Wakuu habari,
Kwa mwenye uelewa tusaidiane. Watoto wa shule za primary wamekua wakipewa dawa za meno na mswaki kwa lengo la kuhamasisha usafi wa kinywa. Licha ya nia kua nzuri lakini pamekua na sintofahamu ikidaiwa dawa za meno zinazotolewa zina madhara kwenye upande wa hormones. Wadau mnaopita huko mashuleni hawa watoto wetu wanapewa hizi dawa na miswaki.
Je, kuna usalama wa kiafya?
Kwanini kampeni haikujikita kuhamaisha bila kugawa dawa za kuswakia? Je kama kuna madhara, si hizo bidhaa zilithibitishwa na tbs? Watoto wetu wasije kukosa uwezo kufanya mambo.
Wizara ya elimu na wadau husika chunguzeni, tusije kuharibu watoto wetu.
View attachment 2571870