Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

una ujuzi gani ,una uelewa na bishara gani ,ulishawahi kujaribu kuifanya .....
 
Asante kwa ushauri ila ninachohitaji ni kuzungusha mtaji kwa kufanya biashara ndio ardhi inalipa ika kwa baadae sana, mi bado kijana nahitaji kuwa bize na biashara na nipate experience pia. Kwa Ardhi ni kama nazika pesa ili zifufuke baadae

Ndio ulnavyojidanganya?
 
Naunga mkono hoja tena ikiwezekana awekeze milion 5 milioni 5 pembeni maana mgeni huyu
Risk nje nje.
 
Hilo Ndo Tatizo la Tanzania, 98% ni ushauri wa Biashara za Uchuuzi, Biashara ambazo haziwezi kutusaidia kamwe zaidi ya Kusaidia Nchi zainazo zalisha hizo bidhaa, Wanao nufaika na Biashara ya Uchuuzi Pale Kariakoo ni China, India na kazalika

Wazo zuri la Biashara ni kutoka kwako wewe mwenyewe, Usitegemee kutoka kwingineko, haingii akilini Mtu Yuko Dar na Muomba Msaada yuko Arusha unamwambia afungue Grosary, Auze Mitumba, Mara sijui aanzishe tigo pesa, na kazalika,

Nikituko mimi niko Dar halafu nimshauri mtu aliyeko Arusha kwamba fanya kitu fulani, tuacheni utani wakuu,

Kwa Mtoa Maada

- Hutembei?
- Huugui?
- Husomi?
- Huli?
- Huvai?
- Huchezi?

Na zani furusa mara nyingi huja kwa wewe kutumia matatizo yanayo kupata au yanayo pata jamii fulani na wewe kujaribu kupata suluhisho, na hii inaweza kuwa katika nyanja nyingi sana, mkuu angalia matatizo unayo kumbana nayo katika maisha yako ya kila siku na jaribu kutafuta suluhisho, hapo unaweza kuja na wazo bora kabisa la Biashara

Katika swala zima la Ujasirimali hakuna uzoefu,wala elimu, hii sio sahihi kabisa, Unaweza ukawa umesomea Udaktari, lakini mwisho wa siku ukaishia kuwa Mkulima Bora kabisa,

Mwisho kabisa

Usiingie katika Biashara kwa nia ya Kutaka kutajirika, hakika hutakaa ufanikiwe kamwe, Na hakuna biashara isiyo lipa, kila Biashara inalipa, mimi naweza kuwa na Milioni 10 nikaja na wazo la kuuza Karanga watu wataniona kama mwenda wazimu, lakini ukweli ni kwamba kila biashara inafaa ila tataizo ni jinsi ya kuifanya wewe. Kuna watu walianza na Vibanda vya Chips lakini leo hii wanamiliki Migahawa mikubwa kabisa, kuna walio anza na kuuza mchicha lakini leo hii wana suply mboga international,

Unaweza anza na kuku mmoja lakini mwisho wa siku ukawa unamiliki kuku milioni Moja, kila kitu ni hatua, lakini leo hii ukianza biashara kwa lengo la kutaka kuonekana mtaani utaishia kushindwa.

So Utajiri Mara zote ni Matokeo ya Kazi yako wewe, Pesa mara zote ni matokeo ya kazi au huduma yako, leo hii hata Bakhres ukimhoji atakuambia alikua hatarajii kuja kuwa Tajiri mkubwa kabisa Tanzania, Ila imetokea kutokana na juhudi zake na watu kukubali product zake

Hili la kila Muanzisha biashara na kutaka kuwa tajiri ndo inapelekea watu kufanya biashara zisizo eleweka na kushindwa kujua malengo ya huyu mtu ni nini, hebu fikilia Unakuwa unafanya Biashara ya Gest house, halafu hapo hapo una miliki Bajaji mbili, hapa kwa kweli ni vigumu kujua huyu mtu yeye ndoto zake ni kufikia wapi,
 
You are surrounded by simple, obvious solutions that can dramatically increase your income, power, influence and success. The problem is, you just don't see them – Jay Abraham
 
You are surrounded by simple, obvious solutions that can dramatically increase your income, power, influence and success. The problem is, you just don’t see them – Jay Abraham

Chasha chasha,,,, u made my day! Umenifungua akili na mawazo kwa upana wake! Asante kwa yote, nashukuru pia kwa kutumua mda wako kuandika haya yote kwa kina na hakika wewe ni miongoni mwa watanzania wachache waonao jambo na kulifafanua kwa mapana. Have a nice time
 
Zamani watu walikuwa wanamwaga point tupu
 
Nimelipenda sana wazo lako la kununua hisa mkuu.
Hata mimi mwenyewe sikua na hiyo exposure.
Umenipa shule tayari nitataka kuelewa zaidi kuhusu hilo
 
Ml 2,peleka sadaka kanisan/msikitini kwako.
Ml 2 wape wazaz/walezi wako
*Ml 2 saidia familia yako
*Ml 1 mpe mkeo
*Ml 1 kanunueni "pamba"(nguo)
*Ml 2 znazobaki nunua bodaboda
 
Ng`ombe kweli wanalipa ( maziwa sio nyama),lakini jamaa yuko nje ya nchi. Mziki wa kutunza ng`ombe ukiwa mbali,tena ng`ombe wa maziwa si mchezo. Angekuwa Bongo ningemsaidia kumwonyesha kiwanja safi cha kufugia ng`ombe hao.

Kama vipi anunua Toyo huko nje ya nchi aje kuuza Tz kwa bei poa apige cha juu.
 
swala ni kwamba wewe unamawazo gani ili uweze kuchanganya na yetu upate la kufanya maana mimi napata tabu kidogo kuona kama ulikuwa na wazo la kupata mtaji why ukujiandaa unafanyia nini kaa chini jipange uwe na wazo alafu tukusaidie kuliboresha kwa kutumia swot analysis
 
Mimi ni mfugaji, nitakushauri kufuga ngombe kwa mchakato ufuatao:

Ujenzi wa banda = Ths 500,000/=
Manunuzi ya Ngombe 5 x Tsh 900,000 = Tsh 4,500,000/=
(Ngombe utawanunua wakiwa na mimba ya miezi 6)
Kuwahudumia ng'ombe kwa miezi mitatu kabla ya production = Tsh 1,500,000/=
(inahusisha mshahara kwa wafanyakazi wawil + chakula + madawa)

Jumla = Tsh 6,500,000/=

Baada ya Miezi 3;

UZALISHAJI:

Ngombe hawa watakuwa wakitoa maziwa si pungufu ya lita 5 kwa asubuhi na jioni kwa kila ng'ombe. Hivyo uzalishaji kwa siku utakuwa lita 10 kwa siku kwa ng'ombe.

MAPATO

Lita 10 x Ng'ombe 5 = lita 50 kwa siku x Tsh 1000 (bei ninayouza mimi hapa) = Tsh 50,000 kwa siku
Mapato kwa mwezi = Tsh 50,000 x 30 = 1,500,000/=

Gharama za uendeshaji kwa mwezi = Tsh 600,000/=

Faida = Tsh 900,000/= kwa mwezi

BAADA YA MIAKA 5:

Kumbuka ng'ombe huzaa kila mwaka hivyo basi baada ya miaka mitano utakuwa na ng'ombe wasiopungua 25. Kipato chako kwa mwezi unaweza kufikia si pungufu Tsh 18,000,000 endapo utakuwa na ngombe jike 20 kati ya hao 25.

lakini hii inategemea na eneo alilopo na hali ya hewa kwa sasa ni si yakuridhisha saana. Iko poa ila ni long run project.
 
Wadau na mpango wa kuchukua mkopo wa milioni 10 mpaka 15 sasa nauliza je ni biashara gani ama mradi gani ambao naweza kuufanya katika miji ya dar,tanga pwani,dodoma mwanza?
 
Kitu kingine kuwa mbunifu,usiwe copy cat eti kwa kuwa biashara inamlipa fulani name ufanye.
Also waweza hudhuria seminars zap wajasiriamali,if possible ujikite ktk uzalishaji aka viwanda vidogo kutengeneza soap,kupack unga, etc
 
Ushauri wangu, endapo utakuwa tayari umepata idea, hakikisha kuwa faida inayotokana na mauzo kwa mwezi baada ya kutoa matumizi na kodi, itoshereze kulipia mkopo huo na riba yake. Vinginevyo usichukue kabisa mkopo utapoteza nyumba na vitu vyako.
 
Wadau na mpango wa kuchukua mkopo wa milioni 10 mpaka 15 sasa nauliza je ni biashara gani ama mradi gani ambao naweza kuufanya katika miji ya dar,tanga pwani,dodoma mwanza?

Mkuu soma hii mada hapa chini

https://www.jamiiforums.com/ujasiriam...llion-tzs.html

..all the best...........hii mada imenilipa na inaendelea kunilipa, ...kwa kifupi imenitoa!!........nawashukuru wote waliochangia mawazo........
 
Halafu anaweza kutoka na kitabu kidogo cha ideas mseto za ujasiriamali na akala pesa !!!!!!!!!

Samahani bwana Malila nahisi nimechelewa sana hii thread ni toka 2009 lakini nahisi ntafaidika na usaidizi wako,nimeacquire hekari 100 sumbwanga Rukwa na hekari 20 hapo Bungu mkoani Pwani na nina vision ya kilimo kikubwa.....nimefikiria miti natarajia usaidizi wako mkuu wa kiushauri na connections.Email yangu ni willynyakua@gmail.com
 
Back
Top Bottom