Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Tunashukuru saa kwa hili darasa. Hata mimi ningependa kujua miti ya aina gani unafikiri itaweza kustawi maeneo ya mkoa wa pwani eg mkuranga, chalinze. Kuna eneo nilitembezewa siku za nyuma.


Kwa sababu sisi ni watafutaji na mitaji yetu ni midogo(sina hakika na wewe uko kundi lipi),ni muhimu kuwekeza ktk kitu kinacholipa kwa uhakika. Miti inayostawi pwani ni mingi sana, ila mimi nakushauri kapande mitiki,uanze kidogo kidogo ili ufikie kuwa na estate/msitu. Mitiki soko lake liko nje kwa sasa na baadaye tutakuwa na kiwanda pale kilombero hivyo itakuwa rahisi kuuza pale.

Vinginevyo panda milonge/miarobaini ili uisaidie serikali/jamii kutunza mazingira.
 

Mkuu Next Level,
Hao jamaa unawaita wajanja-wajanja na wako tayari ku-take risk hawajachuna watu ngozi hao kweli? (joke)
Lakini nasikia ukimbiwa jinsi baadhi ya watu walivyopata utajiri unaweza ukaamua ukae masikini maisha yako yote.
 
"You can never earn in the outside world
more than you earn in your own mind."
— Brian Tracy: Personal and business training author, speaker, and consultant

Pamoja na mawazo na ushauri wa wengi, lakini huyo mtaalam ana mchango wake katika swali lako
 


Mkuu, ni ubunifu tu. Opportunity ziko kila mahali. Kinachotakiwa ni kubuni biashara itakayoendana na kiwango cha mtaji na kukupa faida na kukua.

Mfano: DSM kuna Traffic Jam kubwa. Watu wanaspend 2-5 hours kila siku barabarani, Je kuna mtu ameshafikiria mahitaji yao kama ya Chakula, Elimu nk katika muda huo? Selling Hot Humburg, Sandwich with juices take away coulf fetch a lot of money.

Huu ni mfano tu, could be more. Unapobuni mradi ni vema kuangalia walaji au soko. The big the market the better will be your business.
 

bw we watu wanakuzungusha, nunua speedboat mil 4,na ak 47 mbili watume vijana nje pale sinda wakamate meli wakaziweke msasani wewe hapo ulipo unapatana bei, ila angalia bendera inayopepea,hapo unapata hela ya nguvu tena kwa jasho lako.
 
Mkuu Next Level,
Hao jamaa unawaita wajanja-wajanja na wako tayari ku-take risk hawajachuna watu ngozi hao kweli? (joke)
Lakini nasikia ukimbiwa jinsi baadhi ya watu walivyopata utajiri unaweza ukaamua ukae masikini maisha yako yote.

Haha!haha!ha mkuu Zebra.....humo hakuna ngozi kabisa mkuu.....!

Jamani ni wajanja sana...kama nilivyosema biashara yao kubwa ni nguo....mwanzoni walikuwa wanauzia tunduma baadaye dar....but now wamenda hatua nyingine mbele.....wako kule China, Thailand etc...wanaact kama maagent wawafanyabiashara wanatoka bongo na nchi nyingine za Africa wanawalink na suppliers wa mizigo huko apart from supplying mizigo hapa Tz.....so wanapiga hela kinyama!

BWT....Hawajama wanaendesha business zao informally na TRA wanalipa si zaidi ya Ths 500,000 kwa mwaka...wakati hiyo kwa mfanyakazi anayelipwa say 2m kwa mwezi ni kodi ya mwezi mmoja tu!
 
Dah huku kumbe nimelikosa darasa!........yaani nilikuwa nawasiliana na jamaa yangu muda si mrefu kuwa miti iko tayari kwa kuvunwa.......anayosema Malila kuhusu miti ni kweli biashara inalipa...........
 
Hapo kazi kwelikweli mtu mzima,unazo mil10/- cash mkononi.Kuhusu jinsiutakavyo tumia inategea sana historia yako wewe unashughulika na nini na hapo tutapata pa kuanzia maana kama ulizoea kushika laki5 na sasa uazo mil.10,umepata wapi?Kama ni mkopo utawork hard kwa kuwa unajua sio zako na unatakiwa kuzirejesha japo kila mwezi otherwise kama umemwibia mtu/au umechuna ngozi mambo yanakuwa very hard maana pesa yako inakuwa inaandamana na laana.Kazi kwako,nakushauri nenda Dodoma ukalime maparachichi najua yanalipa kwa sana tu.
Naamini nimesomeka.
 
Mbu!

Umeshaanza mchanganuo wa biashara au bado mapema..Still thinking maana ideas za business umepewa nyingi!!??

Usije ukaenda vakesheni ikaisha 10/-..ha ha ha
 
Mbu!

Umeshaanza mchanganuo wa biashara au bado mapema..Still thinking maana ideas za business umepewa nyingi!!??

Usije ukaenda vakesheni ikaisha 10/-..ha ha ha

...nataka kwenda vakesheni Barcelona! 😀
 
...nataka kwenda vakesheni Barcelona! 😀

Speechless!..Tusikumbushiane mabaya, ni muda wa kuinvest kwa sasa.

Barca walituvuruga sana..Kuliko kuenda huko chambua business kadhaa kwenye hii thread na utilie maanani..

Nakuaminia entrepreneur!
 
Kwa Tanzania Mil. 10 unaweza kupata faida ya mwaka kama ifuatavyo:
1. ukanunua used Corola na kuifanya taxi. Mradi huu unakuhakikishia a minimum net revenue ya Shs 2.92 mil per year (8000*365).
2. Hisa za TCC: 10mil. * 10% = 1 mil per year + annual appreciatiatin ya ?%
3. Gunia za mahindi June na kuuza December: 10 mil * 50% = 5mil
4. Ziweke deposit bank upate interest: 10 mil * 7% = laki 7
5. Anzisha ka-saccos kasiko rasmi (zikopeshe at interest): 10 mil * 17% = 1.7 mil
6. Nunua shamba, chimba kisima ufanye kilimo cha umwagiliaji: 10 mil * 2mil
7. NAENDELEA KUBUNGABONGO. WILL GET BACK TO YOU SHORTLY
 

Mbu...huyu Bavuvi anakitu fulani......hizi idea zake si mpya but zinaleta matumaini sana!
 

Fiksiman,

Usimpoteze mwenzako bwana. Hakuna ubunge wa milioni 10 CCM. Ubunge wa CCM kijijini ni kuanzia Tshs. 40,000,000. Mjini kwa mikoani weka mara mbili ya hiyo. Na kwa Jijini Dar es Salaam weka mara tatu au zaidi.

Ila kama ulivyosema sio kosa lako. Ni kwamba hauna uzoefu bado. Uliza wastaafu waliongia kichwa kichwa kugombea ubunge wa CCM wakidhani ubunge bado ni "utumishi wa umma" wakajikuta wanazika pensheni zao zote na kuanza maisha ya tabu.
 
/msitu. Mitiki soko lake liko nje kwa sasa na baadaye tutakuwa na kiwanda pale kilombero hivyo itakuwa rahisi kuuza pale.



Malila nimependa wazo lako, mie nina shamba Mapinga naona watu wamepanda mitiki ila sijaelewa inachukua muda gani kuvunwa? na je gharama zake kwa say eka 3 za kuanzia? na nini faida yake?
 
Hii thread ni nzuri sana. Nimependa sana mchango wa Malila. Anaonekana ni mjasiria mali mzuri sana na generous. Watu wengi wana mawazo ya kibiashara lakini ni wachoyo kuwashirikisha wengine -- most of us are selfish. Lakini Malila ametoa na ndio maana anaongezewa.

Changamoto kwetu wana JF, tubadilishane mawazo na kukuza JF community!

JF is second to none!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…