Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Nunua magari ya zamani kuna kwa watu bei izsizidi m 1.5 unayapeleka mikoani na kuyauza kwa m3 hapo na kulisafirisha hukosi 700000 kwa kila gari kuna magari mengi ya zamani bongo hayauziki mikoani yanauzika watu bado washamba wengi
 
quote_icon.png
By Mgombezi

Mimi ni mfugaji, nitakushauri kufuga ngombe kwa mchakato ufuatao:

Ujenzi wa banda = Ths 500,000/=
Manunuzi ya Ngombe 5 x Tsh 900,000 = Tsh 4,500,000/=
(Ngombe utawanunua wakiwa na mimba ya miezi 6)
Kuwahudumia ng'ombe kwa miezi mitatu kabla ya production = Tsh 1,500,000/=
(inahusisha mshahara kwa wafanyakazi wawil + chakula + madawa)

Jumla = Tsh 6,500,000/=

Baada ya Miezi 3;

UZALISHAJI:

Ngombe hawa watakuwa wakitoa maziwa si pungufu ya lita 5 kwa asubuhi na jioni kwa kila ng'ombe. Hivyo uzalishaji kwa siku utakuwa lita 10 kwa siku kwa ng'ombe.

MAPATO

Lita 10 x Ng'ombe 5 = lita 50 kwa siku x Tsh 1000 (bei ninayouza mimi hapa) = Tsh 50,000 kwa siku
Mapato kwa mwezi = Tsh 50,000 x 30 = 1,500,000/=

Gharama za uendeshaji kwa mwezi = Tsh 600,000/=

Faida = Tsh 900,000/= kwa mwezi

BAADA YA MIAKA 5:

Kumbuka ng'ombe huzaa kila mwaka hivyo basi baada ya miaka mitano utakuwa na ng'ombe wasiopungua 25. Kipato chako kwa mwezi unaweza kufikia si pungufu Tsh 18,000,000 endapo utakuwa na ngombe jike 20 kati ya hao 25.


Mrad mziri ila tatizo lipo kwenye hzo calculations

nijuavyo mimi hakunaga flat rate profit ktk biashara au ujasiriamali

kuna expectations tu... Maana kuna emergenvy hutokea ktk ujasiriamali hvyo faifa inaweza kupanda au kushuka

jamani biashara syo mshahara
 
  • Thanks
Reactions: amu
Mr mbu Nina mashamba makubwa,naomba mtaji tuingie ubia tufanye kilimo cha kisasa,nakwambia hutajuta me mbu
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Nenda pwani kanunue shamba heka tano is around laki 3 kwa heka jumla 1.5 utaspend utasafisha msitu kwa m1 kwa hizo heka tano then utalima kwa kila heka elfu45 kwa tr3ka then panda matikiti .Gharama jumla utatumia milioni 4.5 then utabakiwa na hakiba .Nenda mkuranga au kibaha.

uko sahii bro, lkn ni watanzania wachache sana ambao wako tayari kufanya kazi hizo za kitwana, wengi wanapenda zile za kuvaaa nguo nyeupe na tai kidha kukaa pembeni na kuangalia fedha zao zikifanya kazi. wao wenyewe hawapendi kushiriki kufanya kazi. other ni good idea.
 
You are right on this, lakini hii huapply sana kama anataka kufanya iwe formal kidogo! Vinginevyo mi naona 10m ni nyingi sana, ambayo in 10 years inaweza kuwa some billions of money!

Kuna wajasilimali fulani that I know wako hapo k/koo sasa ni billioneas lakini wameanza bunisess kati ya miaka ya late 90s na 2000+ kwa mitaji ya kuanzia Tshs 500k mpaka 5m....lakini business zao ni informal but making a lot of money ni wajanja sana, wao wanauza nguo (most of them) na walianzia kule Tunduma, then mitaji ilipokua wakahamia Dar....k/koo, now wanaown most of the buildings hapo city centre!

Tatizo sisi tulioenda darasani kidogo, huwa tunaanalyse issues mno, mara nyingi we can't take risks...ndo maana tunaishia kuwa average people au mafisadi......kulazimisha utajiri kwa kuchota zilizotafutwa na wengine!

Mbu hiyo hela inatosha kabisa ni nyingi...ila inategemeana na wewe mwenyewe una mtazamo gani, na je, upo tayari kuacha white collar job na kuchafuka na hiyo business mpya au utamwachia mtu mwingine aimanage? etc!

uko sahii sana. azingztie " CAMPARI" principle. hiyo itamsaidia. kiuhalisia, kama hutoweza kushiriki katika biashara yoyote ujue umekwisha. you hav at large to particiate kwenye project yoyote.
 
Wakuu ninataka niweke mtaji wa Milioni kumi kwenye biashara ukiwa ni mtaji.. Hapa Nalenga biashara ya jumla ambayo itanifa faida chaputachapu. Nitaka ile biashara ya kuchukua mzigo ninauuza kwa jumla naenda tena kuchukua na kuuza kwa jumla sokoni. Nataka nipate pesa halali ya chapchap. Sitaki biashara yakuzinguana yaani ile ya mama fulani kakopa kisha unamfatilia mwezi mzima kixsha, anakupiga kalenda. Nataka biashara itakayonipa faida ya kutosha ndani ya muda mfupi.

Naomba mawazo yenu wakuu wangu.
 
Kafuge nguruwe.
Nguruwe nafuga. Na nilishaweka post yangu hapa inayosema baada ya kuangalia mawazo ya watu mbalimbali humu jamii forum nikaona nianze hivi. Inahusu ufugaji nguruwe. Soma vizuri post yangu. Nguruwe siyo kwa ajili ya pesa ya chapchap. Nguruwe ni uwekezaji wa muda kidogo. Hata hivyo naheshimu mawazo yako.
 
Unahitaji active investment ( marejesho ya haraka na risk ni kubwa) au passive investment (risk hiko chini sana, marejesho ni ya taratibu sana)?
 
Tafiti sekta ya madini, fanya kununua na kuuza madini kama ya vito au dhahabu.

Simple projection
dhahabu unaweza kupata kwa gramu 50,000-60,000 na unaweza pata faida ya minimum 10,000 kwa kila gram. hivyo kwa mil.10 unapata faida max. mil.2 kwa kila mzunguko.

kwa biashara ya vito unaweza kujaribu madini kama rhodolite na red garnet ambayo yana soko sana arusha unanunua gramu moja kwa max. 5,000 kwa jiwe la gramu 5 na zaidi na wewe unauza mpaka 50,000 kwa gramu kwa jiwe lililozuri ni biashara inayolipa sana.

ila kumbuka ulingo wa madini una pesa nyingi sana hivyo utapeli ni mwingi yakupasa kuwa mwangalifu sana all in all AIM HIGHER AND REACH FOR THE SKIES.
 
kama uko serious, njoo tufanye partnership kwenye kijimradi. Mtaji wa 5M. Unatosha kutengeneza fedha ya kutosha. Unaweza kuni PM au nitafute kwenye +260973050218
 
kama una utayari wa kuvuka mpaka, njoo kwa jirani zetu wazambiani, hiyo fedha zinafunguliwa ofisi mbili ambazo zinaweza kurejesha fedha yako ndani ya mwezi mmoja tu. Zaidi ya hapo ni kutengeneza faida. Ni PM kwa info zaidi
 
PM za nini sasa??!!
Unayesema hostel, labda ila akaangalie mapungufu ya wanafunzi vyuo vyote then awe informed!!!
Kaangalie aina ya maduka ya nguo then fikiria kuhusu nguo za ndani classic
 
njoo tufanye biashara ya vipodozi iringa! tenga 5milion tu kwa kuanzia!
 
Back
Top Bottom