Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

BJ naona una uwezo wa kufuatilia kweli kama jamaaa kishawekeza, hapo hajavuna akivuna ana usalama kweli-ahaaaaaaaaaaaaaaaha

ni kweli nafuatilia ili nipate mwangaza wa hiyo investment, usalama utakuwepo mkuu ha ha ha....Hii ni topic iliyonivutia sana!!!
 
tafuta eneo ambalo ni strategic kibiashara kisha nunua hapo na ujenge choo cha kulipia. pia hakikisha kina ubora na maintenance ni MUHIMU sana kuhakikisha huduma bora
 
got something here sana si mchezo hii kitu!!
me nipo zaidi ktk nyumba za kupanga hasa kwa wanachuo na lecturers nk
 
pia nchi hii kwa sherehe hatujambo na hazitaisha,semina/mikutano nk
sasa basi ukifanikiwa kujenga ukumbi eneo murua ambalo pia unakuwa na kabustani flani ivi (sio lazima centre maana bei ya eneo ni kifo). kazi inakuwa kukodisha tu na ukiweza zaidi basi unakua na vifaa vyako vichache ambavyo unakua wakodisha apo ukumbini mf tents viti,meza
 
Kama umechukua mtaji kabla ya kujua utaufanyia nini ie a deadly mistake unaweza ishia fuja izo pesa.
Next time usithubutu kukopa ua kuchukua mtaji sehemu unless uko na feasible business idea that needs to be implemented.
Ushauri wangu ziludishe ulikozitoa then ujipange upya
 
Kuna PDF ya Thread Nzima ikiwa imefanyiwa editing....kuondoa comment zingine na zingine zimewekwa...zilie ambazo zilikuwa zinatoka ushauri wa biashara iliyotajwa zimewekwa...inapatikana....sijui jinsi ya kuiattach hapa...ili mtu awe nayo bila kuingia online kila wakati..na kusoma....na kwa wale ambao hawana access mara kwa mara..nimeiandaa...anaye hitaji please let me knw.
 

Uzuri wa JF ni kuwa na watu Vichwa kama Buswelu............Heshima mbele Mkuu.........kazi nzuri
 
Tunakushukuru Mkuu Buswele,
Haswa kwa muda wako na kwa uzalendo-watu kama nyinyi ndio mnapashwa kuzidishiwa mara 10 ya mlichonacho,sio wale -ve characters au kina RC( roho cashewnut)
 
Ina bidi kuwaza mbali pia.Kwani kila kukicha Nchi za Afrika zina kopi maendeleo ya Ulaya na America.
Ulaya hakuna umeme wa kupita kwenye Manguzo.Nadhani muda sio mrefu hii idea itakuja east
Africa.Umeme wa kupita kwenye Manguzo ni hatari sana.kwahiyo itakuwa ni mwisho wa biashara ya miti ya nguzo.
Hata miti ya mbao za ujenzi ipo pindi haita uzwa kwani mambo ya Global warming ndio yamecharuka kila kona
ya Dunia.Itabidi tusitumie miti tena kwenye ujenzi wa Makazi yetu,tuige technolojia ya Ulaya.
Hii biashara ya miti ni Non-ethical/immoral.Tupande miti kwa kupreserve mazingira,tulete mvua.
 
Mkuu maelezo yako tosha nimerizika mimi nipo tayari kuwa mfugaji naeneo lakutosha je ng' mbe wanapatkana wap na huwa wanuzwa wakiwa na mimba ya miezi sita kuna tofauti zipi za kuwatambua ikiwa si wa maziwa
Ubarikiwe sana

 
Boss nimekuwa na mawazo ya kuwa mfugaji bada ya kusoma ushuri ulompa ndgu yetu ufafanuziwake upowazi na umeeleweka vizuri sana ispokua na maswali upatikanaji wapi ntawapata ng'mbe wa mifugo na huuzwa wakiwa na mimba ya miezi sita ndivyo ilivyo kawaida na je unamtalam wa mifugo anaekupa ushaur
Asante ubarikiwe
 
ng`ombe kweli wanalipa ( maziwa sio nyama),lakini jamaa yuko nje ya nchi. Mziki wa kutunza ng`ombe ukiwa mbali,tena ng`ombe wa maziwa si mchezo. Angekuwa bongo ningemsaidia kumwonyesha kiwanja safi cha kufugia ng`ombe hao.

nioneshe mimi, nifanyeje?
 

Cheki na taaluma yako kwanza. Kwa mfano usithubutu kufungua biashara ya kuuza genge wakati umesoma I.T. Utafulia au utasingizia kuna mkono wa mtu.
 
nioneshe mimi, nifanyeje?

Unataka kufuga ng`ombe wangapi kwa kuanzia? Bonde la mto mpiji ni zuri sana kwa sababu lina nyasi mwaka mzima na karibu sana na sokoni.
Upande wa kiluvya karibu na kwa PM mstaafu kuna maeneo mazuri sana ya kufugia ng`ombe,ila bei ziko juu.
 
Cheki na taaluma yako kwanza. Kwa mfano usithubutu kufungua biashara ya kuuza genge wakati umesoma I.T. Utafulia au utasingizia kuna mkono wa mtu.


Hapo mkuu unampa ushauri ndivyo sivyo...mfano uliotumia wa mtu mwenye cheti cha IT ni mbovu. Cheti ni cheti tu iwapo moyo wake upo kwenye kuuza genge. Kama aliweza kusoma IT na akafaulu vizuri basi biashara ya kuuza genge haitamsumbua ikiwa tu atajituma kujifunza kutoka kwenye vyanzo makini, kuweka bidii na kujipanga inavyotakiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…