Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

...nikibadilisha hiyo pesa ya madafu kuwa Stg (£) ya malkia nitapata approx £5,000 tu,....

kuna bidhaa yeyote (hot-cake!) inayohitajika sana Tanzania, ambayo upatikanaje wake ni wa tabu huko?
 

Mbu, mtaji wako ni mdogo na biashara za tender zinataka pesa zaidi ya hizo 10m. Ukitegemea tender unaweza kulaza familia kwa njaa na kupata maisha magumu kwani hao serikali kuwasupply si tatizo lakini wakati wa malipo utazungushwa hadi utoe rushwa. Kwa tabia hio mara ya kwanza na ya pili utafanya biashara. Lakini mara ya tatu sija ukawekwa kwa list ya mafisadi maana baada kuzungushwa sana ulipo supply mara ya kwanza na pili basi nawe unakuwa sugu na unaanza kusupply hewa upate pessa za bure nk. Mambo ya tender usiyafikirie nakushauri.
 

Mkuu, sorry niliahidi kukushauri ukikanusha kuwa kukukwapua hizo pesa na umefafanua vizuri. Kaka so far watu wengi wametoa ushauri. Wewe pia umetoa wazo lako la tender, etc. Miaka ya nyuma nikiwa Bongo nilifungua company na kazi zangu kubwa zilikuwa supplies. Ni kweli kazi hii inalipa sana lakini upataji kazi wake ni nimgumu sana. Unatakiwa kuwa na network ya uhakika. Pia kwa supplies hiyo pesa ni ndogo kwani unaweza pata kazi ya kwanza ukatakiwa utumie say 15m na malipo yakaje say 3 weeks after say 3 weeks. Kwa namna hiyo kama huna 'rescue plane' yaani mtu wakukupa pesa kiasi chochote unachotaka muda wowote itakushinda. Ninauzoefu nayo mkuu nilifanya japo kwangu tatizo ilikuwa kupata kazi kwani nilikuwa na rescue plane anytime nikitaka pesa nikaonyesha LPO jamaa fasta ananiwezesha.

Kwakuongezea ushauri wawakuu, mi nakushauri kama unaweza kakodi ha kadhaa Dodoma ulime Zabibu soko guaranteed na Breweries mkuu
 


Good idea japo sijui atachimba katika ardhi/viwanja vya nani hivyo visima. Waweza pia kuchezea kamari, ukaibuka bilionea!
 


utajaribu pia..ila its not guranteed.
Hiyo itabidi uwe unaangalia matangazo ya tenda.....
( kwani ulishawahi ku supply chochote mahali? Kama hujawahi inaweza ikawa ngumu kupata.)
 

10 million unataka kufanya biashara ndogo ndogo?
 
...hivi Quemu ndio wewe QM aka QuickMover?

Naam kaka ndio mimi.

Nafikiri ile biashara Billboards niliizungumzia tu kama mfano. Sidhani kama nilikuwa naifuatilia.
 
10 million unataka kufanya biashara ndogo ndogo?
...naaaaaaaaaam, haba na haba inshaallah nitakijaza kibaba, nami nijekuwa mjasiriamali kamili. Hata Mzee Mengi alianzia na zile peni za Bairo, na Bakhressa alianzia na lamba lamba, kisha mikate...


...Gotcha Bro,...Nikiwa mitaa ya Bongo, zile Billboards siku zote zinanikumbusha ule mjadala miaka miwili iliyopita;

" https://www.jamiiforums.com/habari-hoja-mchanganyiko/4131-home-place-you-dont-whant.html "
 

Good luck bro, Dah usinikumbushe Mengi alikuwa na peni zake zinaitwa (A)laska kitu kama hicho dah walimu wamechapia sana wanafunzi kwenye viganja.
 
Nilipoingia ktk ufugaji wanyama,rafiki yangu aliamua kufanya risk assessment(analysis) ya mradi ule,akaona ni hatari tupu kuufanya.Nilipoingia tena ktk mradi wa miti (ya mbao/poles) jamaa yangu yule akafanya tena risk analysis yake. Miradi yote ninaendelea nayo. Nikamwambia tena nataka kuanza ufugaji wa nyuki,jamaa yangu bado anasisitiza juu ya usalama wa mtaji wake. Watz/waliopata elimu kidogo au sana biashara za kibongo hawaziwezi. Ukianzisha biashara fulani bongo utakaa nayo siku mbili halafu utaanza kupata photocopy nyingi hatua mbili kutoka ulipofungua wewe.

Umeshapewa ushauri mwingi tu na wanajf,ingia tu mambo mengine mbele kwa mbele.
 
Watu wengine bana?......every single coin has value, and therefore anything with value is possible to increase its value at increasing rate!.....10m is a lot of money wa jameni!


Labda kama mtu ana dhana potofu "biashara" ni nini, anaweza kudhani vinginevyo.
Put all that money in one basket is not the way to go; especially for someone entering into business venture as a newbie.
 

Hii kiboko!!

Bila shaka Mkuu huko Bongo, ni uzoefu wa siasa halisi za bongo. Ni projects za walio wengi na hasa tunapoelekea 2010 na zinalipa!.
 
Hii kiboko!!

Bila shaka Mkuu huko Bongo, ni uzoefu wa siasa halisi za bongo. Ni projects za walio wengi na hasa tunapoelekea 2010 na zinalipa!.

"project ya ubunge" 10m.? haitoshi kitu..na kumbuka ni patapotea pia.
halafu nadhani hii idea inakinzana na tunacho advocate hapa JF - si tunataka kupambana na ufisadi? au?
 
Jenga Choo ya kulipia eneo la Kariakoo. Utakuwa na uhakika wa kurejesha gharama zako ndani ya muda mfupi kama ifuatavyo:

Wateja - Akina mama (200 * 100/= * 30days) = 600,000/=
- Akina baba (150 * 100/= * 30days) = 450,000/=
- Watoto/vijana/wanafunzi (200 * 100/= * 30days) = 600,000/=
JUMLA KWA MWEZI 1,650,000/=

Kwa mwaka (19,800,000), kwa miaka kumi (198,800,000/=).

Yaani baada ya miaka kumi utakuwa millionea mkubwa sana, na usisahau kurudi hapa JF na kutushukuru.

NB: Kumbuka, uzuri mmoja kwa biashara hii, haina suala la mvua wala kiangazi. Kila siku biashara inaenda.
 
Last edited:

hii tofauti ya bei kwa akina mama/baba inatokana na nini????
 
Bei ni ile ile Tsh. 100/=, mistake imefanyika kwenye assumption ya akinababa watakao tumia huduma hiyo kwa siku. Anyway fanya 200 badala ya 150.
 

...haswaa!... hapo umemnena kila kitu. Shukrana sana Malila, nimepokea michango ya kutosha (mawazo), ilobakia sasa ni utekelezaji! Shukran.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…