza kutuliza vichwa wakiwa darasani wakijua kuwa wapo kwenye ndoa na wanatakiwa kuziheshimu.
Pia mfumo wa elimu upunguze miaka hii ya kusoma ni mingi sana. Miaka 7 primary, 6 sekondari,chuo maiam 3 kuendelea hii kwa mabinti inawaharibia sana.
Na tuongee ule ukweli. Wanapomaliza chuo ni wangapi wana ajiriwa na wakipata ajira mishahara huwa inatosha kuendesha maisha yao ya kila siku, maisha yenyewe wanafanya na nani sasa ?!
Wanaume hawana interest na mwanamke aliyekwenda shule sana sababu wengi huwa hawana uwezo wa kujishusha kuwa mke wa mtu kwa maana ya kusikilizana na mwanaume wake. Sio wote, wapo mabinti ni wastaarabu, wamesoma adabu ipo mbele hadi raha.
Tuna mengi ya kurekebisha katika jamii yetu especially katika eneo hili. Mabinti ndio ambao wapo katika wakati mgumu. Kijana atasoma, ata hangaika na ajira akikosa ataenda fanya biashara akija toboa hata ana miaka 35 kwenda juu ana uhakika wa kupata binti chini ya miaka 25 na wakayajenga maisha na utulivu ukawepo.
Hawa mabinti mnaowapotosha hadi wanakuja stukia wapo na miaka 30 wanatanga tanga tu, maisha hakuna, ajira hakuna , pesa ngumu, maisha gharama zipo juu, miili inazeeka na wengine masikini wameshazalishwa watoto wawili hivi wanaishia na nani?!
Nani atawasitiri hawa. Na mshawajaza akili za kimasikini kuwa akiwa na elimu kubwa maisha yake yatabadilika,atakuwa na kazi ya mshahara mzuri,ataishi kama wazungu, ataolewa na meneja wa benki akishamaliza shule. Atamudu maisha kwa urahisi. Je, hii ni kweli?!
Hivi maisha mnayachukuliaje kwa mfano?!