Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Malila vipi bonde la Kilombero............naona Serikali wamekuwa wakali kweli kweli..........mwendo ni mdundo.......i.e. Kilimo kwa kwenda mbele............

Nikwenda Kiroka Moro, ni kuzuri ajabu, tatizo vishamba ni vidogo kama taulo. Kilombero poa, ukienda Mbingu utashangaa kwa nini watu tunaminyana Manzese badala ya kulima huko. Tatizo linalolikabili bonde hilo kwa sasa ni wafugaji wa ng`ombe, hata Kilosa/Mvomero - Mabana kuna ugomvi na wafugaji. Ukiweza piga kwata hadi Chita, kuna mvua huko hadi raha.

Nimesikia juzi nikiwa Kiroka eti wana-plan kuwahamisha wafugaji Kilombero, yaani nchi hii vurugu tupu.
 
Yani hii thread ni RESPECT, nimekusanya mambo mengi tangia mjadala wake umeanza. Thanks kwa wote esp. Malila! Panapo majaliwa nitawapa feedback karibuni kuhusu mtaji wangu nimewekeza kwenye nini. Nipo kwenye mipango ya awali kabisa.
Mbu hatujakusikia kabisa..???
 
Reactions: Mbu

Itatia moyo sana.
Mimi nitawasilisha hivi punde mwanzo wangu wa mradi. Naamini tukitiana moyo tutafanikiwa wote kila mtu kwa kiwango chake.
 


Itatia moyo sana.
Mimi nitawasilisha hivi punde mwanzo wangu wa mradi. Naamini tukitiana moyo tutafanikiwa wote kila mtu kwa kiwango chake.

Mkuu Malila unakumbuka zile ekari 60!............hivi sasa nimenunua trekta kwa ajili ya kuchapa kilimo sawa sawa.............aisee raha sana..............

mwaka jana....nimekodi shamba huko kibaigwa.......kuelekea maeneo ya karibu na kiteto..........ekari mia mbili sasa.....mwendo mdundo.....mahindi, alizeti nk.........

Feedback ni muhimu jamani.........
 

Mkuu safi sana,
Nami nataka mwaka huu nitembelee Kiteto/Chunya. Hii mitaa ya Pwani bei zimeharibika vibaya.
 
Tafuta eneo kama ekari mbili mpaka nne chimba kisima kama ulivyoelekezwa na ikiwezekana tenganisha matumizi ya maji binafsi na maji ya biashara. uza maji kwa ajili ya kutafuta gharama za kuendeleza na kukuza mtaji zaidi, lakini ni vizuri ukafuga kuku wa mayai kama 700 ambao nauhakika hutakosa tray 25 kwa siku kwa muda wa mwaka mmoja na nusu, tumia fuga ngombe wa maziwa wawili tu watunze vizuri wakupatie lita 20-30 kwa siku, hata kama mazima haya lipi unahitaji mbolea kwa ajiri ya mbogamboga na kupata bio gas pamoja na matunda achilia mbali kwa sababu maji unayo unaweza kuwa na bwawa dogo la samaki ukaanza kuvuna kila miezi minne mara baada ya kupanga na haya chini ndio mapato kwa miezi sita kwa kila mwezi.


[TD="class: xl22"]maziwa[/TD]
[TD="class: xl23, width: 90"] 1,080,000.00[/TD]

[TD="class: xl22"]mbogamboga[/TD]
[TD="class: xl23"] 600,000.00[/TD]

[TD="class: xl22"]mayai[/TD]
[TD="class: xl23"] 4,500,000.00[/TD]

[TD="class: xl22"]maji[/TD]
[TD="class: xl23"] 450,000.00[/TD]

[TD="class: xl22"]samaki[/TD]
[TD="class: xl23"] 500,000.00[/TD]

[TD="class: xl22"]passion[/TD]
[TD="class: xl23"] 400,000.00[/TD]

[TD="class: xl22"]jumla[/TD]
[TD="class: xl24"] 7,530,000.00[/TD]

Natengeneza mchanganuo ukikamilika nitwawasilisha kwenu, vinginevyo humu ndani kuna vibiashara na mawazo ya watu wengi nayaheshimu sana na yamenisaidia sana.

Kama muoga unaweza ukanunua ardhi kiasi wakati unajipanga.
 
Nimeitafuta hii thread mpaka nimeiona, ina ideas nzuri sana za biashara.
Tayari napractice moja ya idea ambayo niliitoa humu na naona mambo yanakwenda vizuri.
Shauri yenu mnaosoma na kusahau hata mambo mazuri!
 
habari zenu wakuu, nafuatilia uzi huu kwa mda sasa, I am interested to know MBU aliishia wapi na 10m zake.

kwa kifupi mimi nimefaidika na mawazo ya humu, na hivi ninavyoongea nimeshaanza kuwekeza kwenye misitu huko Njombe.

Nawashukuru wote walichangia kwenye uzi huu.

Ningependa huu uzi uwe endelevu, in a way watu walio practice some of the ideas watupe updates
 
Dar_millionare. Mkuu napendaa unijuze zaidi kuusu internet population ku explode by Aug. this year. Inakuaje?
 
Last edited by a moderator:

Mkuu uko Njombe upande upi? Na mimi nimefungua mashamba mengine kule Njombe njia ya Songea. Kuna jamaa anapanda matunda kama hana akili nzuri vile, nimempenda na anayauza Italy.
 
Mkuu uko Njombe upande upi? Na mimi nimefungua mashamba mengine kule Njombe njia ya Songea. Kuna jamaa anapanda matunda kama hana akili nzuri vile, nimempenda na anayauza Italy.

Tunafahamiana na wewe ndio umenisaidia kupata mashamba hayo , hizi ID za JF bwana...
 

Soko la hisa wengi wameishaliwa sana. gawiwo (Dividend) huwa ni kiduchu sana. Huu siyo uwekezaji makini kwa TZ.
 
Mkuu uko Njombe upande upi? Na mimi nimefungua mashamba mengine kule Njombe njia ya Songea. Kuna jamaa anapanda matunda kama hana akili nzuri vile, nimempenda na anayauza Italy.

Ni matunda gani yenye soko ulaya mkuu,that's good kama waTZ tumeanza kuangalia na soko la nje sasa kama wenzetu wakenya walivyolishika soko la ulaya kwa maua Watz tunatakiwa kulishika kwa Matunda na Zabibu
 
matunda yote yana soko Ulaya, tatizo liko ktk kujua tunda lipi linatakiwa wapi na lini na kwa standard gani, sasa matunda yaliyolimwa kwa kilimo hai yana soko sana nje.

Kwa sasa avacado aka parachichi, embe,nanasi,apple ( zote hizi zinamea njombe niliko) zilizolimwa kwa utalaam wa kilimo hai zina soko la nguvu.
 
Habari wana JF; nategemea kupata kiasi cha Tshs millioni 10 hivi karibuni. Ninachowaza ni kufanya biashara tu. Ni biashara nyingi nawaza kufanya lakini naombeni ushauri wenu katika hili. Mi ni kijana je nifanye biashara gani?
 
kuna business consultant humu naona anaweza kukusaidia,
Ushauri wa biashara ni kitu kipana mno, huwezi kurupuka tu kumtajia mtu biashara fulani itamfaa bila kujua mambo kama kiwango cha elimu, mazingira, interests,time, uwezo binafsi(charisma), networking, background yako umeshawahi kufanya jambo gani successful in terms of personal accomplishments, managerial skills and the like.
Mkuu ni vitu vingi sana vinahitajika ili mtu uweze kupata ushauri wa kibiashara.
That's the reason kwamba hata mie sijaweza kukushauri biashara ya kufanya.
 
yaani mimi nikipata hiyo hela ni kufungua ka grocery maana watanzania kw ngano nawakubaki
pia waweza fungua ststionary karibu na vyuo maana inalipa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…