Ndiyo, ni juzi tu tarehe 2/7 nikapewa artequine. Leo namalizia dozi. DALILI: Mwili kuchoka, miguu (kwenye nyayo) na kifua kuwaka moto.
Hakuna kichwa kuuma, wala baridi wala joto kupanda. Magonjwa mengine kama typhoid huwa natibiwa kama kawaida na kupona hata miaka. UTI, naitibu kwa kunywa maji mengi
Kutokana na miguu na kifua kuwaka moto, nimewahi kufanyiwa kipimo cha endoscopy Bugando nikakutwa na GERD (kuna sehemu umeeleza kama aina mojawapo ya vidonda vya tumbo), nikatibiwa na kwa kiasi kikubwa nimpata nafuu. Miguu na kifua inawaka moto pale tu ninapokuwa na malaria
Karibu