Malila plz nitafute pm
Tayari nimetuma pm mkuu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Malila plz nitafute pm
Tayari nimetuma pm mkuu.
By Mgombezi![]()
Mimi ni mfugaji, nitakushauri kufuga ngombe kwa mchakato ufuatao:
Ujenzi wa banda = Ths 500,000/=
Manunuzi ya Ngombe 5 x Tsh 900,000 = Tsh 4,500,000/=
(Ngombe utawanunua wakiwa na mimba ya miezi 6)
Kuwahudumia ng'ombe kwa miezi mitatu kabla ya production = Tsh 1,500,000/=
(inahusisha mshahara kwa wafanyakazi wawil + chakula + madawa)
Jumla = Tsh 6,500,000/=
Baada ya Miezi 3;
UZALISHAJI:
Ngombe hawa watakuwa wakitoa maziwa si pungufu ya lita 5 kwa asubuhi na jioni kwa kila ng'ombe. Hivyo uzalishaji kwa siku utakuwa lita 10 kwa siku kwa ng'ombe.
MAPATO
Lita 10 x Ng'ombe 5 = lita 50 kwa siku x Tsh 1000 (bei ninayouza mimi hapa) = Tsh 50,000 kwa siku
Mapato kwa mwezi = Tsh 50,000 x 30 = 1,500,000/=
Gharama za uendeshaji kwa mwezi = Tsh 600,000/=
Faida = Tsh 900,000/= kwa mwezi
BAADA YA MIAKA 5:
Kumbuka ng'ombe huzaa kila mwaka hivyo basi baada ya miaka mitano utakuwa na ng'ombe wasiopungua 25. Kipato chako kwa mwezi unaweza kufikia si pungufu Tsh 18,000,000 endapo utakuwa na ngombe jike 20 kati ya hao 25.
Mrad mziri ila tatizo lipo kwenye hzo calculations
nijuavyo mimi hakunaga flat rate profit ktk biashara au ujasiriamali
kuna expectations tu... Maana kuna emergenvy hutokea ktk ujasiriamali hvyo faifa inaweza kupanda au kushuka
jamani biashara syo mshahara
Nenda pwani kanunue shamba heka tano is around laki 3 kwa heka jumla 1.5 utaspend utasafisha msitu kwa m1 kwa hizo heka tano then utalima kwa kila heka elfu45 kwa tr3ka then panda matikiti .Gharama jumla utatumia milioni 4.5 then utabakiwa na hakiba .Nenda mkuranga au kibaha.
You are right on this, lakini hii huapply sana kama anataka kufanya iwe formal kidogo! Vinginevyo mi naona 10m ni nyingi sana, ambayo in 10 years inaweza kuwa some billions of money!
Kuna wajasilimali fulani that I know wako hapo k/koo sasa ni billioneas lakini wameanza bunisess kati ya miaka ya late 90s na 2000+ kwa mitaji ya kuanzia Tshs 500k mpaka 5m....lakini business zao ni informal but making a lot of money ni wajanja sana, wao wanauza nguo (most of them) na walianzia kule Tunduma, then mitaji ilipokua wakahamia Dar....k/koo, now wanaown most of the buildings hapo city centre!
Tatizo sisi tulioenda darasani kidogo, huwa tunaanalyse issues mno, mara nyingi we can't take risks...ndo maana tunaishia kuwa average people au mafisadi......kulazimisha utajiri kwa kuchota zilizotafutwa na wengine!
Mbu hiyo hela inatosha kabisa ni nyingi...ila inategemeana na wewe mwenyewe una mtazamo gani, na je, upo tayari kuacha white collar job na kuchafuka na hiyo business mpya au utamwachia mtu mwingine aimanage? etc!
Nguruwe nafuga. Na nilishaweka post yangu hapa inayosema baada ya kuangalia mawazo ya watu mbalimbali humu jamii forum nikaona nianze hivi. Inahusu ufugaji nguruwe. Soma vizuri post yangu. Nguruwe siyo kwa ajili ya pesa ya chapchap. Nguruwe ni uwekezaji wa muda kidogo. Hata hivyo naheshimu mawazo yako.Kafuge nguruwe.
nitafute mkuu 0713774746