Msigwa: Rais Samia hakukodi ndege ya Emirates wakati wa safari yake ya kwenda na kurudi Ufaransa na Ubelgiji

Msigwa: Rais Samia hakukodi ndege ya Emirates wakati wa safari yake ya kwenda na kurudi Ufaransa na Ubelgiji

Raha ya Tanzania kila mtu ni CAG na niwabobezi ktk ukaguzi wa mahesabu mixer (VFM)[emoji1787][emoji23]
Na raha zaidi ni pale CAG anapotoa taarifa rasmi ya mahesabu ya sehemu fulani, wengine wa huko kulikokaguliwa huikataa taarifa hiyo na kuiita ya uwongo..
 
Sahihi kabisa, Msigwa anaupiga mwingi kwenye propaganda za kitoto.
Bila bila

Kwenye ^sirikali^ ya Bi Mikopo, usipoupiga mwingi, kipengele lazima kipulizwe na utolewe nje ya uwanja hata kama hukuugusa mpira wala kufanya kosa lolote!

Kigezo ni KUUPIGA MWINGI!
 
Sio kweli kwamba ameokoa fedha, wanaomshauri Mh rais wapo na interest zao hasa kwa masuala ya per diem.

wameweza kumwingiza chaka kwa sababu Rais anatakiwa asafiri kwa ndege yake lkn kwa sababu inabeba abiria wachache wameamua kumdanganya kwa kuwa aghalabu ndege yake yenye kubeba abiria 18 kuna wengi wangeachwa kwenye msafara na ndio maana wanamdanganya wana save pesa lkn kwa idadi wa delagation ya watu 70 anaosafr nao ni dhahiri upo upotevu mkubwa wa fedha zinazolipwa kama per diem and accomodation.

Lakini kiusalama kwa kweli bado kusafiri na ndege binafsi si afya sana kwa mkuu wa nchi!!

Mama ajitazame!
Ndege binafsi au ulikusudia kusema Ngege yenye abiria wengine?
 
Hata kama 10 Billion ni ndani ya budget yake au?
Kwahio wewe msamiati wa kubana matumizi hukuwahi kuusikia ?

Pili kwa mwendo huu wa kukopa na matozo huenda its time to revisit hizo budget (Au haiwezekani watu kujiwekewa Budget ya kumaliza mpaka ukoko)
 
“Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan hakukodi ndege ya Emirates wakati wa safari yake ya kwenda na kurudi Ufaransa na Ubelgiji.

Mhe. Rais alisafiri kwa kutumia ndege hizo kama abiria.

Ameokoa fedha nyingi ikilinganishwa na kama angetumia ndege binafsi ama angechukua ndege ya ATCL ama angekodi.

Pia soma:

- Rais Samia kufanya ziara ya kikazi Ufaransa na Ubelgiji

View attachment 2127338
Kiitifaki Rais huwa ana msafara mkubwa wa watu pale anaposafiri. Yeye hawezi kusafiri kama abiria mwingine na kuwa na uamuzi wa kukaa katika "economy class". Yeye lazima atakaa katika "business class" na msafara wake.

Kwa hiyo basi usafiri wake na msafara wake bado hugharimu fedha nyingi, ijapokuwa gharama yake haitakuwa sawa na kutumia usafiri wa ndege binafsi. Hivi ndege ya Rais aliyoipigia debe Waziri Mramba kwa inunuliwe hata ikewezekana kwa kupitia gharama ya Watanzania kula nyasi bado ipo?
 
Kwanini akipanda ndege huwa hakuna ulinzi wa msafara wake kama ilivyo barabarani au angani hakuna maadui adui zake ni sisi walalahoi ambao hatuwezi kupanda ndege?
Nimecheka mpaka nikajamba
 
Sio kweli kwamba ameokoa fedha, wanaomshauri Mh rais wapo na interest zao hasa kwa masuala ya per diem.

wameweza kumwingiza chaka kwa sababu Rais anatakiwa asafiri kwa ndege yake lkn kwa sababu inabeba abiria wachache wameamua kumdanganya kwa kuwa aghalabu ndege yake yenye kubeba abiria 18 kuna wengi wangeachwa kwenye msafara na ndio maana wanamdanganya wana save pesa lkn kwa idadi wa delagation ya watu 70 anaosafr nao ni dhahiri upo upotevu mkubwa wa fedha zinazolipwa kama per diem and accomodation.

Lakini kiusalama kwa kweli bado kusafiri na ndege binafsi si afya sana kwa mkuu wa nchi!!

Mama ajitazame!
Hao sabini ume kokotoa wapi? Tanzania kila mtu anajua kila kitu
 
Back
Top Bottom