Kwa ufupi nimekuwa ktk sector hii ya miti kwa muda mrefu sana. Naomba mchague wenyewe eneo mnalotaka nishushe data kati zifuatazo;
1; Ardhi ya bei poa iko wapi? na taabu za huko
2; mbegu zinapatikana wapi? na namna ya kuotesha?
3; Aina ya mti(mbegu,growth rate,soko,na sehemu ya kupanda ktk Tz)
4; Msimu mzuri na maandalizi yake.
5; overhead cost baada ya kupanda.
6; Field management.
Leo niwape item ya tatu tu,mimi nimeajiriwa,najaribu kutumia muda wa mwajiri kwa uangalifu.
Kuna miti mingi ila kwa sisi mizuri ni hii; mitiki(10, nje),milingoti boriti(8),milingoti nguzo (10), milingoti mbao (15),mikrismas(cyprus mbao) (25),
pines (12),ktk mabano ni miaka toka kupanda mpaka kuvuna. Soko la mitiki liko nje ya nchi,locally hakuna commercial market mpaka Kilombero wakijenga kiwanda mwakani. Mbegu zinapatikana kwa wakala wa serikali Morogoro,Iringa,Arusha,Tanga etc. Mbegu za mitiki ni ngarambe kuotesha, kilo moja ni Tsh 6000/ na ukifuata utaalam unapata miche 1000 hivi,lakini wajanja wanafanya kienyeji na wanapata zaidi au wanatumia suckers fulani hivi. Bei ya mche kwa sasa ni Tsh 500/ ya chini na 2000/ ya juu pale dar.
Pine/cyprus kilo moja ni Tsh 18,500/ na unapata miche 30,000 mpaka 35,000 inatosha eka hamsini ya miti ya mbao. Mlingoti kilo moja ni Tsh 22,500/ na unapata miche 120,000. Unapanda boriti eka 100 na unapanda miti ya mbao eka 200.
Utamu uko ktk boriti. Eka moja ni boriti 1200,bei ya boriti moja kwa leo hii ni Tsh 15,000/shambani.kwa hiyo eka moja iliyogharimu Tsh 70,000/ kununua ardhi mpaka kupanda itakupa 1200 x 15,000/=( ) toa gharama za fire break mara moja kwa mwaka. Hakuna kupalilia wala kumwagilia.
Mitiki peke yake inakubali pwani,mingine yote ni ktk nchi za baridi. Nimetoa kwa ufupi sana, ila tutaendelea kuelezana kidogo kidogo, item nyingine kesho.