Habarini wakuu, mimi pia ni kiri ya kwamba huu uzi humekuwa ukinivutia zaidi,ninafarijika na mawazo yanayotolewa, mimi pia nimeanza kilimo cha mazao kama hoho, kitunguu, karoti na nina shamba lenye ekari 2.5 na pia lina vyanzo vya maji vizuri tu, nimeamua kuchimbia mipira chini kwa chini toka kwenye chanzo mpaka kwenye kisima nilichochimba,kwa maana hiyo sasa kilomo changu hakitategemea mvua sana,, sasa basi naombeni ushauri kwa aliyewahi kufanya kilimo cha naamna hii, uzoefu, faida, upandaji uzingatie nini hasa, aina ya mbolea ya kutumia kwenye mazao husika hapo juu,na mengineo