Tunashukuru saa kwa hili darasa. Hata mimi ningependa kujua miti ya aina gani unafikiri itaweza kustawi maeneo ya mkoa wa pwani eg mkuranga, chalinze. Kuna eneo nilitembezewa siku za nyuma.
Kwa sababu sisi ni watafutaji na mitaji yetu ni midogo(sina hakika na wewe uko kundi lipi),ni muhimu kuwekeza ktk kitu kinacholipa kwa uhakika. Miti inayostawi pwani ni mingi sana, ila mimi nakushauri kapande mitiki,uanze kidogo kidogo ili ufikie kuwa na estate/msitu. Mitiki soko lake liko nje kwa sasa na baadaye tutakuwa na kiwanda pale kilombero hivyo itakuwa rahisi kuuza pale.
Vinginevyo panda milonge/miarobaini ili uisaidie serikali/jamii kutunza mazingira.