Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Mbu wekeza kwenye nyumba ya kupangisha rental property. Usijenge nunua nyumba vyumba 6 sehemu nzuri uswahilini pangisha waswahili kila chumba unaweza kupata kati shs. 50,000 kwa mwezi jumla sh. 300,000.00 kwa mwaka Tshs. 3,600,000.00 pesa uliyowekeza inaweza kurudi baada ya miaka 3 na miaka itakayofuata ni faida tupu. Usiwekeze kwenye hisa kwani kuna kupanda na kushuka, usianzishe biashara unless una uzoefu au umejipanga vizuri. Kwa ushauri zaidi nipigie 0755394701
 
Babaloo unampoteza mwenzio. Hiyo nyumba iko wapi ya 10m? kama ipo kweli na je ipo in a prime area?, kama sawa then go for it. Kushuka au kupanda kwa shares inategemea na soko na pia hisa za kampuni. ukinunua hisa za Breweries au sigara hao jamaa hisa zao haziporomoki mara kwa mara. Mimi narudia ushauri wangu kwako nunua shares kwenye shule. wekeza kwenye elimu. utakuwa unapata cream na pesa yako iko pale pale na in long run unaweza jikuta unapata ujuzi wa kuendesha shule bcoz lazima u will be a member wa bodi ya directors. I hope ulishaanza huo mchakato wa kutafuta shule!
 
Si anaanza na day care center mkuu!!!!!!!! Vishule vingi hadi Tusiime vimeanza na chumba kimoja nyumbani kwa mtu, au Sahara p/s pale Mabibo ilianza na wanafunzi 5 tu nyumbani kwa mtu kama tuition fulani. Pole pole atapata uzoefu na kuanza kukua. Kumbuka mbuyu ulianza kama mchicha. Ni maoni tu mkuu wangu.

Natanguliza shukurani nyingi sana kwa info zako...yaani umenitia moyo sana wa kufikiria kufanya biashara haswa nikiangalia kuwa kuna uwezekano wa kufanya kwa kuanzia MIL 10....

Kuhusu biashara ya miti kwangu haitowezekana kutegemea na umri......lakini nalifikiria sana suala la kukamua mafuta ya alizeti au mawese lakini kama ujuavyo nchini na uhaba wa umeme.

Namalizia kwa kutoa shukurani kwa MBU na we mkulu MALILA na wengineo kwa hili darasa...GOD BLESS YOU ALL
 
asante Sana,
Kwa mtindo wa kamata miche,kisha nduki shambani,lazima mle hasara taslimu. Kitaalamu unatakiwa kufanya root prunning mwezi mmoja au hata wiki tatu kabla ya kupanda,hasa kwa maeneo yenye mvua kidogo au za wastani.

Mche ulio ktk kitalu,mizizi yake inakwenda chini na kushikamana na udongo mwingine. kwa hiyo ni lazima/muhimu kuhakikisha mizizi inakatwa na kisu kikali kwa umakini mkubwa na baada ya hapo umwagiliaji unaendelea mpaka vidonda vya mizizi vipone. Kazi hii hufanyika pale ktk kitalu.Hii ndio root prunning kwa ufupi. Miti iliyofanyiwa root prunning mwezi mmoja kabla ikienda shambani inapona yote. Usipofanya root prunning, unapohamisha miche kupeleka shamba,mingi hufa kwa sababu,ilipata vidonda na wakati huo huo umebadilisha mazingira yake,effect of PH,drought,temperature etc.

Sababu nyingine ni size ya shimo,kina na upana,water logging etc.
 
i will save this
Kwa ufupi nimekuwa ktk sector hii ya miti kwa muda mrefu sana. Naomba mchague wenyewe eneo mnalotaka nishushe data kati zifuatazo;

1; Ardhi ya bei poa iko wapi? na taabu za huko
2; mbegu zinapatikana wapi? na namna ya kuotesha?
3; Aina ya mti(mbegu,growth rate,soko,na sehemu ya kupanda ktk Tz)
4; Msimu mzuri na maandalizi yake.
5; overhead cost baada ya kupanda.
6; Field management.

Leo niwape item ya tatu tu,mimi nimeajiriwa,najaribu kutumia muda wa mwajiri kwa uangalifu.
Kuna miti mingi ila kwa sisi mizuri ni hii; mitiki(10, nje),milingoti boriti(8),milingoti nguzo (10), milingoti mbao (15),mikrismas(cyprus mbao) (25),
pines (12),ktk mabano ni miaka toka kupanda mpaka kuvuna. Soko la mitiki liko nje ya nchi,locally hakuna commercial market mpaka Kilombero wakijenga kiwanda mwakani. Mbegu zinapatikana kwa wakala wa serikali Morogoro,Iringa,Arusha,Tanga etc. Mbegu za mitiki ni ngarambe kuotesha, kilo moja ni Tsh 6000/ na ukifuata utaalam unapata miche 1000 hivi,lakini wajanja wanafanya kienyeji na wanapata zaidi au wanatumia suckers fulani hivi. Bei ya mche kwa sasa ni Tsh 500/ ya chini na 2000/ ya juu pale dar.

Pine/cyprus kilo moja ni Tsh 18,500/ na unapata miche 30,000 mpaka 35,000 inatosha eka hamsini ya miti ya mbao. Mlingoti kilo moja ni Tsh 22,500/ na unapata miche 120,000. Unapanda boriti eka 100 na unapanda miti ya mbao eka 200.

Utamu uko ktk boriti. Eka moja ni boriti 1200,bei ya boriti moja kwa leo hii ni Tsh 15,000/shambani.kwa hiyo eka moja iliyogharimu Tsh 70,000/ kununua ardhi mpaka kupanda itakupa 1200 x 15,000/=( ) toa gharama za fire break mara moja kwa mwaka. Hakuna kupalilia wala kumwagilia.

Mitiki peke yake inakubali pwani,mingine yote ni ktk nchi za baridi. Nimetoa kwa ufupi sana, ila tutaendelea kuelezana kidogo kidogo, item nyingine kesho.
 
Prime Dynamics sijampoteza Mbu, ungeuliza ukafahamishwa nyumba hiyo inaweza kupatikana kama unajua mbinu za real estate namna ya kusaka dili za nyumba kwa bei poa mbinu hizi huwa nawapa wateja wangu na mmoja amenunua nyumba kwa bei poa hivi karibuni. Kwa ushauri zaidi nipigie simu 0755394701
 
...mjadala umekuwa mzuri sana, Kwa faida ya wengineo pia.
Vipi urahisi/ugumu wa biashara ya Uzabuni, "Tender to supply..."

Kwa muhtasari, nini demand kubwa ya wakazi wa mijini compared na wale wa 'vijijini'
 
Natanguliza shukurani nyingi sana kwa info zako...yaani umenitia moyo sana wa kufikiria kufanya biashara haswa nikiangalia kuwa kuna uwezekano wa kufanya kwa kuanzia MIL 10....

Kuhusu biashara ya miti kwangu haitowezekana kutegemea na umri......lakini nalifikiria sana suala la kukamua mafuta ya alizeti au mawese lakini kama ujuavyo nchini na uhaba wa umeme.

Namalizia kwa kutoa shukurani kwa MBU na we mkulu MALILA na wengineo kwa hili darasa...GOD BLESS YOU ALL
Unaweza kuifanya biashara hii hata kama unakaribia kwenda mbinguni, kule vijijini watu wanauza misitu yenye miti inayokaribia kuvunwa kwa bei ya kutupwa kabisa, unanunua kamsitu kako, na wewe unatafuta mnunuzi tena unauza au unavuna mwenyewe na unapata faida kubwa,na ukaachana na taabu za tra na ndugu zao. Na kama una vijana/wadogo zangu wafundishe kazi hii, kwa sababu haihitaji usimamizi wa kila siku, kwa mwaka mara moja tu basi. Sehemu kubwa ya mwaka miti inapogoma yenyewe huko shambani.
 
...ha ha ha!, Malila acha dua mbaya bana.
Mwana Tanu penye nia pana njia. Kwakweli Mkulima Malila ametupa darasa lisilo na shaka.
Mw'mungu awapeni nyote umri mrefu..
 
Pretty Maji ni biashara kichaa mimi naifanya inanisumbua sana. Anaweza kuchimba kisima au visima akakuta maji yote hayafai kunywewa au kutumiwa na binadamu maji mengine ya ardhini yana sumu. Hata ukijaribu kwenda Benki kaombe mkopo unataka kuanzisha mradi wa maji watakwambia hiyo ni biashara kichaa hawawezi kukukopesaha, tulishapitia huko tunajua akiwekeza huko ameingia mkenge.
 
I have a very good business idea... favorable rate of return and very low risk... it has ready market and guarantee to redeem the loan....the idea is only up for sale ..... unless otherwise my advice is for you to go and buy a franchise of any type....
 
mimi nakushauri kuwa invester maana michakato ya biashara huwa ina mikanganyiko mingi sana

na moja ya nyanja ambayo unaweza kuwekeza ni local real estate ya kibongo kwanini

1.soko ni la uhakika sasa hivi asilimia 99 ya wabongo akili yao iko katika kujenga si utawakamata nina uhakika
2. hauwekezaji huo hauna presha yaani uko zako ulaya na unasimamia kwa mbali kama rimote

cha kufanya nunua kiwanja chenye hati kabisa na ndio biashara yenyewe kwani nyumba ya 10m hakuna

pili hakikisha kuwa unaweka fence japo ile ya kuzungushia nyaya

tatu subiri ipite miezi sita tu au mwaka then kiweke sokoni kaka

madalali kibao ukiwapatia ofa yako tu wanachacharika kweli

mwisho usiwekeze 10m yote wewe nunua cha 7 au 8m

utakuwa na uhakika wa kuuza kati ya 12, 13, 14 au 15m

angalizo!

usiwe na haraka wakati wa kukiuza taratibu la sivyo utauza kwa bei ndogo

USHUHUDA
Kuna kakiwanja nilinunua mwaka 2007 kwa 3m na sasa ninaenda kukiuza wakati wowote kwa 40 au 45m

any swali nicheki kwa 0713 32 77 13
 
...ha ha ha!, Malila acha dua mbaya bana.
Mwana Tanu penye nia pana njia. Kwakweli Mkulima Malila ametupa darasa lisilo na shaka.
Mw'mungu awapeni nyote umri mrefu..
Ameni.
 
Thread imefunika ile mbaya hadi nimechelewa kutoka ofisin leo saa hii ni 2038 hrs si mchezo.
Mbarikiwe woooote kwa michango muruwa ya kuelimisha, spesho thenx to malila, na mbu kwa kuuliza swali endelevu kiasi hiki
naamini majibu na michango mbalimbali imekuwa ya faida kwa wengi na katika nyanja nyingi sana.
Endeleeni na moyo huo wa kuelimisha jamii, Mungu atawalipa.

Amani yetu inatumiwa vibaya.
 
mimi nakushauri kuwa invester maana michakato ya biashara huwa ina mikanganyiko mingi sana

na moja ya nyanja ambayo unaweza kuwekeza ni local real estate ya kibongo kwanini

1.soko ni la uhakika sasa hivi asilimia 99 ya wabongo akili yao iko katika kujenga si utawakamata nina uhakika
2. hauwekezaji huo hauna presha yaani uko zako ulaya na unasimamia kwa mbali kama rimote

cha kufanya nunua kiwanja chenye hati kabisa na ndio biashara yenyewe kwani nyumba ya 10m hakuna

pili hakikisha kuwa unaweka fence japo ile ya kuzungushia nyaya

tatu subiri ipite miezi sita tu au mwaka then kiweke sokoni kaka

madalali kibao ukiwapatia ofa yako tu wanachacharika kweli

mwisho usiwekeze 10m yote wewe nunua cha 7 au 8m

utakuwa na uhakika wa kuuza kati ya 12, 13, 14 au 15m

angalizo!

usiwe na haraka wakati wa kukiuza taratibu la sivyo utauza kwa bei ndogo

USHUHUDA
Kuna kakiwanja nilinunua mwaka 2007 kwa 3m na sasa ninaenda kukiuza wakati wowote kwa 40 au 45m

any swali nicheki kwa 0713 32 77 13

...in 4yrs thamani imepanda zaidi ya mara 15?! ..maeneo ya Kibada nini?
 
Mimi ni mfugaji, nitakushauri kufuga ngombe kwa mchakato ufuatao:

Ujenzi wa banda = Ths 500,000/=
Manunuzi ya Ngombe 5 x Tsh 900,000 = Tsh 4,500,000/=
(Ngombe utawanunua wakiwa na mimba ya miezi 6)
Kuwahudumia ng'ombe kwa miezi mitatu kabla ya production = Tsh 1,500,000/=
(inahusisha mshahara kwa wafanyakazi wawil + chakula + madawa)

Jumla = Tsh 6,500,000/=

Baada ya Miezi 3;

UZALISHAJI:

Ngombe hawa watakuwa wakitoa maziwa si pungufu ya lita 5 kwa asubuhi na jioni kwa kila ng'ombe. Hivyo uzalishaji kwa siku utakuwa lita 10 kwa siku kwa ng'ombe.

MAPATO

Lita 10 x Ng'ombe 5 = lita 50 kwa siku x Tsh 1000 (bei ninayouza mimi hapa) = Tsh 50,000 kwa siku
Mapato kwa mwezi = Tsh 50,000 x 30 = 1,500,000/=

Gharama za uendeshaji kwa mwezi = Tsh 600,000/=

Faida = Tsh 900,000/= kwa mwezi

BAADA YA MIAKA 5:

Kumbuka ng'ombe huzaa kila mwaka hivyo basi baada ya miaka mitano utakuwa na ng'ombe wasiopungua 25. Kipato chako kwa mwezi unaweza kufikia si pungufu Tsh 18,000,000 endapo utakuwa na ngombe jike 20 kati ya hao 25.
Hulipi kodi?? Au imejumuishwa kwenye gharama za uendeshaji??
 
Hulipi kodi?? Au imejumuishwa kwenye gharama za uendeshaji??

Unatakiwa kufikiri biashara ambayo hutalipa kodi; mfugaji halipi kodi bali ukianza ku-process hayo maziwa utaanza kulipa kodi.
 
Unaweza kuifanya biashara hii hata kama unakaribia kwenda mbinguni, kule vijijini watu wanauza misitu yenye miti inayokaribia kuvunwa kwa bei ya kutupwa kabisa, unanunua kamsitu kako, na wewe unatafuta mnunuzi tena unauza au unavuna mwenyewe na unapata faida kubwa,na ukaachana na taabu za tra na ndugu zao. Na kama una vijana/wadogo zangu wafundishe kazi hii, kwa sababu haihitaji usimamizi wa kila siku, kwa mwaka mara moja tu basi. Sehemu kubwa ya mwaka miti inapogoma yenyewe huko shambani.

This is very true na inalipa sana....kwani ninaifanya hii biashara sasa hivi................

Ni Vizuri tukapeana UPDATES kutokana na mawazo ya hapa...................New update kwa Wakuu wote kwenye huu mjadala............lile shamba langu ekari 60..........limeleta neema kutokana na mawazo ya hapa hapa (mazao na mifugo)..........na sasa napanua wigo wa ujasiriamali with my Newly bought TRUCK! Thank You Malila, Thank you Mbu na Thank you (yule jamaa aliyeshauri kuhusu mradi wa Ngombe wa maziwa)..............it worked for me I'm sure it will work for you guys as well

Trust me...Malila I will look for you ili tuje ongea zaidi haya mafanikio na mikakati zaidi
 
Yule jamaa wa ng`ombe anaitwa Mgombezi kwa jina la humu jamvini,ila sasa mimi namfahamu kwa majina yote na sura yake,tulionana chai day pale Dar. Nikushukuru kwa kurudi jamvini na kutupa updates za kutia moyo, binafsi nimefanikiwa sana kupitia jf. Siku tukionana uso kwa uso patakuwa hapatoshi !!!!!. Nimshukuru sana Mbu kwa sababu wengi tumetafutana baada ya michango kupitia thread hii.

Kwa sasa niko tight,nakamilisha maazimio ya chai day. Misitu inalipa sana, na ukionja huachi.
 
wajameni eeh, nimebahatika "kupata" mahala ka-Mtaji. Ni kiasi cha shs. milioni kumi tu, (10,000,000/=) za Kitanzania.

Nipeni mapendekezo nizi invest wapi, kivipi na matarajio ya faida.
(i.e biashara gani inalipa (plus location), kwa muda gani, na SWOT analysis zake)

..kama hutaki makubwa angalia treasury bills za BOT,zina average at least 5% kuna za siku 35,91,182 na 364 days,nafikiri ni safe investment maana default ni almost zero kwa serikali,minimum bid ni 5million kwa hiyo pesa yako 10m unaweza kutengeneza laki tano kwa mwaka na kwa sasa imefika 6.6% maana serikali imechacha na hiyo ni 660000 kwa mwaka ila kumbuka kuna withholding tax ya 10%,ukitaka details zaidi ya siku za minada na info nyingine angalia www.bot-tz.org then click financial markets then ingia treasury bills na hapo unaweza kuangalia tarehe zote za minada iliyopita na inayokuja,the catch lazima ujue hivi vitu vinavyofanya kazi na ni very simple so educate yourself!
 
Back
Top Bottom