Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Kwa kuwa umekwapua nakushauri mali ya wizi haidumu utapoteza bure pesa zako mrudishie mwenye nazo
 
Mbu hebu jieleze ulichukua ushauri gani kuwekeza hela yako na kukupa faida na changamoto zake,na umeifanya kwa muda gani na je ulianzaje,karibu.
 
Mbu hebu jieleze ulichukua ushauri gani kuwekeza hela yako na kukupa faida na changamoto zake,na umeifanya kwa muda gani na je ulianzaje,karibu.

........in a nutshell, nili/nimewekeza sehemu tatu.

1. Long term; kilimo (mashamba)
-changamoto hapa ni hali ya hewa vs aina ya mazao.
- Faida niwezayo kukwambia ili niwape changamoto wengine ni; ardhi nilipo invest ishapanda thamani kwa 75%

2 . Midterm; Ufugaji kuku wa nyama.
-Faida, mzunguko wa pesa hapa ni monthly.

3. Short term; Usafiri Bajaj mbili tatu,
- Faida, mzunguko wa pesa hapa ni weekly.

BTW, hii thread ni ya muda mrefu kiasi, kiasi kwamba hata graph ya mafanikio imekuwa inapanda mwaka hadi mwaka.

Biashara ni discipline tu, kama muuza njugu anaiweza, why wewe na mimi tusiwe na ustahmilivu wa kutotumia mpaka ule na mtaji?

Hii thread ukiisoma tangu mwanzo, utafaidika sana na ma nguli wa biashara mbali mbali kuliko hata hizi nilizojiamulia mie Mbu
 
Last edited by a moderator:
kwa milioni kumi, weka kwenye akaunti ya profit and loss. baada ya miaka 15 utakuja kutushukuru. usiile tafadhali.
 
Inategemea na ulipo mkuu! Kwa huku kwetu unatafuta viwanja vinne vya maana kwa 2.5m kila kimoja!

Balance inayobaki kwa mshahara wako kazungushie kimoja kimoja wigo! Baada ya miaka mitano uza kimoja ujenge nyumba ya kupangisha! Then hivyo viwili utajua wewe....

Mfanyakazi usijeanza biashara za kushindana na wakinga wenye full time katika kazi zao! Biashara pekee kama upo kwenye ajira ni ujenz wa nyumba za kupangisha tu!

Nawasilisha!
 
au unaweza kufanya partnership au kuziweka kwenye saccos kisha ulimbikize riba (compound interest)
 
Siku nyingine subiri vyuo vinapofungua,kuna baadhi wanafunzi huwa hawasaini boom bila kwanza kulipa baadhi ya michango,kwa vile huwa wanakuwa wamefulia unawakopesha
100000 baada ya mwezi anarudisha 120000, anaweza lipa kabla ya hapo.Uwe na mtu wa hayo maeneo ya chuo wa kukusaidia.Kwa mwezi mmoja unatengeneza faida ya Milioni kama mbili hivi
 
Usije ukarogwa kabisa kabisa. Nilkpoteza 8.5 kwa huo mradi. Tafuta Suzuki Carry mpe mtu na uwe unaifuatilia kwa karibu sana akuletee 50,000 kwa siku. Kama una shamba anzisha ufugaji wa kuku au bata.

How. Much is Suzuki carry now
 
kaka hizo ni changamoto za biashara so zisiwe kigezo cha kuicrash hiyo biashara.
mm naunga mkono wazo hili la mtoa mada ila ninachoweza kukushauri hizo pikipiki zako ziwe za mkataba mean unamtafuta mtu wa uhakika mnaandkishana akuletee elfu 10 kwa siku kwa kipindi cha miez kumi baada ya hapo anachukua pikipiki yeye.Also ww autohusika kwa chchote kuanzia service mpka faini kwa kipindi cha mkataba.
so ukiwa na pikipik 5 ndani ya miez 10 utakua na faida ya sh milioni tano.
 
Weka kwenye fixed deposit for six month ukifikiria cha kufanya
Ukianzisha biashara make sure 70% of ur time uwepo kinyume na hapo inakula kwako mazima, utawapa watu mtaji usipoangalia
 
habarini za mda huu,
nimekopa milion saba na nilicho panga kufanya kimekwama, nataka niitunze hela kwa mda wa miezi mine hadi sita, ndo nii-ingize kwenye mpango, lengo ilikua kuwekeza ktk kilimo, nilikuwa nimepata ekari nne za kukodi lakini kaniomba nisubiri kidogo atoe mazao yake na nitaikodi kwa miaka kadhaa, nimefikiria niiweke ktk fixed acount kwa mda huo, nishaurini kama kuna cha zaidi cha kufanya tofauti na nilivyo waza, kwani hata vifaa vya umwagiliaji nimesitisha kununua, pia mkopo huu nimeukopa kama mtumishi.
karibuni.
 
Mkuu ungekuwa sio mwajiriwa ningekushauri hiyo hela ungenunua mahindi maana mwaka huu hii bidhaa ni issue sana!
Ungefanya hivi mil3 ungekusanya mahindi na kustore na m4 ungeanza mchakamchaka wa kuchukua mahindi shamba na kuleta mjini mpaka mavuno yatakapoisha utakuwa umezalisha m3 kutoka kwenye hii4mil. Baada ya miezi4 hadi5 mahindi ya stock yangekuzalishia m6-9 nyingine.
Hiyo hela usiiweka fixed a/c haitakusaidia coz ni ndogo sana. Na wala usiipeleke direct kwenye mradi wa shamba utadunda.
Hela ya mikopo midogo km hiyo unatakiwa uingize kwenye short term liquidity projects na sio miradi patapotea km kilimo. Otherwise utalipia mkopo hewa mkuu!!
This advise is based from my own experience.
 
Acha kazi unayofanya sasa... Nakuahidi utapata wazo Zuri sana la biashara na lazima utusue. Ili ufanikiwe lazima uwe centred kwenye kitu kimoja cha kufanya. La uwez hivo, nunua hata kiwanja au shamba.

Onyo. Sikushaur umfungulie mtu biashara ya mtaji wa milioni 7 afu umuache aendeshe, utalia na kusaga meno..... Don't trust people with money you have risked a lot to get.
 
Mkuu ungekuwa sio mwajiriwa ningekushauri hiyo hela ungenunua mahindi maana mwaka huu hii bidhaa ni issue sana!
Ungefanya hivi mil3 ungekusanya mahindi na kustore na m4 ungeanza mchakamchaka wa kuchukua mahindi shamba na kuleta mjini mpaka mavuno yatakapoisha utakuwa umezalisha m3 kutoka kwenye hii4mil. Baada ya miezi4 hadi5 mahindi ya stock yangekuzalishia m6-9 nyingine.
Hiyo hela usiiweka fixed a/c haitakusaidia coz ni ndogo sana. Na wala usiipeleke direct kwenye mradi wa shamba utadunda.
Hela ya mikopo midogo km hiyo unatakiwa uingize kwenye short term liquidity projects na sio miradi patapotea km kilimo. Otherwise utalipia mkopo hewa mkuu!!
This advise is based from my own experience.

Wazo zuri sana ingawa nimebanwa mda naweza jaribu, nashukuru mkuu
 
Back
Top Bottom