the-true-wash
Senior Member
- Oct 14, 2012
- 142
- 109
ziwekeze kwenye kilimo zitakuzalishia faida zaidi ya mara 3
Asante kwa ushauri je ni kilimo gani kinalipa zaidi maana kama ni seasonal kwa kweli itakuwa ngumu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ziwekeze kwenye kilimo zitakuzalishia faida zaidi ya mara 3
Asante kwa ushauri ila ninachohitaji ni kuzungusha mtaji kwa kufanya biashara ndio ardhi inalipa ika kwa baadae sana, mi bado kijana nahitaji kuwa bize na biashara na nipate experience pia. Kwa Ardhi ni kama nazika pesa ili zifufuke baadae
You are surrounded by simple, obvious solutions that can dramatically increase your income, power, influence and success. The problem is, you just dont see them Jay Abraham
Ng`ombe kweli wanalipa ( maziwa sio nyama),lakini jamaa yuko nje ya nchi. Mziki wa kutunza ng`ombe ukiwa mbali,tena ng`ombe wa maziwa si mchezo. Angekuwa Bongo ningemsaidia kumwonyesha kiwanja safi cha kufugia ng`ombe hao.
Mimi ni mfugaji, nitakushauri kufuga ngombe kwa mchakato ufuatao:
Ujenzi wa banda = Ths 500,000/=
Manunuzi ya Ngombe 5 x Tsh 900,000 = Tsh 4,500,000/=
(Ngombe utawanunua wakiwa na mimba ya miezi 6)
Kuwahudumia ng'ombe kwa miezi mitatu kabla ya production = Tsh 1,500,000/=
(inahusisha mshahara kwa wafanyakazi wawil + chakula + madawa)
Jumla = Tsh 6,500,000/=
Baada ya Miezi 3;
UZALISHAJI:
Ngombe hawa watakuwa wakitoa maziwa si pungufu ya lita 5 kwa asubuhi na jioni kwa kila ng'ombe. Hivyo uzalishaji kwa siku utakuwa lita 10 kwa siku kwa ng'ombe.
MAPATO
Lita 10 x Ng'ombe 5 = lita 50 kwa siku x Tsh 1000 (bei ninayouza mimi hapa) = Tsh 50,000 kwa siku
Mapato kwa mwezi = Tsh 50,000 x 30 = 1,500,000/=
Gharama za uendeshaji kwa mwezi = Tsh 600,000/=
Faida = Tsh 900,000/= kwa mwezi
BAADA YA MIAKA 5:
Kumbuka ng'ombe huzaa kila mwaka hivyo basi baada ya miaka mitano utakuwa na ng'ombe wasiopungua 25. Kipato chako kwa mwezi unaweza kufikia si pungufu Tsh 18,000,000 endapo utakuwa na ngombe jike 20 kati ya hao 25.
Wadau na mpango wa kuchukua mkopo wa milioni 10 mpaka 15 sasa nauliza je ni biashara gani ama mradi gani ambao naweza kuufanya katika miji ya dar,tanga pwani,dodoma mwanza?
Halafu anaweza kutoka na kitabu kidogo cha ideas mseto za ujasiriamali na akala pesa !!!!!!!!!